Serikali hoi kifedha, Sasa kukopa...

Serikali hoi kifedha, Sasa kukopa...

Dont go away

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2014
Posts
501
Reaction score
208
Kuna taarifa kutoka serkalini kuwa serikali ipo hoi kifedha na imewasimamisha wakandarasi wote waliokuwa wanangojea fedha ili waendelee na kazi na wale wote waliokuwa site wakiendelea na kazi ili kukwepa riba, hivyo serikali ipo kwenye mazungumzo na bank ya CRDB ili kukopa Bilioni 900 Tshs. Vile vile mishahara kwa watumishi wake imekuwa tabu sana hivyo serikali kulazimika kukopa pesa toka mabank mbali mbali nchini ikiwemo NMB ili kulipa mishahara.

Athari za Acc. ya Escrow ya TEGETA ni kubwa sana kuliko RAIS alivyolidanganya TAIFA kuwa athari zake si kubwa.
 
Ni kweli, haya Wabunge hawajalipwa mishahara yao na posho za Bunge lililopo ya nadhani. Kuna rafiki yangu kachukua tenda ya kuweka kifusi kwenye barabara maeneo Mbagala mpaka leo anapigwa Kiswahili tu.
Benno Ndulu alionya kuwa hutolewaji wa pesa zilizokuwa kwenye akaunti ya Escrow kunaweza kuyumbisha uchumi wetu, lakini majizi hayakutaka kumsikiliza yakalazimisha pesa zitoke na kugawana haraka haraka.
Hali mbaya kweli, kama hakutakuwa na chochote kuna hatari mishahara ya walimu na Polisi ikaanza kupigwa kalenda.
Ova
 
Huyu Jakaya hajui kuwa Historia itamkumbuka kama Rais Bogus kuwahi kutokea Tanzania.
Anachojua ni kutetea mafisadi na kututangazia kuwa anaumwa Busha ili tumuonee Huruma.
Hataki kuwajibika wala kusimamia uwajibikaji wa walio chini yake, siku ziku zote hakosi visingizio.

8888Kabisa...!
 
Mie natamani hali ya serikali, na wananchi izidi kuwa ngumu na mbaya [kwa nia njema] ili ifike mahali tujue umuhimu wa kutowachekea viongozi na watendaji wapuuzi. Kwa upuuzi unaofanywa sasa hivi ni nguvu ya wananchi pekee ndo inayoweza kutoa ujumbe kwa viongozi kuwa tukiamua wao na familia zao hawabaki salama. Kitu kibaya, mijitu mingine hawajatambua hilo hivyo wacha tule shida wote mpaka akili itukae vizuri.
 
hawawezi kopa crdb wao hiyo bank wapo heka heka ya kurudisha hela walizokopesha wenye shea kubwa wametoa notes kutoa shea zao hiyo bank
 
Kuna taarifa kutoka serkalini kuwa serikali ipo hoi kifedha na imewasimamisha wakandarasi wote waliokuwa wanangojea fedha ili waendelee na kazi na wale wote waliokuwa site wakiendelea na kazi ili kukwepa riba, hivyo serikali ipo kwenye mazungumzo na bank ya CRDB ili kukopa Bilioni 900 Tshs. Vile vile mishahara kwa watumishi wake imekuwa tabu sana hivyo serikali kulazimika kukopa pesa toka mabank mbali mbali nchini ikiwemo NMB ili kulipa mishahara.

Athari za Acc. ya Escrow ya TEGETA ni kubwa sana kuliko RAIS alivyolidanganya TAIFA kuwa athari zake si kubwa.
Labda kama tuna matatizo mengine, fedha zilizozuiliwa na wafadhili, sio ile General Budget Support kupitia Busket Funding, ni development budget, hivyo zile sio fedha za kulipia mishahara!. Hata fedha za MCC pia sio fedha za kulipia mishahara!.
Kama ni kweli Watumishi wa umma wamekosa mishahara, then tuna tatizo kubwa kuliko tunavyo jidhania!.

Pasco.
 
Uozo wa Serikali ya Kikwete lazima uanikwe hadharani kwa nguvu zote maana unaingamiza nchi. Sasa hata Wafadhili wamegoma kutoa pesa zao za msaada. Mishahara Serikalini inachelewa sana kulipwa miradi kama ya ujenzi wa barabara imeanza kusimama, mahospitali hayana madawa. Usisahau pia jinsi alivyoingilia zoezi la kuandika katiba mpya na kulivuruga. Hakuna sababu ya kuunyamazia uozo uliopo ndani ya hii Serikali ambao unasababishwa na fisadi Kikwete.

we jamaa inaonesha uko kwenye kampeni maalum!
 
Kwa watu wangine, CCM kwao ni nyumba ya ibada na waliuona ujamaa na kujitegemea kama vile dini mbadala. Hivyo wako tayari kukipa kurahata kama kitawaletea shetani wakuwanyonya damu zao!
 
Naamini hata Mh Rais ameshajua kuwa Watz wamemchoka,na yeye Bila shaka hii Hali inamnyima raha Ila Ndio afanye nini kwani mashambulizi toka kwa raia na msingi mbovu wa utawala aliouweka unamfanya ashindwe kujua pa kuanzia,ninachoomba Watz wezangu hata kama tunataka hii chama iparanganyike lkn tumuombee Mh Rais amalize salama na asije kufanya maamuzI ya ajabu zaidi na kuligharimu Taifa kwani hasara itakuwa yetu sote.......
 
Kikwete hatumtaki tumemchoka aondoke zake na tumchukie...hafai hata kidogo..ametuharibia nchi.ni bora nchi iongozwe na jeshi kuliko kuwa rais fake kama kikwete.
 
Labda kama tuna matatizo mengine, fedha zilizozuiliwa na wafadhili, sio ile General Budget Support kupitia Busket Funding, ni development budget, hivyo zile sio fedha za kulipia mishahara!. Hata fedha za MCC pia sio fedha za kulipia mishahara!.
Kama ni kweli Watumishi wa umma wamekosa mishahara, then tuna tatizo kubwa kuliko tunavyo jidhania!.

Pasco.

Mkuu kuna utaratibu mpya wa matumizi ya pesa kwa sasa ambapo serikali inatoa fedha inayopatikana katika "Important sectors" kwa mfano Afya ili madawa yapatikane muda wote wananchi wasipate hasira dhidi ya serikali.

Kumbuka serikali haina reserve ya kutosha ya US Dollars hata ule ushauri wa Anna kilango bungeni kuwa Madini muhimu ya TANZANITE serikali iweke utaratibu mzuri ili yawe yanawekwa BOT (Kiwango fulani) ulitupiliwa mbali hii ingesadia kustabilize uchumi na kupambana na mfumuko wa bei na kupata pesa za kutosha kuagiza bidhaa nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom