Serikali iache kudanganya Wananchi, hakuna Elimu Bure

Serikali iache kudanganya Wananchi, hakuna Elimu Bure

Mimi sioni tatizo la walimu liko wapi vyovyote vile mambo yatakavyokuwa.

Binafsi sioni shida yoyote hata kama waseme wanafunzi wote waende shule pekupeku au vifua wazi achilia mbali kulipa fedha yoyote!!

Tatizo liko wapi iwapo wewe mwalimu unapata haki zako zote kwa wakati kama vile mshahara na pia unakuta vitendea kazi vyako kama kalamu, daftari, chaki nk??

Defenetely kuna tatizo katika hili especially kwa walimu wakuu wa shule ktk usimamizi na uendesheshaji wa shule walizokabidhiwa.

Mfano kuna shule moja imepokea Tshs. 400,000/= (hii ni shule ya sekondari ya kata ktk mkoa wa Shinyanga) ktk mgawo wa elimu bure nadhani kwa mwezi januari, 2016.

Sasa hebu fikiria utazitumia kufanyia nini hizo pesa wakati katoni ya chaki tu ni karibu Tshs. 200,000??

Tukumbuke kuwa shule hizi zina watumishi kama walinzi na wengine wanaolipwa na shule posho (sio mshahara) ya kati ya Tshs. 100,000 - 200,000 kwa mwezi. Sasa sijui shule ziwafute kazi walinzi hawa? Je, si kweli kuwa itafika wakati wazazi wachangie tu ili huduma hizi ziendelee kutolewa shuleni kwa sbb kwa vyovyote walinzi ni muhimu mashuleni??
Kasome tena waraka waelimu
 
Kasome tena waraka waelimu
Nimeusoma na wewe nisome mimi vizuri unielewe.

Nimesema kuchangia hukuepukiki kwa mzazi/mlezi achilia kwa yeye
kutekeleza wajibu wake kwa mtoto
wake kama mzazi i.e kumpatia
mahitaji ya kibinadamu kama mavazi,
daftari, kalamu, chakula nk

Uchangiaji huu ni lazima wazazi wenyewe wakutane na wakubaliane wachangie ktk nini na kiwango na utaratibu wa kuchangia jambo hata hapo kabla lilikuwa linafanyika!!
 
Bado Elimu bure ipo? Maigizo... Unapotaka kupoka sera ambayo hujui misingi yake matokeo yake kwenye utekelezaji lazima utayumba kwakuwa hujui ni misingi ipi ingetumika kuitekeleza.. Serikali ya CCM imeanza kuyumba na Sera ya elimu bure kwakuwa hawajui Misingi ya sera hii....
 
Back
Top Bottom