Gilbert Prudence
Member
- Oct 30, 2018
- 35
- 62
Kuna hatari kubwa ya maandamano ya vijana kwa sababu ajira ni chache na mikakati ya serikali kupambana na tatizo hili ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa tatizo.
- Sioni mikakati madhubuti ya kusaidia vijana wanaomaliza kidato cha nne na kufeli.
- Sioni mikakati ya kusaidia vijana waliomaliza vyuo vya kati na vyuo vikuu inayoweza kupunguza machungu waliyonayo licha ya ajira chache zinazotolewa karibu na uchaguzi, na ni kama asilimia 20 tu ya wahitimu wanaopata ajira.
- Wanao maliza kidato cha nne na kufeli wapelekwe vyuo vya ufundi moja kwa moja kujifunza kazi za mikono. Serikali igharamie au wapewe mikopo kwa kuwa wana uhakika wa kulipa. Hili linawezekana ikiwa mianya ya rushwa na ufisadi itadhibitiwa.
- Kuna njia nyingi za kukomboa vijana waliohitimu vyuo:
i. Kuanzishwe benki ya vijana, vijana wakopeshwe kwa vigezo na masharti nafuu ili kuanzisha biashara au huduma mbalimbali kulingana na taaluma zao.
ii. Serikali ianzishe mfumo wa ajira za mikataba ya miaka mitano, na iwe mwisho miaka 10 mtu kuajiriwa serikalini. Zaidi ya hapo, aende taasisi binafsi, lakini mishahara iwe mizuri na mtu apewe kiinua mgongo kizuri ili aendeleze maisha nje ya mfumo wa ajira za serikali. Njia hii ya mikataba itasaidia pia waliosoma kwa mikopo ya serikali kulipa madeni yao na kutoa fursa kwa wadaiwa wengine pia kuajiriwa na kulipa pia.
iii. Wigo wa ajira upanuliwe. Nchi ina uhaba wa ajira, lakini mbunge mmoja anakuwa na ajira mbili ya uwaziri na ubunge. Hii si sawa. Waziri aajiriwe kwa taaluma, ila mbunge anajulikana ni kujua kusoma na kuandika tu.
- Ulinzi na usalama
- Madaktari bingwa
- Elimu