1;Waziri mhusika alisema hawana upungufu wa madaktari na kumbe waliopo wanaweza kuwa hata flying doctors.
2;Hiyo iko marekani tu ambako tofauti ya maisha ya daktari wa mjini na yule wa kijijini ni ndogo sana ndugu,unajisikia vipi mmesoma chuo kimoja mnafanya kazi moja halafu unamuona mwenzio ana usafiri wewe kila siku unaazima baiskeli ya katibu kata?
Udaktari sio witu kwani watu wanalipia upto 30m za heslb,makato per month karibu 300k halafu unataka mtu akae huko kijijini.
3;Huko kijijini kielimu wanapaweza CO na nurses tu kulingana na vitu wanavyopaswa kufanya kwa majukumu yao na mazingira halisi ya vijiji vyetu.
What is the logic ya daktari kwenda mkanyenye dispensary kila siku anatibu malaria ya vichocho tu?Hakuna procedures huko,update ya shule hakuna mwisho wa siku anaishia kuwa mnywa vibuku tu kama wananzengo wengine.
Waboreshe mazingira ya kazi vijijini,waboreshe mapato ya waendao vijijini,waboreshe miundombinu ya vijijini then everyone atapakimbilia huko na ndipo unaweza sema udaktari ni wito