Serikali iache kudanganya Wananchi, hakuna Elimu Bure

Serikali iache kudanganya Wananchi, hakuna Elimu Bure

Juzi nimempeleka mwanangu kimbwe shule kuchukua fomu ya kujiunga na shule ya kata.....mkuu wa shule kaniambia kuwa waraka walio letewa hauonyeshi fedha za chakula kwa wanafunzi wa shule za kata( day schools) hapa sijailewa wizara nasubiri mwanangu kimbwe anze shule tarehe 13 nitakuja kuwaeleza hapa kama kuna elimu ya bure au la!
Kani wakati anasoma ahule ya msingi mtoto wako alikuwa anapata chakula cha mchana shuleni?
 
Sasa ndo umeandika nini? Au Joyce Kiria kakukera leo? Maana sijui kama umeelewa nini umeandika na nini kinaendelea. Hasira zako na mkeo usizihamishie kwenye jukwaa. Unavuruga
Hawa wafuasi wa Lowassa tangu watelekezwe AKILI Zimewaruka kabisa.Hakuna cha maana utakachopata zaid ya matusi tu...........
 
We kwel uelewa wako ni mdogo sana,ladba watumie michoro na catoon ndo utaelewa,kuna baadh ya shule zimefunguliwa jana tar 4/01/2016 na wazaz wanatakiwa kulipa 50000 za ujenz,15000 za viti na meza, magodoro,madaftar tena ya sh 3000 kila moja,pesa ya uji na chakula sh 120000 kwa mwaka,na mengne mengi 2,sasa unacho ongerea wew kuwa shule zifunguliwe ni kuhsu shule gan?kimsing elimu bure kwa serikal ya ccm haiwezekan.
 
Hahahahahaaaaa! Usieleze kwa ujumla. Taja jina la shule, mahali ilipo na aina ya michango wanayotoza. Usiandike mambo ambayo umeambiwa wakati umepakatwa then unakuja kuyaweka humu
 
Mimi nimempeleka Mwanangu Mtakuja Primary schoo, kumuandikisha darasa la kwanza, wamempokea, nikawauliza, Je kuna mchango wowote? wakanijibu hakuna, Mwl mkuu akanifafanulia kuwa, Tshirt za kuvaa Ijumaa na Nembo, zikiwa tayari, wazazi tutafahamishwa, tulipie elfu 10 tu, kwa zote!
 
View attachment 314952

Soma vizuri waraka namba 5 wa Mwaka 2015hapo juu kisha soma vizuri maelezo haya ya Serikali hapa chini

SERIKALI imepanga kupeleka Sh. 18.77 bilioni kila mwezi katika shule za sekondari na msingi kwa ajili ya kugharamia elimu ili kutekeleza dhana ya elimu bure kuanzia Januari, 2016.

Taarifa hiyo ilitolewa Mjini Dodoma jana na Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa elimu bure.

Alianisha fedha zitakazotolewa na Serikali kwa ajili ya kugharamia elimu ni pamoja na gharama za mitihani ya kidato cha nne ambazo zitatolewa moja kwa moja na Serikali katika Baraza la Mitihani (Necta).

“Serikali itatoa pia ruzuku ya uendeshaji wa shule Sh. 10,000 kwa shule za msingi na Sh. 25,000 kwa shule za sekondari kwa kila mwanafunzi kwa mwaka.

“Vilevile itatoa Sh. 1,500 kwa siku kwa mwanafunzi kwa shule za msingi na sekondari kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi wanaokaa bweni,” amesema.

Simbachawene amesema pia Serikali itatoa fedha kwa ajili ya fidia ya ada Sh. 20,000 kwa kila mwanafunzi wa shule ya kutwa na Sh. 70,000 kwa mwanafunzi wa sekondari kwa mwaka.

Amesema fedha za ruzuku ya uendeshaji wa shule zitasaidia pia uendeshaji wa shule za hosteli ikiwemo gharama za chakula, mlinzi, mpishi, umeme na maji.

Aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri husika kuhakikisha fedha hizo zinafika kwa wakati na zinatumika kwa kazi iliyokusudiwa.

Simbachawene amesema majukumu ya wazazi pamoja na mambo mengine yatakuwa ni kununua sare za shule, vifaa vya kujifunzia, gharama za matibabu, nauli, gharama za chakula kwa wanafunzi wa shule za kutwa na kununua magodoro, shuka, vifaa vya usafi binafsi kwa wanafunzi wa bweni.

“Natoa wito kwa viongozi wote wakiwemo wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa kusimamia utekelezaji wa elimu bila malipo,” amesema.

Aidha, Simbachawene aliziagiza halmashauri na mikoa ambayo haikufanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba kujieleza sababu za kutofanya vizuri.

“Iwapo itathibitika kwamba kuna wahusika walizembea kutimiza majukumu yao wachukuliwe hatua zinazostahili.

“Nawaagiza pia wakurugezi mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma kwamba ifikapo Februari 15 mwakani wawe wamekamilisha miundombinu ya shule ili wawewezeshe wanafunzi 12,647 waliosalia kujiunga na elimu ya sekondari wanaenda shule,” amesema.

Simbachawene pia alizitaka kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya kuwachukulia hatua za kisheria watu watakaosababisha wanafunzi kukatisha masomo kwa utoro na mimba pamoja na wale waliooa watoto wa kike.

‘’Tusifanye kazi kwa mazoea, tunatakiwa tuendane na kasi ya Rais John Magufuli ya kufanya kazi kuwasaidia wananchi hasa katika sekta ya elimu,’’ amesema.

Hii ni serikali ambayo imetoa Waraka, Wakati huwo huwo imegeuka Waraka wake na kutoa maelekezo mengine.

Huhitaji kuwaza sana kujua kuwa hawajamaa wanahadaa UMMA tu na Hawana jipya zaidi ya kujitafutia uhalali wa kisiasa.

Sinto chambua kwakuwa IPO wazi yakuwa sh 20000 ama 70000 mzazi asingeshindwa kulipa ila tatizo ni hizo gharama zingine ambazo ni kubwa sana kuliko Ada.... Tusiwahadae Wananchi kwa janja janja ya siasa.
wewe mleta uzi ni bure kabisa kwani nani hajasoma katika hizo shule ,,,,ni mwanafunzi wangapi walikuwa wakirudishwa shule kwa kukosa hiyo elf 20,,,sasa wazazi wanapewa relief wewe unakuja hapa na hoja zako zisizo na kichwa wala miguu. Au wewe ulivyosikia elimu bure ulifikir serikali itagharamia kila kitu hadi majukumu yako wewe mzazi kama ni hivyo sasa wewe mzazi ungekuwa na jukumu gani kwa mwanao!!!!?????
 
Katika mchanganuo huo,sijaona pesa zitazolipa madeni ya nyuma.Kuna shule zina madeni ya nyuma,sasa hapo hata maafisa elimu hawajasema ukwel kwa tamisemi,utakuta kuna shule ina deni la sh.mil.10-25 au chini ya hapo.
 
wewe mleta uzi ni bure kabisa kwani nani hajasoma katika hizo shule ,,,,ni mwanafunzi wangapi walikuwa wakirudishwa shule kwa kukosa hiyo elf 20,,,sasa wazazi wanapewa relief wewe unakuja hapa na hoja zako zisizo na kichwa wala miguu. Au wewe ulivyosikia elimu bure ulifikir serikali itagharamia kila kitu hadi majukumu yako wewe mzazi kama ni hivyo sasa wewe mzazi ungekuwa na jukumu gani kwa mwanao!!!!?????

Anataka kugeuza shule kituo cha kulelea watoto wao
 
We kwel uelewa wako ni mdogo sana,ladba watumie michoro na catoon ndo utaelewa,kuna baadh ya shule zimefunguliwa jana tar 4/01/2016 na wazaz wanatakiwa kulipa 50000 za ujenz,15000 za viti na meza, magodoro,madaftar tena ya sh 3000 kila moja,pesa ya uji na chakula sh 120000 kwa mwaka,na mengne mengi 2,sasa unacho ongerea wew kuwa shule zifunguliwe ni kuhsu shule gan?kimsing elimu bure kwa serikal ya ccm haiwezekan.
Hakuna shule au mwalimu anaweza kufanya upuuzi huo kwa sasa hata wao wanaogopa
 
Labda nikulize wazazi hawatachangshwa fedha ta chakula ,hasa kwa shule za kutwa ambapo wanakula shulen mchana?? Naona hapo kwenye maelezo ya wizara hakuna mahali ameandika kuhusu chakula cha mchana kwa shule za kutwa
Kwani shule zote za kutwa wanakula shuleni mchana???????????????Wabongo mna vichwa vizitoooooooooooooo
 
Hakuna mwanafunzi aliyekuwa anarudishwa kwa kushindwa kulipa sh 20000 za ada bali pesa za michango,mfano ambao upo hali,mdogo wangu alitoa pesa kiasi cha sh 70000 ktk shule ya sekondar CHAKARURU iliyoko wilaya ya KARAGWE mkoa KAGERA,alitaka alipie mtihan lakin mkuu wa shule akaipeleka ktk upande wa michango kama umeme,ukarabat,taaluma n.k,akikenga kumfanya mzaza,aumie kutafuta pesa nyingne ili mtoto aweze kulipia mtihan,bahat mbaya zikakosa,mpaka sasa mdogo wangu hana matokeo ya mtihan tangu 2013 alipomaliza 4m4
 
Last edited by a moderator:
Kwani shule zote za kutwa wanakula shuleni mchana???????????????Wabongo mna vichwa vizitoooooooooooooo
Wewe ndo kichwa kizito huku kilimanjaro watoto wanakula shulen , na hii ni lazimab,huwez kumkalishabshulen mwanafunzi kuanzia saa moja asubuh had saa kumibasile ni kumnyanyasa
 
Ha ha haaaa.... kuzaa wazae wenyewe mizigo ya kulea waitishe serikali
Yani katika vyote mtu anakuja kulalamika kuhusu chakula kwa wanafunzi wa kutwa...Mzazi kama Huyu nahisi kama chakula kingekuwa kinatolewa basi angekuwa yuko ladhi mtt asihudhurie vipindi ila ikifika muda wa lunch anamwambia nenda shule kapige msosi
 
Wewe ndo kichwa kizito huku kilimanjaro watoto wanakula shulen , na hii ni lazimab,huwez kumkalishabshulen mwanafunzi kuanzia saa moja asubuh had saa kumibasile ni kumnyanyasa

Ni kweli mkoa wa kilimanjaro wanakula shuleni mchana na ni lazima. Hii inasaidia sana wanafunzi wa huo mkoa kufaulu vizuri.
 
Hii itakuwa imetulia kama itafatiliwa kwa umakn, maana wabongo nae kwa uchakachuz hawajambo
 
Back
Top Bottom