Serikali ianzishe kampuni zake za uchimbaji madini tuondokane na unyonyaji huu

Mkuu wazo la kuanzisha kampuni hizo sio baya kama nilivyotangulia kusema, tatizo ni hujuma.Nikuambie kitu mkuu, duniani hakuna nchi kama nchi inayochimba madini yake yenyewe.Afrika ya kusini De Beers ndio wanaochimba alimasi na dhahabu Barrick Gold.

Mkuu yapo makampuni kumi yanayochimba dhahabu duniani, kubwa likiwa Barrick Gold na kumi ya alimasi, kubwa likiwa De Beers.Haya yote mkuu ni makampuni binafsi na yote yana uhusiano wa karibu sana, kwa hiyo ukishatibuana na moja umetibuana nayo yote. Kama nilivyosema tusiruhusu kuibiwa, ila tuwe equal partners na hayo makampuni.Ipo kampuni moja ambayo ndiyo inachimba alimasi ya Botswana, inaitwa DEBSWANA. Hii kampuni taarifa iliyopo ni kwamba ina terms nzuri sana na serikali ya Botswana.Sio vibaya tukipata uzoefu wa Botswana ili wakati wa negotiations na Barrick tuwe na mifano hai ambayo ni implementable.

Sawa mkuu, kama hivyo ndivyo. Nakubali hoja ya kuwa equal partners. Nasikia hata Angola ni nchi inayonufaika sana na madini yake. Tuchukue uzoefu kutoka nchi hizi mbili; Angola na Botswana.
 
Back
Top Bottom