rubii
JF-Expert Member
- Feb 22, 2015
- 14,113
- 18,744
Acha upotoshaji.Kuwa mkweli.Hivi unaelewa maana ya bure?
Acha udandiaji ovyoo post za watu kama huelewi zilipotokea mpaka kufika zilipo!!
Bure ijue wewe inatosha!
Acha upotoshaji.Kuwa mkweli.Hivi unaelewa maana ya bure?
Acha kutopoka anaye lalamika hajui anaulizwa aeleweshweAcha udandiaji ovyoo post za watu kama huelewi zilipotokea mpaka kufika zilipo!!
Bure ijue wewe inatosha!
Acha kutopoka anaye lalamika hajui anaulizwa aeleweshwe
View attachment 314952
Soma vizuri waraka namba 5 wa Mwaka 2015hapo juu kisha soma vizuri maelezo haya ya Serikali hapa chini.
=============
Serikali imepanga kupeleka Sh. 18.77 bilioni kila mwezi katika shule za sekondari na msingi kwa ajili ya kugharamia elimu ili kutekeleza dhana ya elimu bure kuanzia Januari, 2016.
Taarifa hiyo ilitolewa Mjini Dodoma jana na Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa elimu bure.
Alianisha fedha zitakazotolewa na Serikali kwa ajili ya kugharamia elimu ni pamoja na gharama za mitihani ya kidato cha nne ambazo zitatolewa moja kwa moja na Serikali katika Baraza la Mitihani (Necta).
“Serikali itatoa pia ruzuku ya uendeshaji wa shule Sh. 10,000 kwa shule za msingi na Sh. 25,000 kwa shule za sekondari kwa kila mwanafunzi kwa mwaka.
“Vilevile itatoa Sh. 1,500 kwa siku kwa mwanafunzi kwa shule za msingi na sekondari kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi wanaokaa bweni,” amesema.
Simbachawene amesema pia Serikali itatoa fedha kwa ajili ya fidia ya ada Sh. 20,000 kwa kila mwanafunzi wa shule ya kutwa na Sh. 70,000 kwa mwanafunzi wa sekondari kwa mwaka.
Amesema fedha za ruzuku ya uendeshaji wa shule zitasaidia pia uendeshaji wa shule za hosteli ikiwemo gharama za chakula, mlinzi, mpishi, umeme na maji.
Aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri husika kuhakikisha fedha hizo zinafika kwa wakati na zinatumika kwa kazi iliyokusudiwa.
Simbachawene amesema majukumu ya wazazi pamoja na mambo mengine yatakuwa ni kununua sare za shule, vifaa vya kujifunzia, gharama za matibabu, nauli, gharama za chakula kwa wanafunzi wa shule za kutwa na kununua magodoro, shuka, vifaa vya usafi binafsi kwa wanafunzi wa bweni.
“Natoa wito kwa viongozi wote wakiwemo wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa kusimamia utekelezaji wa elimu bila malipo,” amesema.
Aidha, Simbachawene aliziagiza halmashauri na mikoa ambayo haikufanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba kujieleza sababu za kutofanya vizuri.
“Iwapo itathibitika kwamba kuna wahusika walizembea kutimiza majukumu yao wachukuliwe hatua zinazostahili.
“Nawaagiza pia wakurugezi mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma kwamba ifikapo Februari 15 mwakani wawe wamekamilisha miundombinu ya shule ili wawewezeshe wanafunzi 12,647 waliosalia kujiunga na elimu ya sekondari wanaenda shule,” amesema.
Simbachawene pia alizitaka kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya kuwachukulia hatua za kisheria watu watakaosababisha wanafunzi kukatisha masomo kwa utoro na mimba pamoja na wale waliooa watoto wa kike.
‘’Tusifanye kazi kwa mazoea, tunatakiwa tuendane na kasi ya Rais John Magufuli ya kufanya kazi kuwasaidia wananchi hasa katika sekta ya elimu,’’ amesema.
MY TAKE: Hii ni Serikali ambayo imetoa Waraka, Wakati huo huo imegeuka Waraka wake na kutoa maelekezo mengine.
Huhitaji kuwaza sana kujua kuwa hawa jamaa wanahadaa UMMA tu na Hawana jipya zaidi ya kujitafutia uhalali wa kisiasa.
Sinto chambua kwa kuwa IPO wazi yakuwa sh 20000 ama 70000 mzazi asingeshindwa kulipa ila tatizo ni hizo gharama zingine ambazo ni kubwa sana kuliko Ada.... Tusiwahadae Wananchi kwa janja janja ya siasa.
Subir ukizaa ndiyo ulalamikeAcha ujuaji! Anayehitaji kueleweshwa hana shari!
Juzi nimempeleka mwanangu kimbwe shule kuchukua fomu ya kujiunga na shule ya kata.....mkuu wa shule kaniambia kuwa waraka walio letewa hauonyeshi fedha za chakula kwa wanafunzi wa shule za kata( day schools) hapa sijailewa wizara nasubiri mwanangu kimbwe anze shule tarehe 13 nitakuja kuwaeleza hapa kama kuna elimu ya bure au la!
Wewe umeskiliza Mimi walaka ninao.
Gharama unazodai ni kubwa ni zipi? Wewe kununua kiatu,sare na daftar kwako yamekuwa nongwa?
Kweli msemaovyo ni chombo cha gulioni. Sijui hata unaandika nini
Huyo yeye binafsi analelewa na kiria itakua kununua kiatu cha mwanae?
Subir ukizaa ndiyo ulalamike
Post za watu zilizo wazi humu?Acha uwakili wa hovyo.Acha udandiaji ovyoo post za watu kama huelewi zilipotokea mpaka kufika zilipo!!
Bure ijue wewe inatosha!
wewe mleta uzi ni bure kabisa kwani nani hajasoma katika hizo shule ,,,,ni mwanafunzi wangapi walikuwa wakirudishwa shule kwa kukosa hiyo elf 20,,,sasa wazazi wanapewa relief wewe unakuja hapa na hoja zako zisizo na kichwa wala miguu. Au wewe ulivyosikia elimu bure ulifikir serikali itagharamia kila kitu hadi majukumu yako wewe mzazi kama ni hivyo sasa wewe mzazi ungekuwa na jukumu gani kwa mwanao!!!!?????
sidhani kama una mtu unaemsomesha kwa kuwa Jana nilimpigia simu Mwalimu mkuu wa shule moja ambae kuna mtoto nilijitolea kumsomesha kwa kuwa wazazi wake hawana uwezo kudai ufafanuzi wa michango akaniambia nisome waraka ili nijue majukumu ya mzazi/mlezi , nikamwambia nimeusoma akanijibu sasa unatakiwa ulipe 160000 lasivyo mtoto hatapokelewa.
Post za watu zilizo wazi humu?Acha uwakili wa hovyo.
Kaoshe chombo.Yaani nimuulize mtu anaishi wapi unijibu wewe unapoishi kisa nimeuliza wazi??? ha ha haa maajabu tena
HUU NI UVIVU WA KUFIKIRI ....SHULE NI BURE HADI FORM FOUR. ! GHARAMA ZA SHULEVZIMEBEBWA NA SERKALI. ILA SIYO ZW KUVAA . KULA MADAFTARI NA KUSAFIRI.. MTOTO NI WAKO ULIYEMZAA. NSNI AKUBEBEE ZOTE WAKATI ANABEBA JINA LAKO ?
Pongezi sawa, lakini bado eneo la vyuo vilivyo chini ya nacte,,hakuna mikopo na watoto hawapewi chakula.Tupongeze basi hata hizi juhudi zinazofanyika...
Poleni sana. Mirija yenu ya kifisadi imekatwa. Mlizoea kutuibia sisi wazazi