Serikali hii "force account" mnaua ajira za vijana wetu wahandisi, badilisheni huu mfumo

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
15,797
28,460
Ndugu zangu! Sote tunafahamu kazi kubwa ya wandisi wanaohitimu katika vyuo vyetu ajira zao nyingi zilikuwa zinapatikana kupitua kampuni za ujenzi.

Kumbukeni miradi mingi katika nchi ni ile ya serikali, kama zahanati, barabara za vijijini, majengo ya madarasa, mabweni, na shughuli nyingine nyingi za ujenzi.sasa unakupa vijana wanaajiriwa katika kampuni hizo. Hao vijana wakipata ajira hizo nao huanzisha miradi tofauti tofauti ambapo nao huajiri watu katika biashara zao na mwisho ni muendelezo wa uzalishaji wa ajira hivyo hivyo.

Kumbuka kutokana na uchumi duni Watanzania walio wengi hawatumii wahandisi katika ujenzi hata was nyumba zao,ndipo linapokuja swala la ajira zao kuwezeshwa na serikali pekee.

Sasa huko serikalini kitu kinaitwa force akount yani wanatumia mafundi wa kawaida-mwisho wake madhara ya kiufundi huwa ni makubwa lakini kubwa zaidi ni madhara ya kiuchumi.

Serikali inasema lengo kubwa ni kupunguza gharama, lakini mile naona hii sio haja maana kama ungwekwa utaratibu mzuri na usimamizi haya yote yanawezekana.
 
Hili suala, serikali iliangalia impacts zake upande mmoja tu wa shilingi.

Nimesoma uhandisi na ninawaona vijana wenzangu wengi tu kwa namna wanavyohaha mtaani.
 
Yule aliyekuwa anapiga hela kwenye miradi ya ujenzi akiwa nyapara anadhani kila mtu ni mpigaji kama yeye
 
Hili suala, serikali iliangalia impacts zake upande mmoja tu wa shilingi.

Nimesoma uhandisi na ninawaona vijana wenzangu wengi tu kwa namna wanavyohaha mtaani.
Nipo kwenye kamati ya ukarabati wa shule hapa kijijini kwetu, nusu ya waliopata kazi ni wahandisi.
Wao ndio wanaomba kazi wakipata wanatafuta local fundi
Hata wasio wahandisi na wao pia ni mafundi wamesomea ufundi
 
Dah maisha yanaenda kasi sana
Hakuna tofauti ya kusomea art na science moto ni ule ule. Tena bora na art ata wanapata Pa kujishikiza ata utendaji

Ngoja Tuendelee kuishi Kama mashetani tutaelewana kidogo kidogo
 
Serikali inasema lengo kubwa ni kupunguza gharama,lakini mile naona hii sio haja maana kama ungwekwa utaratibu mzuri na usimamizi haya yote yanawezekana.
Sijakuelewa,unaifundisha serikali jinsi ya kutumia pesa zake au unataka ajira?
 
Sio tu hilo siku hizi serikali inafyatulisha Hadi matofari ya kuuza unaweza waza watu wa kawaida watafanya kazi gani sasa.
Nilianzusha uzi humu kuzungumzia mambo haya ya kijaa Cha kushangaza watu hata hawajaona shida wanajibu eti tuwe wabunifu
 
Kikubwa hapa ni kuwafuata hukohuko tu kwenye force account tukapambane nao nasisi tuwe mafundi unajaza form halafu unaajiri fundi kupiga kazi Sema changamoto fundi wanajazaa being ndogo.​
 
Wahandisi wetu wanatu- let down sana. Wakipewa tu kikazi cha milioni mia tano, kwanza akanunue gari mpya na kuanza kujenga nyumba yake. Wakati mchina anakufanyia kazi kwanza faida anahesabu baadae. Matokeo ni kuanza kuzunguushana. Anafanya kazi kidogo anadai malipo makubwa.
Hiyo force account imeondoa kadhia hii na kuongeza ajira locally.
Local content baby.
 
Ndugu zangu! Sote tunafahamu kazi kubwa ya wandisi wanaohitimu katika vyuo vyetu ajira zao nyingi zilikuwa zinapatikana kupitua kampuni za ujenzi.

Kumbukeni miradi mingi katika nchi ni ile ya serikali, kama zahanati, barabara za vijijini, majengo ya madarasa, mabweni, na shughuli nyingine nyingi za ujenzi.sasa unakupa vijana wanaajiriwa katika kampuni hizo. Hao vijana wakipata ajira hizo nao huanzisha miradi tofauti tofauti ambapo nao huajiri watu katika biashara zao na mwisho ni muendelezo wa uzalishaji wa ajira hivyo hivyo.

Kumbuka kutokana na uchumi duni Watanzania walio wengi hawatumii wahandisi katika ujenzi hata was nyumba zao,ndipo linapokuja swala la ajira zao kuwezeshwa na serikali pekee.

Sasa huko serikalini kitu kinaitwa force akount yani wanatumia mafundi wa kawaida-mwisho wake madhara ya kiufundi huwa ni makubwa lakini kubwa zaidi ni madhara ya kiuchumi.

Serikali inasema lengo kubwa ni kupunguza gharama, lakini mile naona hii sio haja maana kama ungwekwa utaratibu mzuri na usimamizi haya yote yanawezekana.
Chief...mimi nadhani kwenye hoja yako wanaoathirika ni wakandarasi wala si vijana kukosa ajira kama unavyodai. Vijana wanapata ajira hata kupitia hao hao mafundi mchundo ambao unawajengea hoja hapa. Maana ili kazi ikamilike, hawezi kufanya fundi mmoja pekee.

Cha msingi wakandarasi mjitathimini. Hili kaburi mmejichimbia wenyewe kwa kujisahau kwenu katika utendaji. Gharama zenu ziko juu sana. A mlifocus kufanya kazi na serikali pekee na kuwatenga watu binafsi.

Nakumbuka nilipata quotation ya ujenzi wa nyumba ya kawaida tu kwa sh 600,000 kwa square meter toka kwa kampuni moja wapo ya ujenzi. Nyumba ya square meter 10 kwa milioni 60. Hali nyumba imekamilika kwa 27mil pekee hivi sasa.

Jitathiminini upya
 
Back
Top Bottom