Lamzettttt
JF-Expert Member
- May 28, 2020
- 1,031
- 3,123
Salaam
Kama ilivyo ada mimi ni muuza mboga mboga mjini pale Dar es Salaam nikiwa na tenga langu kichwani asubuhi tu nipo nazunguka mitaa ya mjini pale Posta, Upanga yote asubuhi, huwa naumia roho sana ninapoona mazingira na hali ambazo wanakuwa nazo dada zetu wa Kitanzania katika nchi yao ni kama vile wapo Ughaibuni.
Kazi zao ni ngumu, mshahara ni mdogo lakini watafanyaje tu vile wanaishia kukomaa tu na kutoa malalamiko yao kwa sisi wauza mboga asubuhi tunapowapelekea.
Hebu serikali kupitia Wizara ya Kazi kama ipo angalieni raia wenu hawa fuatilieni maendeleo yao kwa kweli hawana wa kuwasema ni kama vile wapo nchi ambayo sio yao.
Kazi wafanyazo hazina mikataba, mshahara ni mdogo, hawana bima yoyote, wanaachishwa kazi kiajabu ajabu, hamna mafao, kiinua mgongo wala nauli pindi waachishwapo kazi, nao ni wananchi wenu, viongozi tuonesheni umoja basi.