Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 38,399
- 47,783
Wale wanaopinga serikali 3 wana hoja na hofu za msingi japo huwa hawasemi sana. Tatizo kubwa la serikali tatu ni serikali ya Tanganyika yenye nguvu zilizopitiliza ambayo inaweza kumpuuza Rais wa Jamuhuri wakati wowote.
Serikali moja kwa upande mwingine haitakaa ikubalike na Zanzibar. Tayari wana serikali kwa sasa na kwa maana hiyo kukubali kumezwa kabisa kuwa sehemu ya Tanzania itakuwa kivumbi cha aina yake, kama Nyerere hakuweza wakati huo sio rahisi mwingine kuweza kwa sasa.
Serikali 2 zenye mfumo ulioboreshwa ndio muafaka wa dilemma hii. Tujifunze na ikiwezekana tuige mfumo wa "China wa One country two systems". Tanzania na Zanzibar kwa sehemu kubwa zibaki kama zilivyo na mifumo yake ya msingi ya uongozi ila tufanye mambo kadhaa kuboresha.
1. Tuondoe wabunge wa Zanzibar kuwa sehemu ya bunge la sasa la Tanzania. Wabaki katika bunge lao tu.
2. Tuondoe takwa/hitaji la katiba la mmojwapo kati ya Rais wa Tanzania au makamu kutoka Zanzibar.
3. Zanzibar ipewe rasmi kikatiba 10% ya viti vya ubalozi.
4. Zanzibar ipatiwe fursa za kidiplomasia kwa mfano uanachama kamili katika mashirika kadhaa ya kimataifa kama OIC.
5. Kuundwe bunge la seneti lenye wawakilishi 2 kutoka kila mkoa Tanzania bara na Zanzibar. Hili liwe linapitisha bajeti na maamuzi yote kutoka bunge la sasa kwenda kwa Rais wa Tanzania.