Serikali: Biashara 16,252 zafungwa na 147,818 zafunguliwa kwa kipindi cha Julai, 2018 hadi Aprili, 2019

Biashara nyingi zilikuwa za michepuko wanaopelekwa China na vigogo... sasa vigogo wako back to their families....
 
Haka kabibi kapuuzi kweli yan!
 
Kama ndivyo kwanini Dr.Mpango kipindi cha Bunge hili hili la Bajeti aliwazuia TRA kufungia biashara?
 
Reasoning ya namna gani hii
Clueless Hutus, mxieeew!

Kwa hiyo wewe Mzee Mwanakijiji Shoprite na Nakumatt wakifunga maduka yao, Fastjet ikafa, Bakhresa akapitisha mizigo yake Bandari ya Mombasa badala ya Dar Port na wafanyabiashara wa Kariakoo wakafuata mizigo Kampala badala mzigo uwakute hapo Kariakoo....

halaf nyinyi kwa akili zenu za Kihutu mkatoa vitambulisho vya wamachinga 165,000 na kufungua vibanda vya chips na Mpesa kila kona ya mtaa ndo akili yako inakutuma kuwa biashara zilizokufa/kufungwa ama kuhamishwa ni pungufu kwa thamani na idadi ya hivyo vitambulisho vya wamachinga mlivotoa?
 
Biashara zilizofungwa na impact yake tunaiona huku mitaani. Hizo zinazofunguliwa hatuzioni wala impact yake haionekani? Sijui takwimu hizi za serikali zinakusanywaje?
 
Kariakoo ilikuwa supermarket ya nchi za Africa mashariki na kusini! Na walioendesha biashara hapo ni vijana wa kitanzania (na wala si watanzania wenye asili ya kiasia)! Siasa yao iikuwa kutafuta pesa! Leo hii wengi wamefunga biashara. Wewe unadai walikuwa hawalipi kodi na walikuwa wanatakatisha fedha za wizi! Ni madai yasiyo sahihi. Lakini hata kama ni sahihi je nchi ilikuwa haifaidiki kwa biashara hiyo? Ni upofu kufikiri kwamba biashara itafanywa na malaika wasio kwepa kodi. Tujifunze kutoka nchi zilizoendelea Marekani na marafiki zetu wachina wakiwemo. Hawa wanasupport wafanyabiashara wao kwa kila hali.
 
Tunaomba picha ya atleast ya fremu tatu zinazotafuta wapangaji kkoo sasa hivi na kipindi hicho zikiwa zimejaa.

Si unajua fact ndio uhai wa mjadala wowote ule???
 
Hakuna kitu kama hivyo Kariakoo ilikuwa inatumika sana na Money Launders kusafisha pesa za wizi sasa wamebanwa ndiyo maana wanafunga na wengi wao walikuwa hawalipi kodi

We buku 7 yako imekatwa kodi?
 
Mkuu wengi hapo walikuwa madalali wafanyabiashara halali hapo walikuwa wanaumia sana hujui tu. Pesa za kutakatisha hazijawahi endeleza nchi.
 
Kama serikali kwa sasa inakusanya mapato ya trilioni 1 kwa mwezi, basi makusanyo yameshuka kuliko wakati wa Jakaya.

Wakati wa Jakaya, makusanyo yalikuwa bilioni 900, bila ya kuhusisha makusanyo ya halmashauri kama vile ya ardhi na majengo, bila kuhusisha mapato ya agencies mbalimbali kama vile TANAPA, mahospitali, n.k.

Lakini keo kila kitu kinaenda mfuko mkuu, jumlisha na depreciation ya shilingi, makusanyo trilioni moja!! Nchi inasonga kwa kurudi nyuma.

Uchumi wa nchi unadidimia lakini wa chattle na wanachattle unapaa maana mpaka Intern Airport ipo.
 
Macho yenu ni mabovu
 
Ndiyooo niliyasema juzi..mtu anasema "biashara zinafungwa" tunamuuliza kulinganisha na nini na lini? Chegeni (au mwingine) anachoweza Ni kuoneshwa takwimu zinazopingana na hizi za serikali
Tuache habari zenu za takwimu! Je nikikuonyesha maduka 100 yaliyofungwa kwenye mtaa mmoja je wewe Utaweza kunionyesha biashara 200 zilizofunguliwa kwenye mtaa huo huo? Sasa hivi kwa maneno kama haya ndiyo nimeamini Haki ya Mungu kuwa kumbe ni kweli kabisa kuwa huwa mnatuona sisi ni wapumbavu!!! Na kwa hili roho inaniuma kweli! Hapa mtaani ninapoishi palikuwa na maduka sita! Sasa hivi yamebaki mawili tu,nna moja nalo linapumulia mrija!! Hakuna duka jipya lililofunguliwa hapa zaidi ya kiji saloon kidogo cha kunyolea kwenye kibanda ambacho awali kilikuwa stationary na ikafungwa pia!! Halafu we mzee si ulishahama nchi? Mbona unawasaidia watesaji wa ndugu zako?huna hata binamu aliyebaki Tanzania mzee wetu? Au wewe wanakupa nini? Basi tu! Tunamwachia Mungu
 
Sijawahi kuwapinga hawa watu kwenye takwim zao ila hili wamechemka sana... Watawadanganya wananchi wanaokaa sehemu moja tangu waingie awamu ya 5. Lakini kwa tuliozoea kuzunguka tangu awamu zilizopita hadi hii tulishakuwa tukiona biashara nyingi na kila siku zinafungwa, na anaefungua inakuwa chini ya ile iliyokuwepo mwanzo, ambayo nayo itaenda muda mfupi sana inafungwa pia.. Tatizo kwasasa biashara kukua ni ngumu sana ila Tra wao ukishapita mwaka hawaangalii kama biashara yako imekua au imedumaa wao wanaongeza kiwango cha kodi coz huo ni mwaka mwingine haiwezi kodi kubaki palepale... Sasa kama faida nikipata kwa mwaka m4 unanipangia kodi m1.2 hapo sijalipa frem la biashara, pango la kuishi, watoto hawana ada na kodi za ndani ya mji zilivyo nyingi mwisho unaona kama hujatumia mtaji basi umebaki palepale kwanini usifunge ukalime tu... Hawa watu wanapotosha ukweli kumridhisha mtu, hawajui hali ikiachwa hivi itakuwa shida sana kuirejesha kama mwanzo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…