Serikal yaongeza mishahara ghafla?

Serikal yaongeza mishahara ghafla?

mkuu hebu uwe siriazi bana, hizi ni tetesi ama???.....mbona utanifanya niende kukopa tena lol!

Wala usijaribu kujitusu bibie, kama serikali imesitisha nyongeza ya mishahara kwa waliopanda vyeo na hata ajira vipi kuhusu kuongeza mishahara????

Huo ni uongo wa waziwazi.
 
ina maana zaid ya walivyoongeza mwez wa saba wameongeza tena??? imetumika sheria gani kuongeza ama lile ongezeko la mwez wa saba walituchakachua??
Mama Klein mambo? hivi unaamini kuwa serikali hii ya bro. inaweza ?
 
Gazeti linaeleza kuwa nyongeza ni kwa waraka wa mwezi Julai. sina hakika lakini nahisi si ntongeza mpya ila ni kitu kilishafanyika ila gazeti limeandikwa habari iliyopitwa na wakati. Ni mtazamo wangu.
mkuu gazeti linatuuza, hii issue ilitokea tangia July, wao ndo wanaandika leo!!!!!
 
*Yapandisha mishahara ya vigogo ghafla

*Waziri Kombani adai imefuata taratibu
*Wengine waongezewa Sh milioni moja

SERIKALI imefanya marekebisho ya mishahara kwa watumishi wake kwa mwaka wa fedha 2012/2013, MTANZANIA imebaini. Sambamba na hilo, mishahara ya viongozi wa Serikali kwa mwaka huo wa fedha, nayo imefanyiwa marekebisho.

Marekebisho hayo ni kwa mujibu wa waraka wenye kumbukumbu namba S/AC 205/ 399/ 01/ 44, kutoka Ofisi ya Rais Ikulu (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), uliotolewa Julai 25, mwaka huu.

Waraka huo, umesambazwa kwa wakuu wote wa idara za Serikali, wakurugenzi wa majiji, manispaa, miji na wakurugenzi wa halmashauri zote za wilaya nchini.

Waraka huo, uliosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu (Utumishi), Hab Mkwizu, umehusisha pia marekebisho ya ngazi za mishahara kwa viongozi hao wa Serikali.

Kwa mujibu wa waraka huo, ngazi za mishahara zilizokuwa zinaanzia TGS I hadi TGS Q, zimebadilishwa na sasa zitasomeka LSS (E) 1 hadi LSS (E) 9.

Watumishi na viongozi wa Serikali walionufaika na marekebisho hayo, ni pamoja na makatibu wakuu wa wizara, manaibu wao pamoja na wakurugenzi wa idara zote za Serikali. Marekebisho hayo yameanza kutekelezwa Julai, 2012.

Hata hivyo, marekebisho hayo yamelalamikiwa na baadhi ya watumishi wa Serikali, wakidai kuwa hayana uwiyano unaoeleweka kati ya mishahara ya wamtumishi wa Serikali.

Marekebisho hayo yanaoneshwa katika kiambatanisho namba 1 cha waraka huo, ambapo watumishi na viongozi hao wameongezewa mshahara usiopungua 400,000.

Mfano mshahara wa mtumishi wa ngazi TGS P, umepanda kutoka Sh 3, 216, 000 hadi Sh 4, 500, 000 katika ngazi mpya ya LSS (E) 9, ongezeko ambalo ni zaidi ya Sh milioni moja.

Mmoja wa wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alikosoa marekebisho hayo na kusema kuwa, hayana uwiyano mzuri kati ya mshahara wa mtumishi na mtumishi mwingine.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani, amekiri kuwapo kwa marekebisho hayo ya mishahara kwa watumishi na viongozi wa Serikali.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu, Kombani alisema, marekebisho hayo ni ya kawaida na kwamba yanawagusa watumishi wote wa Serikali bila kubagua.

“Serikali ikifanya marekebisho ya mishahara, inafanya hivyo kwa watumishi wake wote. Hatuchagui nani aongezewe nani asiongezewe ni wote,” alisema.

Alisema vigezo vilivyotumika katika marekebisho hayo, ni pamoja na aina ya kazi, uzoefu na muda aliotumia mtumishi kukaa kazini.

“Unauliza kwanini watumishi wengine wamepewa nyongeza kubwa na wengine kidogo, ndugu yangu sifa zinatofautiana, mtumishi anayeanza kazi leo, hawezi kulipwa mshahara na mtumishi aliyepo kazini kwa miaka 20,” alisema.

Alipoulizwa ni sababu zipi zilizoifanya Serikali kurekebisha ngazi ya mshahara kutoka TGS na sasa kutumia ngazi mpya ya LSS, Waziri Kombani alisema. “Hayo ni masuala ya kitaalamu zaidi.”

Kombani alikiri kima cha chini cha mshahara ni kidogo na kueleza kuwa, Serikali ipo katika majadiliano.

“Kima cha chini kilipanda kutoka Sh 130, 000 hadi Sh 170, 000. Tunajua kima hiki hakitoshi lakini tupo katika majadiliano,” alisema.
 
hata siye wafanyakazi wa chuo kikuu cha DSM hatujapewa mishahara mipya toka ilivyopandishwa July
 
Source:Mtanzania Jumatatu

..........kima cha chini wanajadiliana ila wenyewe wanajiongezea mamilioni? Poleni watumishi wa serikali 'sikivu'......
 
hivi wewe unakunywa kinywaji gani wewe??? manake umenifurahisa sana kuniita jina hilo lol! nakupenda bure

Si unajua tena, lazima nikupe heshima yako. Tayari najua wewe ni mama Klein kwanini nisikuheshimu?..Umenifurahisha hapo kwenye kinywaji...mimi huwa nakunywa "Smoothy" ya matunda mchanganyiko,"Milk shake" na Maji.
Asante sana dear...!!
 
Kweli lakn haukuhusu wewe inawahusu mawaziri na makatibu wakuu na wakuu wamikoa na wilaya wakuurugenzi na makatbu tawala?
 
Serikali yafanya kufuru
JUMATATU, NOVEMBA 19, 2012 05:56 NA KHAMIS MKOTYA, DAR ES SALAAM
*Yapandisha mishahara ya vigogo ghafla
*Waziri Kombani adai imefuata taratibu
*Wengine waongezewa Sh milioni moja
SERIKALI imefanya marekebisho ya mishahara kwa watumishi wake kwa mwaka wa fedha 2012/2013, MTANZANIA imebaini. Sambamba na hilo, mishahara ya viongozi wa Serikali kwa mwaka huo wa fedha, nayo imefanyiwa marekebisho.

Marekebisho hayo ni kwa mujibu wa waraka wenye kumbukumbu namba S/AC 205/ 399/ 01/ 44, kutoka Ofisi ya Rais Ikulu (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), uliotolewa Julai 25, mwaka huu.

Waraka huo, umesambazwa kwa wakuu wote wa idara za Serikali, wakurugenzi wa majiji, manispaa, miji na wakurugenzi wa halmashauri zote za wilaya nchini.

Waraka huo, uliosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu (Utumishi), Hab Mkwizu, umehusisha pia marekebisho ya ngazi za mishahara kwa viongozi hao wa Serikali.

Kwa mujibu wa waraka huo, ngazi za mishahara zilizokuwa zinaanzia TGS I hadi TGS Q, zimebadilishwa na sasa zitasomeka LSS (E) 1 hadi LSS (E) 9.

Watumishi na viongozi wa Serikali walionufaika na marekebisho hayo, ni pamoja na makatibu wakuu wa wizara, manaibu wao pamoja na wakurugenzi wa idara zote za Serikali. Marekebisho hayo yameanza kutekelezwa Julai, 2012.

Hata hivyo, marekebisho hayo yamelalamikiwa na baadhi ya watumishi wa Serikali, wakidai kuwa hayana uwiyano unaoeleweka kati ya mishahara ya wamtumishi wa Serikali.

Marekebisho hayo yanaoneshwa katika kiambatanisho namba 1 cha waraka huo, ambapo watumishi na viongozi hao wameongezewa mshahara usiopungua 400,000.

Mfano mshahara wa mtumishi wa ngazi TGS P, umepanda kutoka Sh 3, 216, 000 hadi Sh 4, 500, 000 katika ngazi mpya ya LSS (E) 9, ongezeko ambalo ni zaidi ya Sh milioni moja.

Mmoja wa wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alikosoa marekebisho hayo na kusema kuwa, hayana uwiyano mzuri kati ya mshahara wa mtumishi na mtumishi mwingine.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani, amekiri kuwapo kwa marekebisho hayo ya mishahara kwa watumishi na viongozi wa Serikali.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu, Kombani alisema, marekebisho hayo ni ya kawaida na kwamba yanawagusa watumishi wote wa Serikali bila kubagua.

“Serikali ikifanya marekebisho ya mishahara, inafanya hivyo kwa watumishi wake wote. Hatuchagui nani aongezewe nani asiongezewe ni wote,” alisema.

Alisema vigezo vilivyotumika katika marekebisho hayo, ni pamoja na aina ya kazi, uzoefu na muda aliotumia mtumishi kukaa kazini.

“Unauliza kwanini watumishi wengine wamepewa nyongeza kubwa na wengine kidogo, ndugu yangu sifa zinatofautiana, mtumishi anayeanza kazi leo, hawezi kulipwa mshahara na mtumishi aliyepo kazini kwa miaka 20,” alisema.

Alipoulizwa ni sababu zipi zilizoifanya Serikali kurekebisha ngazi ya mshahara kutoka TGS na sasa kutumia ngazi mpya ya LSS, Waziri Kombani alisema. “Hayo ni masuala ya kitaalamu zaidi.”

Kombani alikiri kima cha chini cha mshahara ni kidogo na kueleza kuwa, Serikali ipo katika majadiliano.

“Kima cha chini kilipanda kutoka Sh 130, 000 hadi Sh 170, 000. Tunajua kima hiki hakitoshi lakini tupo katika majadiliano,” alisema.

Hapo kwenye red, ni kazi gani hiyo nikaisomee maana licha ya huo mshahara lazima kutakuwa na posho za kutosha
 
mkuu gazeti linatuuza, hii issue ilitokea tangia July, wao ndo wanaandika leo!!!!!

Habari yenyewe ni kama ilishatolewa siku nyingi halafu mwandishi kai retrieve na kuitoa upya. Maana nashangaa watu inaowa quote k.m waziri Kombani, hivi wame comment leo kwa issue ya iliyopitwa na wakati?!
 
Watumishi wa ngazi ya chini pumb..v zetu! Acha tukome, kwenye uchaguzi ndo huwa tuko mstari wa mbele kuchakachua kura! Tutakomii!
 
Habari yenyewe ni kama ilishatolewa siku nyingi halafu mwandishi kai retrieve na kuitoa upya. Maana nashangaa watu inaowa quote k.m waziri Kombani, hivi wame comment leo kwa issue ya iliyopitwa na wakati?!

RAIS WA TOGO AFUMANIWA,Habari kamili zinasema rais wa mchezo wa bao katika mtaa wa Adebayo nchini Togo, amefumaniwa akitembea kwa miguu wakati anamiliki bajaji.LENGO NI KUUZA GAZETI.
 
Si unajua tena, lazima nikupe heshima yako. Tayari najua wewe ni mama Klein kwanini nisikuheshimu?..Umenifurahisha hapo kwenye kinywaji...mimi huwa nakunywa "Smoothy" ya matunda mchanganyiko,"Milk shake" na Maji.
Asante sana dear...!!

basi pata glasi 2 za milk shake bili kwangu lol! asante sana kwa heshima ulonipa
 
Back
Top Bottom