Serikal yaongeza mishahara ghafla?

Serikal yaongeza mishahara ghafla?

mkuu hebu uwe siriazi bana, hizi ni tetesi ama???.....mbona utanifanya niende kukopa tena lol!

Umenichekesha wakati mwenzio nilikuwa na huzuni! Shosti usikope mpaka uione salary slip mpya! Lol!
 
Madaktari wameongezewa ngapi? au ndio liwalo na liwe?
 
Umenichekesha wakati mwenzio nilikuwa na huzuni! Shosti usikope mpaka uione salary slip mpya! Lol!

pole mwaya unahuzuni ya nini tena??
lakin bora nimekuchekesha umepata raha lol!
 
Wale wa TGS D -H wako katika kiwango gani? Maana wengi wenye degree waaanzia D ingawa nazo zinatofautiana kulingana na fani yako!!
 
jaman mwenye habar kamili anijuze,ni kwel serikal imeongeza mishahara ya watumishi ghafla?

ni ile ya july mkuu,hili gazeti sijui lilikuwa limelala wapi.namshangaa mwandishi habari ilitokea july,mishahara ikalipwa august pamoja na arrears eti leo ndio LIMEKURUPUKA NA HEADING HIYO,NYIE MTANZANIA MKO SERIOUS??????
Mmekosa habari kiasi hicho? si mje niwasimulie ndoto yangu muiandike???
come on!
 
Yani 170,000 kima cha chini cha mtu aishi nacho kwa mwezi wakati kuna watu ambao matumizi ya kawaida kwa siku ni 200,000 (kwa chakula na mambo madogo ya nyumbani) bado hujaweka entertaiment na mambo mengine!! Nikiwa na 100,000 mfukoni ni kama vile sina kitu!!! Nasema ukweli msinirushie mawe, nazitafuta kwa nguvu zangu halali na ajira!!! Najuwe wengine wanaweza kuwa wanatembelea milions kama change but mimi kwa kiwango hicho kahela ka mfukoni tu si mbaya ati!!! Ha ha ha!! Serikali kuweni makini, acheni kutesa hawa watumishi wa kima cha chini!! Kwa nini mjiongezee mamilion mnashindwa kufanya kima cha chini hata 500,000?
 
Hakunaga kitu kama hiki ikiwa mpaka leo sisi polisi hatujapokea mshahara wa mwezi Oktoba sasa watawezaje kuongeza mshahara ,Tunaomba serikali msitugombanishe na wenye nyumba wetu.
Hivi ule mpango wa kuwapatia makazi ili muondoke kuishi uswahilini umeishia wapi|?
 
Serikali hii ya CCM imejaa wahuni kila kona na ubababishaji kila idara
 
Yapandisha mishahara ya vigogo ghafla
*Waziri Kombani adai imefuata taratibu
*Wengine waongezewa Sh milioni moja
.........Kombani alikiri kima cha chini cha mshahara ni kidogo na kueleza kuwa, Serikali ipo katika majadiliano.

“Kima cha chini kilipanda kutoka Sh 130, 000 hadi Sh 170, 000. Tunajua kima hiki hakitoshi lakini tupo katika majadiliano,” alisema.

Watumishi wa kima cha chini vuteni subira, majadiliano yanaendelea vizuri na yatakamilika Agosti/Sept 2015 mtaongezewa tu!
 
That how a quick flow of money start,we need to be prepared coz mwinyi's theory may be possible.
 
mkuu kama ni kweli aisee nawapeni pole sana.
sasa kama serikali imeshindwa kuwalipa ni wazi kwamba haina hela kwa uwezo wangu mdogo wa kufikiri, na ikiwa kwamba CCM waliweza kufanya mkutano wa mamilioni kule Dodoma bila kujali kwamba kuna watumish ambao hawajalipwa mishahara basi CCM imekosea sana. Nafikiri kama iliweza kutafuta hela kwa wafadhili na popote pale ili kufanikisha ule mkutano basi wangeweza kutumia nguvu hizo hizo kutafuta hela za kulipa watumish wake kwakua CCM ndo serikali yenyewe...............

ccm haina jukumu la kulipa watumishi wa umma mishahara,kwa iyo swala la mkutano dodoma halina uhusiano na nyongeza za mishahara
 
There are currently 169 users browsing this thread. (25 members and 144 guests)

at this hour... ishu nyeti sana hii...
 
Hivi mnakaa kujadil huu ***** hamjui mshara ni issue ya ki bajeji ? nilini bunge limekaa kupisha bajeti ndogo hiyo story ya Mtanzania ni ya mwezi wa saba huko.
 
Hapa Tanzania,kazi ukubwa wa ng'ombe,Mshahara Mbuzi...kodi Tembo...mfanyakazi wa Tanzania,mtu mwenye mateso mengi sana,mshahara haukutani...kabla haujaingia umeisha....daaaahhh....
 
Back
Top Bottom