Serikali Awamu ya Sita kuifungua Mtwara?

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
unnamed (2).jpg

Katika sera ya utawala bora ni pamoja na kuhakikisha maendeleo sawia katika kanda zote za nchi husika. Ni ukweli usiopingika kuwa katika miongo kadhaa iliyopita tangu nchi ya Tanganyika ijipatie uhuru na baadae Tanzania, Moja ya maeneo yaliyokuwa nyuma sana hata baada ya uhuru ni maeneo ya ukanda wa kusini.

Maeneo hayo ambapo mkoa wa Mtwara Lindi imekuwa ikiwa nyuma kimaendeleo ikiringanishwa na mali asili zipatikanazo maeneo hayo, haswa bahari, kilimo cha korosho, utalii wa fukwe na kadharika.

Hali hii imekuwa ni mtambuka na sasa Serikali ya awamu ya sita chini ya jemedali na mzalendo namba moja Rais Samia Suluhu Hassan ameamu kuifungua kanda ya kusini kwa kuboresha miundo mbinu ya usafirishaji haswa bandari ya mtwara.

Maono yake Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ya kuipanua bandari hii ya Mtwara imekuwa inatija sana si katika mkoa wa Mtwara tu bali katika ukanda wote wa kusini.

Ujenzi wa gati jipya katika bandari hiyo imeongeza mapato mara dufu katika mkoa huo wa Mtwara. Gati hilo jipya lenye urefu wa mita 300 limeiwezesha bandari hiyo kuhudumia meli zenye uzito wa 65,000.

Imeelezwa kuwa kuongezeka kwa gati jipya katika bandari ya Mtwara kumeongeza mapato yanayokusanywa katika Bandari hiyo kutoka bilioni 14 kwa mwaka 2020 na kufikia bilioni 23 kwa mwaka 2022.

Jana tarehe 12/7/2022 Naibu Waziri Uchukuzi Mwakibete akiwa mkoani Mtwara kwa ziara ya siku mbili ya kukagua miundombinu inayosimamiwa na taasisi za sekta hiyo, Akizungumza mara baada ya kutembelea Bandari hiyo Atupele Mwakibete amesema "kukua kwa mapato hayo kumechangiwa na maboresho yaliyofanywa katika bandari hiyo kwa kuongeza gati nyingine kubwa yenye uwezo wa kuhudumia meli yenye uwezo wa kubeba tani takribani elfu 65."

“Serikali imewekeza hapa na ndio maana tunaona matokeo ya kupanda kwa mapato lakini hii isiishie hapa tunahitaji mapato zaidi kwani mzigo wa kupitisha hapa upo wa kutosha ambapo kama tutajipanga vizuri basi tunaweza kukusanya zaidi’ amesema Naibu Waziri Mwakibete.

Naibu Waziri Mwakibete ameeleza umuhimu wa kutangaza zaidi bandari hiyo na kusema kuwa bila kuitangaza bandari hiyo makampuni makubwa kama ya simenti, makaa ya mawe, korosho yanaweza kuendelea kutumia barabara badala ya kutumia bandari.

Aidha, Naibu Waziri Mwakibete amewataka TPA kuitisha vikao vya mara kwa mara vitakavyowakutanisha na wadau wote wa usafiri na usafirishaji ili kujadili namna nzuri ya kutumia bandari hiyo ambayo imeboreshwa kwa kutumia zaidi ya bilioni 150.

Naye Meneja wa bandari ya Mtwara, Abdilah Salim amemuhakikishia Naibu Waziri Mwakibete kuwa TPA iko kwenye mpango wa kutenga maeneo kwa wafanayabiashara wakubwa kama Dangote anayesafirisha simenti na Kampuni ya Ruvuma ambayo inasafirisha makaa ya mawe na wasafirishaji wa korosho ili kuhakikisha wanasafirisha mizigo yao kwa wakati bila changamoto zozote.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano, Thomas Mushi amesema tayari juhudi mbalimbali zimeanza kufanyika kwa kuitangaza bandari hiyo ndani na nje ya nchi ili kuwavutia wasafirishaji wengi hususani wa Nchi za Zambia na Malawi ambao wanatumia bandari ya Dar es Salaam.

Hakika Maono ya Mama ni makubwa na tuendelee kumpatia ushirikiano thabiti.
 
Wamakonde bana waendelee kulala tu hawa hata ukiwapa li nchi zima watalalamika tyuuuuuu!!! Gas tumewapa msaada mmeiacha ikaenda nchumbiji!!...wavivu wavivu tu!

hilo limkoa wenu mtajenga wenyewe tu! hkn namna!...acheni kulalama si mwende mikoa mingine makachume mje mjenge kwenu?? mbona wachaga/wakinga/wakurya/ wapare wanafanya hayo??

hawa ni kuwachapa viboko tyuuu! akili ikae sawa!
 
Back
Top Bottom