Nimeona na mpimbafu mwenzako Yeriko Nyerere amesema Magufulification...
How magufulification katika utawala wa Mh Samia?
Mnataka kutwambia mh samia hana uwezo wa kutafakari na kuamua tofauti na kilichopendekezwa?
Mkuu samahani labda Mimi nina tongo tongo!
Ninachojua mimi kwenye mchakato wa kutunga Sheria bunge halitungi Sheria bali linajadili muswada wa sheria na kushauri kipi kiongezwe na kipi kipunguzwe!
Wizara husika hukaa na kuona mahitaji ya kisheria katima wizara au Idara husika!
Wataalamu wa sheria wa wizara wanadraft mapendekezo kwa kishirikina na mwanasheria mkuu wa serikali.
Draft husika huwasilishwa kwenye kikao cha Baraza la mawaziri ambapo Rais ndiye mwenyekiti, baada ya Baraza la mawaziri kuijadili na kukubalika juu ya Hiyo Draft inaandikwa Kama Billl of law au muswada wa sheria.
Wakati wa vikao vya Bunge waziri huwasilishwa muswada huo Bungeni ili wabunge waweze kuusikia na kuujadili kwa pamoja huku wakitoa mapendekezo na marekebisho mbalimbali.
Serikali hurudi na kukaa na kupitia mapendekezo yaliyotolewa na wabunge pamoja na wadau wa swala husika.
Baada ya hapo hurudihswa tena bungeni ili kupigiwa kura na kupitishwa ili kuwa Sheria.
Aidha baada ya kupitishwa muswada huo hurudishwa kwa rais ili atie saini kuwa Sheria hiyo imeanza kutumika.
Kwa mujibu wa katiba yetu na mtiririko huo ni dhahiri kwamba sheria au mapendekezo ya Sheria yanaanza na Rais na sio wabunge unless mbunge aje na hoja binafsi katika sheria husika.
Na inapotokea Bunge na serikali wakashindwa kuelewana katika Sheria husika Rais anaweza kulivunja Bunge na tukarejea kwenye uchaguzi!
Kwa Sheria hii iliyoletwa na Waziri Simba chawene Ni Sheria inayoenda kulinda Maslahi ya Viongozi wa CCM ikiwemo Rais wabunge mawaziri na viongozi waandamizi wa serikali ambao kwa nafasi zao wanaweza kuwatumia watu wa usalama wa taifa katika kutimiza majukumu yao au kutimiza matarajio yao kisiasa.
Kufungua kinacholalamikiwa Ni kuwaongezea kinga za kijinai maafisa wa usalama wa taifa au wafanyakazi wa idara ya usalama wa taifa wanapokua wanatimiza majukumu yao.
Swali je Nani anajua mstari wa majukumu ya afisa wa usalama wa taifa kiusalama au binafsi!? Kwamba anaweza kuutwaa uhai wa mtu lakini katika Mazingira ambayo hayana uhusiano na usalama wa taifa lakini sheria itamlinda! (Kinga ya kutishtakiwa) kwa makosa ya kijinai.
Sheria inaenda kubadilishwa kwamba Idara ya usalama wa taifa haitakua Tena chini ya waziri Bali Rais!
Lakini pia kuna kuongezewa kwa kiapo Cha kutunza siri hata baada ya kustaafu au kuacha kazi, kwamba kwakua watakua na Kinga ya kijinai I maana hata makosa ya hovyo watakayofanya kwa kutumiwa na watawala hakuna namna watatoa taarifa kwa vyombo vingine vya dola au serikali nyingine!
Kwahiyo Sheria hii inaonekana kujenga Mazingira ya kuminya wakisoaji wa serikali kwa namna ya tofauti kuliko wakati uliopita!