Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,533
Katika vitu ambavyo bado naishangaa leo hii, ni Serikali yetu kuwa na Sheria ya Habari ambayo inalazimisha kuwepo kwa Waziri wa habari.
Nimejiuliza, kwa nini tunaendelea kuwa na Waziri Kamili ambaye anakuwa na Naibu Waziri, Katibu Mkuu na wataalamu kibao kwa shughuli ambayo si ya uzalishaji mali bali yahitaji mwongozo na uratibu wa cheo cha Kamisheni na kuongozwa na Kamishna au Mkurugenzi?
Nikiangalia jinsi Mamlaka ya Kodi livyo na kazi nyingi, ni heri basi kungekuwa na Waziri wa Kodi lakini si Waziri wa habari na Michezo!
Je tangu tupate uhuru wa pili baada ya kuzaliwa kwa Azimio la Zanzibar na Vyama vingi, kumekuwa na umuhimu gani wa kuwa na Waziri kamili na manaibu kwa ajili ya Habari, Michezo na utamaduni?
Hatuna miundombinu ya kuendeleza michezo na kufanya michezo iwe ni sehemu ya Uzalishaji mali, Utamaduni tunaupuuzia kuwa ni kujiliwaza na si kuweka kipaumbele kulinda Utamaduni wa asili na kutumia elimu kuboresha shughuli za Utamaduni, iwe ni maigizo, muziki, mila au desturi.
Jana Rais wetu Kikwete akifungua rasmi kuzaliwa kwa mara ya Tatu kwa TBC (Tanzania Broadcating Corportation) amesifia jinsi anavyoheshimu fani ya Uandishi wa habari. Nikajiuliza, kwa nini Serikali inaendelea kuwa na mashirika kama TBC na TVT? kwa madhumuni gani? Tayari tuna idara ya maelezo, Shihata ambayo ilikuwa ni sawa na Associated Press au Reuteurs imekufa, lakini Serikali inatumia kodi zetu kuwana na Magazeti, Tovuti na Redio?
Kwenye hii karne ya nano technology ambapo traditional media zinakufa kutokana na Internet, sisi bado tunakimbilia kutumia pesa za walipa kodi kuchapa magazeti? je mapato yanatoka wapi? Je Magazeti, redio na tovuti ya Serikali vinajiendesha kutoka pesa gani? je wanavianzio vvya pesa kibiashara amabzo si fungu la Bajeti?
Ndipo narudi kwenye kauli za Mheshimiwa Kikwete. katika kusifia uandishi, katoa tahadhari, onyo na kuonyesha kukwerwa kwa ke kwa habari ambazo ni za upande mmoja, ambazo zinamlena mtu mmoja au taasisi na kazipa jina la Ukanjanja.
Ametoa tamko rasmi kutaka udhibiti wa mfumuko wa Makanjanja na waandishi wawe waadilifu. Amekiri kukerwa sana na huu mfumuko wa Makanjanja!.
Nanukuu
My first reaction was the saga tha led to Mike and Mac the JamboForums operative in ground zero to be arrested!
We live in a modern world where freedom of speech and opinion is the key. Our government is still operating and runs itself in medieval times, enzi za habari kutumia kopo na ngoma kwa chifu!
Uhuru wa habari (information) umefanya Watanzania tuwe mahuiri sana kuchangua mambo mengi mazuri na hata mabaya. Sikatai kuwa mara nyingine, uhuru wetu hukosa mwelekeo au uadilifu na kuishia kuonekana kana kwamba ni uzushi uzushi au ukosefu wa maadili.
Nikajiuliza, hivi Rais Kikwete akisoma ile mada yangu ya Screw Muungwana http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=2204&highlight=screw+muungwana si atapata shinikizo na kuamuru nikamatwe na kuwekwa ndani?
Uhuru wa maoni ni haki ya kila mtu. Sheria za habari zinahusu habari na si maoni! Maoni ni mapokeo na makisio ya mtoa maoni, ndio maana yanaitwa maoni. Maoni yanaweza kuwa na nguvu kubwa za ushawishi hasa ikiwa maoni yanaandamana na vigezo na nyenzo ambazo zaonekana wazi machoni, masikioni na mawazoi pa wasomaji na wasikilizaji.
Maoni kuhusu udhauifu wa Serikali yetu kuhusiana na suala la IPTL,BOT-EPA, Richmond, Radar, Buzwagi, Madini, Kiwira, Uwajibikaji, Ufisadi ulitoka kwa hawa makanjanja na ni ujasiri wao ulioshinikiza Serikali ikae chini na kuamua kufanya ufuatiliaji ambao tayari tunaona matokeo yake.
Walichotumia Makanjanja ni vigezo halisi (facts and data) kuoanisha udhaifu, uzembe na hata ubadhrifu na uhujumu wa wazi ambao ulitishia usalama wa Taifa letu.
Kilichokera na nahisi kndiyo kiini cha kwako mheshimiwa Raisi kufoka kistaarabu, ni unazi wa makanjanja, tunashupalia kwa hali ya juu na hata kuwaumbua na kuwasurubu bila huruma wote ambao wanaelekea ni wazembe, dhaifu, wakiuka maadili na wabangaizaji, wewe ukiwa mmojawapo.
Hivyo basi, nakuomba ujifunze kwenda na wakati na kujua kuwa hatuko kwenye nyakati za Ujamaa au nyakati za Mtawala asemalo basi ni sheria na kila mtu alitetemekee. Ukisema kitu tutakichambua na kama umetoa pumba au ulaghai, tutakwambia wazi bila kuficha.
Wakasirikie wale wanaokudanganya kwa kusema "yes" kwa kila kitu, wao ndio wakosa maadili.

WAVAMIZI wa taaluma ya habari maarufu kama makanjanja, wamemkera Rais Jakaya Kikwete ambaye sasa amewataka wanahabari kuwadhibiti ili kulinda heshima ya taaluma hiyo.
Rais Kikwete alisema hayo jana alipokuwa akizindua Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) katika sherehe zilizofanyika kwenye makao makuu ya shirika hilo, jijini Dar es Salaam.
"Mimi ni mmoja wa watu wanaounga mkono taaluma ya habari. Hivyo, msiiache ikachukuliwa na makanjanja. Nasema haya kutoka rohoni na nina nia njema," alisema Rais Kikwete.
Alisema wavamizi hao wamekuwa wakiivunjia heshima taaluma ya habari kwa kuandika habari za upotoshaji, uzushi na zilizoegemea upande mmoja, kwa nia ya kumbomoa mtu au taasisi kwa maslahi binafsi.
Alisema kama wanahabari wataruhusu taaluma hiyo kuvamiwa na makanjanja, watajuta baada ya kuanza kushambuliana wenyewe kwa wenyewe.
Alisema chombo cha habari kinatakiwa kutangaza habari sahihi na za kweli kama maadili ya taaluma yenyewe yanavyotaka kinyume chake, ni kutowatendea haki na kuwadharau wananchi.
Aliwataka wanahabari kutumia maadili ya taaluma hiyo na kuepuka uchochezi wa kidini na ukabila, lakini akawataka pia kutokuwa waoga na kuoneana haya katika mambo ya msingi yanayikera jamii na Watanzania kwa ujumla.