Serikali 3 au 1 ni mwisho wa muungano. Zibaki 2, Zanzibar iwe na hadhi maalumu kama Hong-Kong

Uzalendo ni kutekeleza kile ambacho wananchi walikipendeza katika tume ya Warioba mfumo wa sekari 3 huo ndio uzalendo
Hatutaki
Hata Zanzibar hawataki..
Kama ni Kuvunja Muungano tuuvunje Tu ... tusitumie serikali tatu kama kichaka
 
tugawane , mbao mtu akiwa nje ya muungano ndio atajua faida na hasara. alitaka kuungana atakuwa na adabu.
hawastahili hata asilimia Moja ya vitu vya ubalozi kwani hawachangii hata senti Tano kuendesha nchi
Kwa nini wachangie wakati wao huo muungano wenyewe hawautaki nyinyi watanganyika ndio munaulazimaisha huo muungano
 
Wale wanaopinga serikali 3 wana hoja na hofu za msingi japo huwa hawasemi sana. Tatizo kubwa la serikali tatu ni serikali ya Tanganyika yenye nguvu zilizopitiliza ambayo inaweza kumpuuza Rais wa Jamuhuri wakati wowote.

Serikali moja kwa upande mwingine haitakaa ikubalike na Zanzibar. Tayari wana serikali kwa sasa na kwa maana hiyo kukubali kumezwa kabisa kuwa sehemu ya Tanzania itakuwa kivumbi cha aina yake, kama Nyerere hakuweza wakati huo sio rahisi mwingine kuweza kwa sasa.

Serikali 2 zenye mfumo ulioboreshwa ndio muafaka wa dilemma hii. Tujifunze na ikiwezekana tuige mfumo wa "China wa One country two systems". Tanzania na Zanzibar kwa sehemu kubwa zibaki kama zilivyo na mifumo yake ya msingi ya uongozi ila tufanye mambo kadhaa kuboresha.

1. Tuondoe wabunge wa Zanzibar kuwa sehemu ya bunge la Tanzania. Wabaki katika bunge lao tu.

2. Tuondoe takwa/hitaji la katiba la mmojwapo kati ya Rais wa Tanzania au makamu kutoka Zanzibar.

3. Zanzibar ipewe 10% ya viti vya ubalozi.

4. Zanzibar ipatiwe fursa za kidiplomasia kwa mfano uanachama kamili katika mashirika kadhaa ya kimataifa kama OIC.

5. Kuundwe bunge la seneti lenye wawakilishi 2 kutoka kila mkoa Tanzania bara na Zanzibar. Hili liwe linapitisha bajeti na maamuzi yote kutoka bunge la sasa kwenda kwa Rais wa Tanzania.
Nn faida ya huu Muungano kwa Tanganyika.Tunaitaka Tanganyika yetu
 
Naogopa kuzungumzia muungano maana Wazenchi wataniparura
 
Serikali mbili au tatu hazitaweza kuimarisha muungano hata chembe.
Zanzibar yenye mamlaka yake kwenye mambo yanayoitwa yasiyo ya muungano itatamani kuwa na mamlaka kamili kwa mambo yote. Na hili linakwenda hatua kwa hatua. Linganisha mamlaka ya Zanzibar huko nyuma na sasa.
Tanganyika(Hii ipo kwa sababu Zanzibar ipo) kwa upande mwingine, kwa kadiri mamlaka ya Zanzibar yanavyozidi kujitanua, itaona kama yenyewe tu ndio iliyopoteza mamlaka yake tu.

Suluhisho ni serikali MOJA nchi MOJA TANZANIA.
Kiongozi akiwa katoka Zanzibar itakuwa sawa na aliyetoka Tabora tu maana ni Mtanzania. Hakutakuwa na Mzanzibari na Mzanzibara. Yaani mzanzibari amiliki ardhi nanjilinji sawasawa na muchari amiliki ardhi chakechake au matangatuani huko maana kote ni ardhi ya Tanzania.
Wewe ni mtanganyika hujui Thamani ya Nchi ndio maana NChi yako Tanganyika huijui hata iko wapi
 
Wale wanaopinga serikali 3 wana hoja na hofu za msingi japo huwa hawasemi sana. Tatizo kubwa la serikali tatu ni serikali ya Tanganyika yenye nguvu zilizopitiliza ambayo inaweza kumpuuza Rais wa Jamuhuri wakati wowote.

Serikali moja kwa upande mwingine haitakaa ikubalike na Zanzibar. Tayari wana serikali kwa sasa na kwa maana hiyo kukubali kumezwa kabisa kuwa sehemu ya Tanzania itakuwa kivumbi cha aina yake, kama Nyerere hakuweza wakati huo sio rahisi mwingine kuweza kwa sasa.

Serikali 2 zenye mfumo ulioboreshwa ndio muafaka wa dilemma hii. Tujifunze na ikiwezekana tuige mfumo wa "China wa One country two systems". Tanzania na Zanzibar kwa sehemu kubwa zibaki kama zilivyo na mifumo yake ya msingi ya uongozi ila tufanye mambo kadhaa kuboresha.

1. Tuondoe wabunge wa Zanzibar kuwa sehemu ya bunge la Tanzania. Wabaki katika bunge lao tu.

2. Tuondoe takwa/hitaji la katiba la mmojwapo kati ya Rais wa Tanzania au makamu kutoka Zanzibar.

3. Zanzibar ipewe 10% ya viti vya ubalozi.

4. Zanzibar ipatiwe fursa za kidiplomasia kwa mfano uanachama kamili katika mashirika kadhaa ya kimataifa kama OIC.

5. Kuundwe bunge la seneti lenye wawakilishi 2 kutoka kila mkoa Tanzania bara na Zanzibar. Hili liwe linapitisha bajeti na maamuzi yote kutoka bunge la sasa kwenda kwa Rais wa Tanzania.
Umeiweka vizuri, umeleta suluhu ya kuondoa 'usisi' na 'wao' halafu kuna sehemu umerudisha tena tatizo la 'sisi' na 'wao'.

Unapoleta suluhu inayofuta pande mbili na kuleta sura ya kitaifa, halafu in between unasema wale wapewe % fulani halafu wapewe hadhi fulani unakua Umelirudisha tatizo palepale ulipolikuta.
 
Kwa nini wachangie wakati wao huo muungano wenyewe hawautaki nyinyi watanganyika ndio munaulazimaisha huo muungano
Wewe nani kakuambia Zanzibar hawautaki huu muungano??
Bakhresa anaweza kuukataa huu muungano??
Wazanzibari na familia zao waliooana na wabara, waliojenga bara, walioajiriwa bara na wanaofanya biashara za kila aina bara wana sababu gani za kuukataa muungano??
 
Sababu zote zinazofanya hadi sasa tuwe na mambo ya Muungano.
Nakuhakikishia MUUNGANO imara utapatikana pale ambapo pande zinazounda muungano zitakapokubali kupoteza mambo yote na kuyakabidhi kabisa kwenye hiyo nchi moja unganishi.
Mbona suala rahisi tu umeulizwa unazunguka tu? Suala kama wewe ungekuwa ni mzazibari ungekubali Nchi yako kumezwa kabisa na isiwepo
 
Umeiweka vizuri, umeleta suluhu ya kuondoa 'usisi' na 'wao' halafu kuna sehemu umerudisha tena tatizo la 'sisi' na 'wao'.

Unapoleta suluhu inayofuta pande mbili na kuleta sura ya kitaifa, halafu in between unasema wale wapewe % fulani halafu wapewe hadhi fulani unakua Umelirudisha tatizo palepale ulipolikuta.
Hii sio suluhu ya kufuta pande mbili, ni ya kuondoa malalamiko makubwa ya msingi ya pande mbili na kuzifanya ziwe katika mpangilio bora zaidi ambao unaleta tija kwa wote.
 
Wanaweza pia kuwa wanaung'ang'ania kwa sababu ndio huu tu wanaoujua na hawana uhakika aina nyingine ya muungao utaleta matokeo gani. "Fear of unknown"
Itakuwa ule msemo wa nyumba uloizowea kuihama ina tabu
 
Hii sio suluhu ya kufuta pande mbili, ni ya kuondoa malalamiko makubwa ya msingi ya pande mbili na kuzifanya ziwe katika mpangilio bora zaidi ambao unaleta tija kwa wote.
Sasa nduyo haitaondoa malalamiko, sababu upande mwingine baada ya kumya cha muda mrefu na kuonekana kama wanawanyonya wale wengune, na wao sasa wameamua kuanza kulalamika. Sasa ukusema ushughulikie matatizo ya upande mmoja unakua unazidi kuleta uhasama
 
Nimeweka hoja 5 mezani ambazo naamini zitakuza maslahi ya pande zote huku pande zote zikiwa na maamuzi makubwa zaidi ya mambo yake kuliko ilivyo sasa kwa mabadiliko kiasi katika mfumo huu uliopo sasa wa serikali 2. Ungechambua kwa kurejea hoja moja baada ya nyingine.
 
"Kuundwe Bunge la JMT la seneti lenye wawakilishi 2 kutoka kila mkoa Tanzania Bara na Zanzibar"

Nakubaliana kabisa na wazo hili, kwani ndilo Bunge pekee ambalo litakuwa na hadhi kujadili na kupitisha bajeti ya wizara zenye kubeba masuala ya muungano.
Wale wanaopinga serikali 3 wana hoja na hofu za msingi japo huwa hawasemi sana. Tatizo kubwa la serikali tatu ni serikali ya Tanganyika yenye nguvu zilizopitiliza ambayo inaweza kumpuuza Rais wa Jamuhuri wakati wowote.

Serikali moja kwa upande mwingine haitakaa ikubalike na Zanzibar. Tayari wana serikali kwa sasa na kwa maana hiyo kukubali kumezwa kabisa kuwa sehemu ya Tanzania itakuwa kivumbi cha aina yake, kama Nyerere hakuweza wakati huo sio rahisi mwingine kuweza kwa sasa.

Serikali 2 zenye mfumo ulioboreshwa ndio muafaka wa dilemma hii. Tujifunze na ikiwezekana tuige mfumo wa "China wa One country two systems". Tanzania na Zanzibar kwa sehemu kubwa zibaki kama zilivyo na mifumo yake ya msingi ya uongozi ila tufanye mambo kadhaa kuboresha.

1. Tuondoe wabunge wa Zanzibar kuwa sehemu ya bunge la Tanzania. Wabaki katika bunge lao tu.

2. Tuondoe takwa/hitaji la katiba la mmojwapo kati ya Rais wa Tanzania au makamu kutoka Zanzibar.

3. Zanzibar ipewe 10% ya viti vya ubalozi.

4. Zanzibar ipatiwe fursa za kidiplomasia kwa mfano uanachama kamili katika mashirika kadhaa ya kimataifa kama OIC.

5. Kuundwe bunge la seneti lenye wawakilishi 2 kutoka kila mkoa Tanzania bara na Zanzibar. Hili liwe linapitisha bajeti na maamuzi yote kutoka bunge la sasa kwenda kwa Rais wa Tanzania.
Lakini pia muundo wa uongozi wa serikali ya Zanzibar utapasa ubadilishwe. Iondolewe nafasi ya Rais wa Zanzibar na badala yake iwekwe nafasi ya Waziri Mkuu.

Hapo kutakuwa na mawaziri wakuu wawili kutoka Tanzania Bara na Visiwani, ambao wote watapaswa kuwajibika kwa Raisi wa JMT, na wote wawe viongozi wa shughuli za serikali bungeni katika masuala ya wizara zote zisizokuwa za muungano.
 
Back
Top Bottom