Yohimbine
JF-Expert Member
- Jan 6, 2019
- 844
- 1,754
Habari za uzima wapendwa poleni na majukumu ya wiki nzima.
Turudi kwenye mada yetu, hivi sasa ukiangalia kumekuwa na wimbi kubwa sana la wahitimu wanaomaliza masomo yao ya elimu ya juu lakini ufinyu wa ajira umekuwa mkubwa sana na kusababisha watu wengi kuwapo mtaani bila ya kuwa na shughuli maalumu ya kufanya lakini siku za karibuni kumeibuka wimbi kubwa la wanasiasa wanaowaambia vijana wajiajiri angali wao wenyewe walisomeshwa na wameajiriwa na wananchi lakini kazi yao kubwa ni kupigana vijembe na kuongea mambo dhaifu yasiyo hata na mustakabali kuhusu maisha ya wananchi wanaowaongoza.
Nini kifanyike?
Serikali iangalie uwezekano wa kukaa na wadau wa elimu waanzishe somo la ujasiriamali liwe linafundishwa mashuleni tena liwe somo la lazima kwa mfano unapoanza kidato cha tano au hata kidato cha tatu mpaka mwaka wako wa mwisho wa chuo kikuu na pia katika vyuo vya ufundi uwe unalisoma hili somo hii itasaidia sana kupunguza kwa kiasi chake tatizo hili la ajira.
NAWASILISHA