Serikali ianze ku-export madaktari na manesi nchi zingine

Serikali ianze ku-export madaktari na manesi nchi zingine

Tanzania ina madaktari na manesi wengi waliomaliza na wanaoendelea kusoma.Ni vizuri kuanza kuingia mikataba na nchi zenye uhitaji wa manesi na madaktari na kutoa vibali vya madaktari kwenda nje kwenye hizo nchi kufanya kazi za udaktari na unesi.
we kweli akili ulizonazo zinakutosha ww mwenyewe huku ileje madaktari hawapo au ukiwa ccm haujali wengine
inabidi turudishe azimio la arusha ilikurudisha kujaliana
 
nafikiri huna takwimu na wala hukutaka kutumia hata dakika nne kutafuta takwimu. WHO inapendekeza uwiano wa daktari:wagonjwa isiszidi 1:1,000 lakini kwa hapa Tanzania uwiano upo 1:10,000+. Ni kawaida kukuta hospitali za mikoa kuwa na daktari bingwa mmoja sasa sijui jeuri ya kusema tuna madaktari wengi hadi serikali i-export unaipata wapi. labda kama kwako kila anayevaa koti jeupe maeneo ya hospitali/zahanati/kliniki ni daktari
Kuna uhaba wa madaktar ndio ila nahisi wingi wa madaktar mtaani na manesi wasio na ajira ndio umempa wasiwasi mtoa mada na kushauri hivyo.
 
Sidhani kama nchi yetu imejitosheleza kiivyo! Unaona ni wengi kwasababu wamejazana kwenye miji. Vijijini huko hospitali na zahanati hawana madaktari.
Kuna mdada alisoma unesi tena diploma akapangiwa kijiji fulani hivi. Kufika huko hakukuta mtu yeyote juu yake., ko yeye ndo akawa daktari huko. Imagine, nesi wa diploma ndo kawa daktari! Na hii ni mwaka jana mkuu.
Madaktari wengi wanakimbia wito wao na kwenda kuhudumia watu hadi huko vijijini, wanataka life mterezo mijini.

Swali: ile doctors without borders iko nchi zote? Au ni Marekani tu?
Nafuu huyo ana diploma huku kwetu zahanati wanaohudumia wagonjwa ni manesi wa cheti wale waliosomea unesi miaka miwili. Nesi wa kiume ndio amejivika udaktari.
 
Nafikiri wataalamu wataalamu mbali mbali wanatakiwa wapewe hiyo fursa. Maana serikali yetu inaonekana ina wataalamu wa kutosha na ndio maana imegoma kuajiri.
MF. Shahada za udaktari wa mifugo na wataalamu wa mifugo, Uvuvi, kilimo, wataalamu wa udongo (Agronomists), Agricultural Engineering, Irrigation engineering etc. Tunatoka chuo kimoja tu Tanzania nzma (with exception of Agricultural Engineering, Irrigation and Agriculture General) na inaonekana tume-exceed capacity ya kuajiriwa na serikali, Tayari Batch Mbili tupo mtaani na Batch nyingine unafuata.
 
Sidhani kama nchi yetu imejitosheleza kiivyo! Unaona ni wengi kwasababu wamejazana kwenye miji. Vijijini huko hospitali na zahanati hawana madaktari.
Kuna mdada alisoma unesi tena diploma akapangiwa kijiji fulani hivi. Kufika huko hakukuta mtu yeyote juu yake., ko yeye ndo akawa daktari huko. Imagine, nesi wa diploma ndo kawa daktari! Na hii ni mwaka jana mkuu.
Madaktari wengi wanakimbia wito wao na kwenda kuhudumia watu hadi huko vijijini, wanataka life mterezo mijini.

Swali: ile doctors without borders iko nchi zote? Au ni Marekani tu?
Wale ni Volunteers!
Mara nyingi husaidia nchi zilizo chini sana kiuchumu na zenye Political conflict.
 
Ugawe chakula wakati wewe huna cha kukutosha???
 
inauma sana ndugu yangu..ninatazama ajira za waalimu wa sayansi pia sioni jibu lao....itabidi watu waachane na kusoma tu wakalime mapema
 
sasa daktari au nesi anahitaji kibali cha kwenda nje? mkuu upo sawa kweli? hizo ni fursa binafsi ukiona Tanzania michosho unatafuta fursa hizo mwenyewe mitandaoni sio lazima kila kitu serikali...hizo ni dalili za ulelemama...
 
Hivi kwa nini watu kila kitu tunategemea serikali itufanyie? Sasa suala la kuajiriwa nje ya nchi unataka serikali iwatafutie mikataba. Mi naona kama mtu ana interest ya kufanya kazi nje ya nchi aende kwa mujibu wa taratibu za uhamiaji. Akichoka kufanya kazi nje ya nchi atarudi nchini. Serikali ikikufanyia mchakato wowote lazima kuwe na figisu figisu nyingi.
Jua wasomi wengi ni wafaidika wa Mkopo wa Elimu ya juu....! Na ni vigumu serikali kuwa ruhusu waende kufanya kazi nje ya nchi.
Plus issue ya afya ni issue sensitive kwenye nchi yetu kwakua wataalamu wa kada hiyo hawatoshi kwa hiyo serikali haiwezi kubwa ruhusu waende kufanya kazi nje ya nchi.
Lakini pia serikali haiwezi kuwaajiri wachache tulionao na ndio maana muanzisha Uzi ameomba serikali iwaruhusu wakafanye kazi nje ya nchi kwa kua uwezo wa serikali kuwaajiri ni Mdogo.
 
Mpaka tar ya leo kuna zaid ya drs 3500 wapo mtaan
Serikali inasema ina uwezo wa kuajir drs 500 tu kwa mwaka
Kwa maana hiyo kuna drs 3000 watabaki mtaani
Ndio maana mleta mada kaja na wazo lake hili muhim,ni kweli kuna uhaba wa drs nchini lakin serikali haioni umihim wa kuwaajir,hivyo wanazunguka mtaan watu waliosoma kwa taabu 5yrs +1 interniship
Ni muhim serkali iruhusu vijana wakatafute maisha nje ya nchi na sio kuwapa stress na kuwakatisha tamaa
 
sasa daktari au nesi anahitaji kibali cha kwenda nje? mkuu upo sawa kweli? hizo ni fursa binafsi ukiona Tanzania michosho unatafuta fursa hizo mwenyewe mitandaoni sio lazima kila kitu serikali...hizo ni dalili za ulelemama...
Vinahitajika vibali .Kenya hapo madaktari waliendesha mgomo serikali ya Kenya ikaomba Toka Tanzania kuwa iwape madaktari serikali ikagoma kuwapa madaktari vibali vya kwenda kufanya kazi Kenya.Kenya ikaona isiwe kesi ikaagiza madaktari mamia Toka Cuba.Hadi Leo wako Kenya .Serikali inawalipa mshahara kwa Mwezi dola elfu nne ambazo Ni sawa na shilingi za Tanzania milioni nane .Kenya ilitupa fursa tukaiacha kwa porojo za kisiasa
 
Back
Top Bottom