Bajeti ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,854
930

BAJETI YA WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb,) amesema ndani ya mwaka mmoja, mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi imetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 713.8.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo bungeni Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara kwa mwaka 2023/24.​


Dkt. Kijaji ameliomba bunge kupitisha bajeti ya zaidi ya Shiling bilioni 119.018 na kati ya hizo Sh 43.566 zinaombwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ambapo Sh bilioni 30.347 ni fedha za ndani na Sh bilioni 13.22 ni fedha za nje.

katika kukuza ushiriki wa wananchi kwenye shughuli za kiuchumi katika kipindi cha Julai 2022 hadi Machi, 2023, mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi zimetoa mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 713.8.

“Mikopo hiyo imetolewa kwa wajasiriamali 2,203,838 na kati yao wanawake ni 1,234,149 sawa na asilimia 56 na wanaume 969,689 sawa na asilimia 44.”

Mhe. Dkt. Kijaji amesema kuwa uchambuzi wa mikopo hiyo unaonesha jumla ya ajira 3,122,104 zilizalishwa, kati ya ajira hizo, wanawake ni 1,623,494 sawa na asilimia 52 na wanaume ni 1,498,610 sawa na asilimia 48.

“Mikopo hiyo imetolewa katika sekta mbalimbali za kiuchumi ikiwemo sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi ambazo ni asilimia 31.07, ikifuatiwa na sekta ya viwanda na biashara kwa asilimia 20.39.” Amesema Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji ameongeza kuwa katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Machi, 2023, Wizara kupitia Mfuko wa Taifa wa Kuendeleza Wajasiriamali Wananchi (NEDF) imetoa jumla ya mikopo 1,474 na kati ya hao wanawake ni 668 sawa na asilimia 45.3 na wanaume ni 806 sawa na asilimia 54.7 yenye thamani ya Sh bilioni 3.50.​


Alisema pia mikopo 516 sawa na asilimia 35 yenye thamani ya Sh bilioni 1.225 ilitolewa kwa miradi ya vijijini. Dk Kijaji alisema mikopo hiyo iliweza kuzalisha ajira 5,489 ambapo wanawake ni wanawake 2,668 sawa na asilimia 48.6 na wanaume ni 2,821 sawa na asilimia 51.4.

Ameongeza kuwa wizara imeweza kuwaungisha wajasiriamali 13 ambao walipata mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 1.151 kupitia Benki za Azania na CRDB ambapo jumla ya ajira 259 zimezalishwa.​

 

Attachments

  • FvRhqo1XsAYAJPG.jpg
    FvRhqo1XsAYAJPG.jpg
    60.3 KB · Views: 4
  • FvStDO6WYAIleQh.jpg
    FvStDO6WYAIleQh.jpg
    111.6 KB · Views: 4
  • FvRpCkHWwAIrEnp.jpg
    FvRpCkHWwAIrEnp.jpg
    157.9 KB · Views: 5
Back
Top Bottom