Sabalkher wadau,
Kutokana na ripoti mbili zote za mchanga wa madini zilizowasilishwa kwa mh Rais, tumeona tunaibiwa mchana kweupe mpaka dunia inatushangaa.
Tumepoteza trilioni za shilingi katika sekta ya madini.
Naishauri serikali ihakikishe inamaliza migogoro hii ya madini inayoendelea hivi sasa. Baada ya hapo ikiwezekana tufute kabisa kampuni zote za madini na iundwe kampuni moja kubwa ya madini itakayosimamiwa na serikali.
Najua fika kwamba kuanzisha kampunia ya madini kunahitaji mtaji mkubwa lakini serikali ina nguvu kubwa. Tuchukulie mfano kidogo tuu kwenye uwekezaji ktk bomba la gesi ambao umegharimu kiasi cha zaidi ya dola bilioni moja za kimarekani ambayo ni zaidi ya trilioni 2 za kitanzania. Ikiwa tumeweza kutekeleza mradi mkubwa namna hii, hata madini tunaweza kuthubutu kuingia.
Tutaanza kwa kutumia teknolojia ya kawaida na zana kadhaa za kisasa na muda unavyokwenda tutaendelea kuboresha zana zetu.
Tusipozingatia hili tutaendelea kuibiwa kwani mwizi akishazoea kuiba hawezi kuacha; Mwl Nyerere alisema Mtu akishazoea kula nyama ya mtu hawezi kuacha.
Ushauri unazingatia pia miaka ijayo ambapo huenda Mh Magufuli akawa ameshamaliza muda wake hivyo wakaibuka wajanja wengine na kuendelea kuitafuana nchi yetu.
Nawasilisha