Serikali iache kudanganya Wananchi, hakuna Elimu Bure

Henry Kilewo

JF-Expert Member
Feb 9, 2010
899
1,103
1451975491063.jpg

Soma vizuri waraka namba 5 wa Mwaka 2015hapo juu kisha soma vizuri maelezo haya ya Serikali hapa chini.
=============

Serikali imepanga kupeleka Sh. 18.77 bilioni kila mwezi katika shule za sekondari na msingi kwa ajili ya kugharamia elimu ili kutekeleza dhana ya elimu bure kuanzia Januari, 2016.

Taarifa hiyo ilitolewa Mjini Dodoma jana na Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa elimu bure.

Alianisha fedha zitakazotolewa na Serikali kwa ajili ya kugharamia elimu ni pamoja na gharama za mitihani ya kidato cha nne ambazo zitatolewa moja kwa moja na Serikali katika Baraza la Mitihani (Necta).

“Serikali itatoa pia ruzuku ya uendeshaji wa shule Sh. 10,000 kwa shule za msingi na Sh. 25,000 kwa shule za sekondari kwa kila mwanafunzi kwa mwaka.

“Vilevile itatoa Sh. 1,500 kwa siku kwa mwanafunzi kwa shule za msingi na sekondari kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi wanaokaa bweni,” amesema.

Simbachawene amesema pia Serikali itatoa fedha kwa ajili ya fidia ya ada Sh. 20,000 kwa kila mwanafunzi wa shule ya kutwa na Sh. 70,000 kwa mwanafunzi wa sekondari kwa mwaka.

Amesema fedha za ruzuku ya uendeshaji wa shule zitasaidia pia uendeshaji wa shule za hosteli ikiwemo gharama za chakula, mlinzi, mpishi, umeme na maji.

Aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri husika kuhakikisha fedha hizo zinafika kwa wakati na zinatumika kwa kazi iliyokusudiwa.

Simbachawene amesema majukumu ya wazazi pamoja na mambo mengine yatakuwa ni kununua sare za shule, vifaa vya kujifunzia, gharama za matibabu, nauli, gharama za chakula kwa wanafunzi wa shule za kutwa na kununua magodoro, shuka, vifaa vya usafi binafsi kwa wanafunzi wa bweni.

“Natoa wito kwa viongozi wote wakiwemo wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa kusimamia utekelezaji wa elimu bila malipo,” amesema.

Aidha, Simbachawene aliziagiza halmashauri na mikoa ambayo haikufanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba kujieleza sababu za kutofanya vizuri.

“Iwapo itathibitika kwamba kuna wahusika walizembea kutimiza majukumu yao wachukuliwe hatua zinazostahili.

“Nawaagiza pia wakurugezi mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma kwamba ifikapo Februari 15 mwakani wawe wamekamilisha miundombinu ya shule ili wawewezeshe wanafunzi 12,647 waliosalia kujiunga na elimu ya sekondari wanaenda shule,” amesema.

Simbachawene pia alizitaka kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya kuwachukulia hatua za kisheria watu watakaosababisha wanafunzi kukatisha masomo kwa utoro na mimba pamoja na wale waliooa watoto wa kike.

‘’Tusifanye kazi kwa mazoea, tunatakiwa tuendane na kasi ya Rais John Magufuli ya kufanya kazi kuwasaidia wananchi hasa katika sekta ya elimu,’’ amesema.

MY TAKE: Hii ni Serikali ambayo imetoa Waraka, Wakati huo huo imegeuka Waraka wake na kutoa maelekezo mengine.

Huhitaji kuwaza sana kujua kuwa hawa jamaa wanahadaa UMMA tu na Hawana jipya zaidi ya kujitafutia uhalali wa kisiasa.

Sinto chambua kwa kuwa IPO wazi yakuwa sh 20000 ama 70000 mzazi asingeshindwa kulipa ila tatizo ni hizo gharama zingine ambazo ni kubwa sana kuliko Ada.... Tusiwahadae Wananchi kwa janja janja ya siasa.
 
Last edited by a moderator:
mndorwe
Rais ametuhakikishia kuwa anaposema Elimu Bure ni Bure kweli. Yeye analeta mipasho ya Joyce Kiria kwenye Wanawake Live. Asubiri shule zifunguliwe aone kama kuna mzazi atachangishwa fedha. Hapo ndo ajikakamue kuja hapa kuandika anachoona kinafaa. Kwa sasa bandiko lake haina thamani na ndo maana limekosa wachangiaji
 
Last edited by a moderator:
Lizaboni
Labda nikulize wazazi hawatachangshwa fedha ta chakula ,hasa kwa shule za kutwa ambapo wanakula shulen mchana? Naona hapo kwenye maelezo ya wizara hakuna mahali ameandika kuhusu chakula cha mchana kwa shule za kutwa
 
Last edited by a moderator:
Simbachawene amesema majukumu ya wazazi pamoja na mambo mengine yatakuwa ni kununua sare za shule, vifaa vya kujifunzia, gharama za matibabu, nauli, gharama za chakula kwa wanafunzi wa shule za kutwa na kununua magodoro, shuka, vifaa vya usafi binafsi kwa wanafunzi wa bweni.

Sinto chambua kwakuwa IPO wazi yakuwa sh 20000 ama 70000 mzazi asingeshindwa kulipa ila tatizo ni hizo gharama zingine ambazo ni kubwa sana kuliko Ada.... Tusiwahadae Wananchi kwa janja janja ya siasa.

Kwahiyo wazazi walipe wenyewe ada lakini uniform na magodoro, sabuni, shuka, nauli ya kwenda shule walipiwe na serikali kwakuwa ni kubwa kuliko ada?????
 
Juzi nimempeleka mwanangu kimbwe shule kuchukua fomu ya kujiunga na shule ya kata.....mkuu wa shule kaniambia kuwa waraka walio letewa hauonyeshi fedha za chakula kwa wanafunzi wa shule za kata( day schools) hapa sijailewa wizara nasubiri mwanangu kimbwe anze shule tarehe 13 nitakuja kuwaeleza hapa kama kuna elimu ya bure au la!
 
SHULE NI BURE HADI FORM FOUR. ! GHARAMA ZA SHULEVZIMEBEBWA NA SERKALI. ILA SIYO ZW KUVAA . KULA MADAFTARI NA KUSAFIRI.. MTOTO NI WAKO ULIYEMZAA. NSNI AKUBEBEE ZOTE WAKATI ANABEBA JINA LAKO ?

Huyu akili zake zimepata mvurugo leoo! yaani anataka elimu bure basi mpaka vyupi wanavyovaa shule watoto wao serikali inunue ha ha haaa!
 
HAKUNA JIPYA MBWEMBWE ZA KISIASA TU.TOFAUTI NI HIYO 20000KWA KUTWA NA 70000 KWA BWENI.MICHANGO KAMA KAWAIDA.SERIKALI IMETAMKA HAKUNA MCHANGO JE WANAFUNZI WA KUTWA WATAPELEKA NINI KWA AJILI YA CHAKULA?
 
SHULE NI BURE HADI FORM FOUR. ! GHARAMA ZA SHULEVZIMEBEBWA NA SERKALI. ILA SIYO ZW KUVAA . KULA MADAFTARI NA KUSAFIRI.. MTOTO NI WAKO ULIYEMZAA. NSNI AKUBEBEE ZOTE WAKATI ANABEBA JINA LAKO ?
Umeandika kwa herufi kubwa (msisitizo), kumbe ni matope tu!
Bora ungeandika ki-lugha cha kwenu huenda ungeeleweka.
 
Labda nikulize wazazi hawatachangshwa fedha ta chakula ,hasa kwa shule za kutwa ambapo wanakula shulen mchana?? Naona hapo kwenye maelezo ya wizara hakuna mahali ameandika kuhusu chakula cha mchana kwa shule za kutwa
Kwani kwenye shule za kutwa wanapika chakula cha mchana? Kama kinapikwa, si mkakati wa serikali bali ni makubaliano baina ya shule na wazazi. Nalo linakubalika. Ila kwa wale wanafunzi wa bweni, bajeti ya chakula ipo
 
Juzi nimempeleka mwanangu kimbwe shule kuchukua fomu ya kujiunga na shule ya kata.....mkuu wa shule kaniambia kuwa waraka walio letewa hauonyeshi fedha za chakula kwa wanafunzi wa shule za kata( day schools) hapa sijailewa wizara nasubiri mwanangu kimbwe anze shule tarehe 13 nitakuja kuwaeleza hapa kama kuna elimu ya bure au la!

Kwako wewe elimu kuwa bure ulitegemeaje?
Gharama na michango ya shule yote imebebwa na serikali, au wataka mpaka gharama binafsi za mwanao?
 
Huyu jamaa kafanya upembuzi yakinifu unless you are mad you can't ignore the fact. Shuleni wametakiwa kuandaa budget za shule kwa mwaka kiukwel serikali inapaswa ichukue muda kwenye kuandaa mipango Kazi yake itakayorandana na recently research finding. Hzo ada za elfu 20 na sabini hats form ya kujiunga na chuo hununui. Work as usual!!
 
Huyu akili zake zimepata mvurugo leoo! yaani anataka elimu bure basi mpaka vyupi wanavyovaa shule watoto wao serikali inunue ha ha haaa!
Kavurugwa huyo. Kwa vile yeye ni gumegume ndo maana anategemea kila kitu wafanye serikali.
 
Juzi nimempeleka mwanangu kimbwe shule kuchukua fomu ya kujiunga na shule ya kata.....mkuu wa shule kaniambia kuwa waraka walio letewa hauonyeshi fedha za chakula kwa wanafunzi wa shule za kata( day schools) hapa sijailewa wizara nasubiri mwanangu kimbwe anze shule tarehe 13 nitakuja kuwaeleza hapa kama kuna elimu ya bure au la!
We tafuta mtu akusaidie kulea huyo mtt wako..Naona anakushinda...
 
Huyu jamaa kafanya upembuzi yakinifu unless you are mad you can't ignore the fact. Shuleni wametakiwa kuandaa badger za shule kwa mwaka kiukwel serikali inapaswa ichukue muda kwenye kuandaa mipango Kazi yake itakayorandana na recently research finding. Hzo ada za elfu 20 na sabini hats form ya kujiunga na chuo hununui. Work as usual!!
Poleni sana. Mirija yenu ya kifisadi imekatwa. Mlizoea kutuibia sisi wazazi
 
Back
Top Bottom