Serikali angalieni kwa jicho la huruma Dada zetu wanaofanya kazi kwa Wahindi

Wahindi ukisaini mkataba nao umekwisha,unaweza kuwa ni machine operator ukashangaa siku kazi hamna au umemaliza mapema ukachukuliwa ukapelekwa kweny kubeba mizigo qu kufagia.

Kuna msela alikuwa dereva wa gari ya muhindi anakuambia siku nyingine anatakiwa kuliosha gari na kuna siku anaambiwa akasafishe store .
Uzuri akiacha wengine wanakuja
 
Kwani ni lazima kuajiriwa, wanashindwaje kujiajiri baada ya kupokea mshahara?
Umesoma ulichokiandika hapa kabla hujaki-post?nadhani kuna umuhimu wa kutafakari kabla hujatamka kitu.

Una marafiki wangapi wameajiriwa wanalipwa zaidi ya 500K na hawajajiajiri?ndugu zako wangapi unawajua wameajiriwa wanalipwa (hata wewe unaweza kuwa umeajiriwa na bado hujaweza kujiajiri) lakini hadi leo wanatumwa tu huyo house girl wa muhindi analipwa million ngapi kiasi yeye iwe rahisi kwake kujiajiri?
 
Labda nikung'ate sikio ndugu kwa kunong'ona


Hawa wahindi ndio Wafadhili Wakuu wa kile Chamaa. Sijui umenisikia
 
Kila mmoja anataka apate mlo wake, hata wewe kuna wanaokuhurumia kuzunguka kwenye mvua na jua na tenga kila siku huku wakijisemea hivi kashindwa kujichangisha akanunua hata pikipiki?

Kuna kima cha chini cha mshahara na ni wajibu wa serikali kufuatilia hilo na sio sisi
 
Itoshe kusema hao ndugu ndo maana mara nyingi hawafilisikagi kazi to kazi😃😃

Pia hao wafanyakazi labda ndo wale walipiga walimu shule/walikataa shule au waligomea ushauri wa walezi wao wakafata ujinga wao!!

Wacha akili ziwakae sawa
 
Ajira nyingi zisizo na mikataba iwe kwa Wafanyakazi wa ndani ama viwandani iwe kwa wageni ama kwa wabongo wenzetu Serikali ni kama haiwasaidii pamoja na kuweka Kima cha Chini cha Mshahara pamoja na Sheria za kuwalinda.

Kuna haja Serikali chini ya Wizara ya Ajira na Makundi Maalumu waone namna ya kuwasaidia kundi hili.

Ukienda Kwenye Viwanda vya Mo, Azam ama kwenye viwanda vya Nondo vya wale wahindi pale Mikocheni utashangaa watu wanavyofanyishwa kazi bila mikataba wala nini.

Ikitokea umefariki hakuna hata cha Mkono wa Pole wala nini.


Mamlaka zitilie Mkazo jambo hili.
 
Wanaofanya kwa waswahili maslahi yao yakoje? Ni wangapi wanapata mshahara wa laki moja tu kwa mfano?
Nyani haoni kundule 🤣🤣🤣
Kwa waswahilo watu wanalipwa 30 ikizidi 50k,

Ila leo et wanawasema wahindi hawalipi vizuri hahahah,

Btw, wadada wakazi inabidi serikali iangalie jinsi ya kuwasaidia, mishahara yao ipande pande aiseeee
 
Back
Top Bottom