Serikali funga kampuni ya tigo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali funga kampuni ya tigo

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Ishaka, Feb 23, 2012.

 1. Ishaka

  Ishaka Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 1, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Kinachoendelea sasa hivi katika kampuni ya tiGO in ubabaishaji mtupu uliosheheni wizi na dhuruma kwa wateja kwa zaidi ya miezi miwili sasa! Hivi hawa tiGO mikataba yao ya uwekezaji hapa nchini inasemaje mbona watanzania tunafanyiwa vituko kama vile nchi haina serikali?!

  TiGO wamechoka mbaya nahisi wanaweza kutimka wakati wowote wakaiacha serikali solemba kama ilivyotokea kwa Meridian Beao Bank miaka ya nyuma.

  Kama mitambo ya mtandao wa tiGO ni mibovu isiyotengenezeka na hawana uwezo wa kununua mipya basi ni vema wafunge virago watanzania tumechoshwa kuibiwa na kunyimwa huduma tulizozitarajia.

  Fikiria hata kuongeza muda wa maongezi inakuwa taabu, watu kupiga simu hamsikilizani lakini pesa inakwenda, ukiweka sh. 2,000 ukatuma meseji 14 tu salio limekwisha, ukiongeza salio kutumia tiGO Pesa yaani ujue umekwisha! na usilogwe ukawakopa unapoishiwa salio maana wataendelea kukukata pesa yako kila unapoweka bila wewe kujua.

  Halafu wanakela na mi-message yao ya kijinga ya promotion na upatu kila wakati mchana na usiku wa manane. Naomba mamlaka zinazohusika kuifungia mara moja hii kampuni kimeo ya tiGO.

  Naomba kuwakilisha.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Acha ukenge wewe hii ni free market mtandao haupo m1 hapa tz,kama tiGO wanakuboa unaweza sepa tu,sasa serikali wakifunga hao wafanyakazi utawalipa wewe? Unajua cost za ku-run sites wewe au kujenga mnara m1?

  Unajua vitu vinavyaffect networks hasa hz za MW? Acha umasabauri wewe,mitandao hapa tz hipo kama nane unaweza ukasepa tu,yani kupata msg moja tu unalalamika, mtu mwenyewe unaweka jero baada ya wiki,ndio maana hata ikipotea sh10 unalalamika fanya kazi wewe uongeze kipato chako!
   
 3. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  hamia sasatel kama unataka mtelemko mtandao unaoishia kimara na hauna wateja wengi huko utapeta tuu tuachie na mtandao wetu tumeridhika mi nautumia tangu enzi za mobitel hadi leo tigo then unaleta udaku hapa
   
 4. enhe

  enhe JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 932
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 80
  Waliokutuma wamekupa pesa kiasi gani??
   
 5. K

  Kiumbe duni Senior Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Msimbeze mtoa mada, kuna uwezekano mkubwa hii kampuni imeshauzwa, baadhi ya ofisi zao zimeshahamishwa na minara yao wameshaiuzia kampuni kutoka nje inayoitwa HTT Infranco limited. Si mnaona jinsi walivyo na dharau kwa wateja wao, sababu wanajua hawana watakachopoteza.
   
 6. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hamia Airtel
   
 7. L'AMOUR

  L'AMOUR Senior Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kweli watanzania hawasaidiki hata ukiwapa ushauri gani wao ni kukaidi tu. Nadhani mtoa mada anataka kampuni iboreshe huduma lakini jinsi alivyoshambuliwa utafikiri hao washambuliaji hawakerwi na hili jambo. Jamani kwenye ukweli tupongeze na sio kubisha hata yale ya msingi.
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Haya madongo bila shaka si ya bongo fleva ni yaa taarab!!!!
   
 9. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Wanachofanya Tigo ni sawa na kazi inayofanywa na 'tigo',hakuna tofauti!
   
 10. B

  Bandio Senior Member

  #10
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umemshtukia eh! Kahongwa huyo. Na huu sio uwanja wake. Asante kwa kumgundua mapema.
   
 11. e

  emkey JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 728
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mwambie huyo.
   
 12. e

  emkey JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 728
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kama kuuzwa tigo cyo ya kwanza, mbona celtel na zain ziliuzwa, acha umbea.
   
 13. N

  Ntambaswala JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kuna wahindi wameinunua hii kampuni, ni wajeuri kama nini? hivi serikali ipo kweli? Hapa ofisini tabu tupu wameanza kupunguza wafanyakazi na kupachika wahindi wenzao. Mikataba mingi ya staff inaiisha mwezi huu.
   
 14. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mkuu King Kong III - punguza hasira!
   
 15. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  sure,mtoa mada hapasw kudharauliwa au kubezwa,anaongea kama mteja wa tiGO wa sasa
   
 16. g

  gamshi Member

  #16
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 3, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukweli ni kwamba tigo wamesha shindwa kazi,haiwezekani unampigia mtu simu na simu ina salio la kutosha harafu unaambiwa huna salio la kutosha.Na tabia hii huwa inajitokeza mara kwa mara,pia masikilizano wakati wa mazungumzo huwa yanasumbua sana
   
 17. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Dah jamaa amepanic sana sijui ni mmiliki wa tigo?
   
 18. K

  Kiumbe duni Senior Member

  #18
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Humu jf ukiongelea suala lolote baya kuhusu tigo hata kama ni la kweli unapondwa ile mbaya, hata ukitaka msaada wowote kuhusu tigo husaidiwi, sijui kwa vile ndio wadhamini humu ndani au wameweka watu wao wawalinde yote sijui.
   
 19. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu kama hicho alichoboa huyo mtoa mada analalamika kwa vitu vya kijinga(sio vya kipumbavu),wa-tz tunapenda kulalamika sana,kama ukiolewa huna haja ya kulala na jeans kama umeomua kupanda bito vumulia kubanana otherwise panda libasi likubwa options zipo kibao tu kama hawezi apige kimya.
   
 20. c

  chief72 JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 567
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  hata kama wanaponda ujumbe umefika, tgo hawana lolote hata voda wazushi tu, air tel sijawah kuitumia
   
Loading...