Dr PL
JF-Expert Member
- Sep 13, 2024
- 588
- 889
Wanasema mwenge wa uhuru ni alama ya taifa yenye kuleta matumaini, mshikamano na kuhamasisha maendeleo.
Pia huhamasisha mapambano dhidi ya maradhi, ujinga, umasikini, rushwa, na kuimarisha amani, nk.
Sasa najiuliza:-
1. Kwa nini Tanzania bado tuna umasikini licha ya uwepo wa mwenge wa uhuru?
2. Mbona kuna nchi za jirani hawana mwenge wa uhuru lakini baadhi tuko nao sawa kimaendeleo au hata kutuzidi kwa kiasi fulani?
3. Kwa nini bado rushwa imeshamiri nchini licha ya kuwepo kwa mwenge wa uhuru unaohamasisha mapambano dhidi ya rushwa?
4. Kama mwenge wa uhuru huleta amani kwa nini huwa haipelekwi kwenye mataifa ya jirani yaliyo na vita ili kutuliza hali?
5. Kwa nini Tanzania tulipitia matukio yale ya October 2025 wakati tuna mwenge wa uhuru? Watu waliuwawa katika nchi ambayo ina mwenge wa uhuru, kwa nini?
6. Kwa nini sasa hivi hakuna uhuru wa watu kutoa maoni yao? Wanaotoa maoni huishia kutekwa na kupotezwa licha ya uwepo wa mwenge wa uhuru.
7. Au mwenge wa uhuru ni utapeli tu usiokuwa na uhalisia wowote kuhusu yanayonasibishwa nayo?
Nafikiri ni muhimu kufanya tathmini juu ya faida za kuendelea kutumia fedha nyingi kila mwaka kukimbiza mwenge.
Ni bora fedha zinazotengwa kukimbiza mwenge zilielekezwe kwenye miradi ya maendeleo kama tulivyoona fedha za sikukuu ya uhuru wa Tanganyika zikielekezwa kwingine.
Mwenge wa uhuru upigwe chini tu kwa sababu hata hali ya maisha (rushwa, utekaji wa watu, ufisadi nk) na siasa (ya chuki, upendeleo nk) hakuna msaada wowote unaoletwa na mwenge huo.
Kuna watu wengi wamekata tamaa, wengine wanasumbuliwa na maradhi mbalimbali na wakati mwingine hushindwa hata kulipia matibabu na mwenge wa uhuru wala haujawahi kuleta matumaini yoyote kwao.