Serikali endelezeni Bandari ya Tanga hakuna haja ya Bandari mpya

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Serikali inatakiwa kuwekeza na kuendeleza bandari ya Tanga badala ya kujenga bandari mpya isiyo na ulazima na kuingiza nchi kwenye madeni yasiyo ya msingi kwa manufaa ya viongozi wachache.

Bandari ya Tanga tayari kuna uwekezaji mkubwa unakuja na pesa za kampuni ya Total ya ufaransa ambayo itatumia Bandari hii kusafisha mafuta. Hivyo ni koongezea pesa ya upanuzi kwenye haya makubaliano na itakuwa nafuu sana kuliko kuanza Bandari mpya kabisa.

Lakini vilevile tunaweza kutumia bomba hilo hilo na mafuta hayo na sisi baadae kujenga sehemu ya kusafishia mafuta Tanga badala ya kutuma magari uganda ya kununua mafuta hata kama tutaanza polepole. Tutakuwa watu wa ajabu kama tutajenga kituo kingine cha usafishaji mafuta wakati tayari kuna hili bomba. Hii itasaidia kuongeza shughuli za kiuchumi pale Tanga.

Kitu kingine ni kwamba Tanga sio mbali na Bagamoyo na Dar es salaama ni maajabu kuwa na Bandari kubwa tatu kwa sehemu fupi hivyo hasa ukizingatia bado tunapanua Bandari zote mbili.

Watanzania tunajua huu ni mradi wa Kikwete na serikali ya China. Wanaisema italeta ajira mpya tuulize kwa soko lipi jipya. Bandari ni lazima iwe na sababu za kujengwa sasa ni soko lipi lipya ambalo tunataka kulihudumia?. Watu wengi wanashangilia pesa za ujenzi ambazo ni madeni ya ajabu kwa vizazi vijavyo tukiulize kuna shighuligani za uchumi kubwa?. Tanga tayari kuna mafuta, Dar kuna Zambia, Rwanda, Burundi, congo na Tanzania .

Kuhusu ile sehemu iliyotengwa . Bado inaweza kuwa sehemu ya mji wa kisasa na kujengwa viwanda, tuweke pipeline ya gas mpaka pale, plant za umeme, na viwanda vidogo vidogo.

Badala ya bandari mpya tuwekeze kwenye Bandari ambayo tayari tuna uhakika itaweza kujiendesha kwa faida kubwa baada ya bomba la mafuta kumalizika ujenzi. Inashangaza wabunge na viongozi wengine wanafungia macho kama vile bandari ya Tanga haipo au hakuna uwekezaji.
 
ni wazo zuri...lakini inabidi kile kisiwa pale kifutwe, ile mikoko kule kama unaeleke Mombasa ifyekwe yoote, na ule mji pale uhame..

Shida ni moja pale, sand deposit ambayo itafanya uchimbuaji wa kina kila mara kufanyika.
kile kisiwa angalau kikiondoka tunaweza kuondoa ule uchochoro na kurahisisha mambo...Yacht club pale inabidi iondoke na maeneo yote yale kuanzia CBA kuzunguka ile kambi ya jeshi mpaka GBP...

Baada ya yote hayo uje uongeze no of berth, uchimbue kina kwelikweli ili mitemba iweze kuingi na kutoka muda woote, ufanye heavy port innovation from the scratch kwa maana ya cranes zile, workshops, lifting equipments zoote, nk..

Hapo sasa utafanya calculation mwenyewe gharama za kujenga port mpya au kuinnovate hiyo ya Tanga...

Idea nzuri pia ambayo inahitaji umafia japo dunia inawenyewe, wakati crude oil pipeline iko kwenye middle stage ya construction tuanze umafia wa siri kujenga refinery plant mahala ( hapa panahitajila umafia)
 
Hela achana nayo kabisa.

Lisu alipohongwa hela akasahau kama alishawahi kuwa mtetezi mkubwa wa madini ya Tanzania.

Kwa sababu ya kuhongwa Waziri Mwambe amemwaibisha Kikwete kuwa aliweka jiwe la msingi bila kuwa na mkataba wowote.
 
Serikali inatakiwa kuwekeza na kuendeleza bandari ya Tanga badala ya kujenga bandari mpya isiyo na ulazima na kuingiza nchi kwenye madeni yasiyo ya msingi kwa manufaa ya viongozi wachache.

Bandari ya Tanga tayari kuna uwekezaji mkubwa unakuja na pesa za kampuni ya Total ya ufaransa ambayo itatumia Bandari hii kusafisha mafuta. Hivyo ni koongezea pesa ya upanuzi kwenye haya makubaliano na itakuwa nafuu sana kuliko kuanza Bandari mpya kabisa.

Lakini vilevile tunaweza kutumia bomba hilo hilo na mafuta hayo na sisi baadae kujenga sehemu ya kusafishia mafuta Tanga badala ya kutuma magari uganda ya kununua mafuta hata kama tutaanza polepole. Tutakuwa watu wa ajabu kama tutajenga kituo kingine cha usafishaji mafuta wakati tayari kuna hili bomba. Hii itasaidia kuongeza shughuli za kiuchumi pale Tanga.

Kitu kingine ni kwamba Tanga sio mbali na Bagamoyo na Dar es salaama ni maajabu kuwa na Bandari kubwa tatu kwa sehemu fupi hivyo hasa ukizingatia bado tunapanua Bandari zote mbili.

Watanzania tunajua huu ni mradi wa Kikwete na serikali ya China. Wanaisema italeta ajira mpya tuulize kwa soko lipi jipya. Bandari ni lazima iwe na sababu za kujengwa sasa ni soko lipi lipya ambalo tunataka kulihudumia?. Watu wengi wanashangilia pesa za ujenzi ambazo ni madeni ya ajabu kwa vizazi vijavyo tukiulize kuna shighuligani za uchumi kubwa?. Tanga tayari kuna mafuta, Dar kuna Zambia, Rwanda, Burundi, congo na Tanzania .

Kuhusu ile sehemu iliyotengwa . Bado inaweza kuwa sehemu ya mji wa kisasa na kujengwa viwanda, tuweke pipeline ya gas mpaka pale, plant za umeme, na viwanda vidogo vidogo.

Badala ya bandari mpya tuwekeze kwenye Bandari ambayo tayari tuna uhakika itaweza kujiendesha kwa faida kubwa baada ya bomba la mafuta kumalizika ujenzi. Inashangaza wabunge na viongozi wengine wanafungia macho kama vile bandari ya Tanga haipo au hakuna uwekezaji.
🙏
 
Back
Top Bottom