Serikal yaongeza mishahara ghafla?

Serikal yaongeza mishahara ghafla?

Hebu badili hicho kicha cha habar mbn hakiendan na ulichoandka?
 
Nyie polisi kwa nini mnailalamikia serikali?serikali si ni nyie wenyewe? Halafu kwa nini mnaua wananchi ovyo wanaoandamana kwa kutumia vitu vizito?

Hakunaga kitu kama hiki ikiwa mpaka leo sisi polisi hatujapokea mshahara wa mwezi Oktoba sasa watawezaje kuongeza mshahara ,Tunaomba serikali msitugombanishe na wenye nyumba wetu.
 
*Waziri Kombani adai imefuata taratibu
*Wengine waongezewa Sh milioni moja

SERIKALI imefanya marekebisho ya mishahara kwa watumishi wake kwa mwaka wa fedha 2012/2013, MTANZANIA imebaini. Sambamba na hilo, mishahara ya viongozi wa Serikali kwa mwaka huo wa fedha, nayo imefanyiwa marekebisho.

Marekebisho hayo ni kwa mujibu wa waraka wenye kumbukumbu namba S/AC 205/ 399/ 01/ 44, kutoka Ofisi ya Rais Ikulu (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), uliotolewa Julai 25, mwaka huu.

Waraka huo, umesambazwa kwa wakuu wote wa idara za Serikali, wakurugenzi wa majiji, manispaa, miji na wakurugenzi wa halmashauri zote za wilaya nchini.

Waraka huo, uliosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu (Utumishi), Hab Mkwizu, umehusisha pia marekebisho ya ngazi za mishahara kwa viongozi hao wa Serikali.

Kwa mujibu wa waraka huo, ngazi za mishahara zilizokuwa zinaanzia TGS I hadi TGS Q, zimebadilishwa na sasa zitasomeka LSS (E) 1 hadi LSS (E) 9.

Watumishi na viongozi wa Serikali walionufaika na marekebisho hayo, ni pamoja na makatibu wakuu wa wizara, manaibu wao pamoja na wakurugenzi wa idara zote za Serikali. Marekebisho hayo yameanza kutekelezwa Julai, 2012.

Hata hivyo, marekebisho hayo yamelalamikiwa na baadhi ya watumishi wa Serikali, wakidai kuwa hayana uwiyano unaoeleweka kati ya mishahara ya wamtumishi wa Serikali.

Marekebisho hayo yanaoneshwa katika kiambatanisho namba 1 cha waraka huo, ambapo watumishi na viongozi hao wameongezewa mshahara usiopungua 400,000.

Mfano mshahara wa mtumishi wa ngazi TGS P, umepanda kutoka Sh 3, 216, 000 hadi Sh 4, 500, 000 katika ngazi mpya ya LSS (E) 9, ongezeko ambalo ni zaidi ya Sh milioni moja.

Mmoja wa wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alikosoa marekebisho hayo na kusema kuwa, hayana uwiyano mzuri kati ya mshahara wa mtumishi na mtumishi mwingine.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani, amekiri kuwapo kwa marekebisho hayo ya mishahara kwa watumishi na viongozi wa Serikali.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu, Kombani alisema, marekebisho hayo ni ya kawaida na kwamba yanawagusa watumishi wote wa Serikali bila kubagua.

"Serikali ikifanya marekebisho ya mishahara, inafanya hivyo kwa watumishi wake wote. Hatuchagui nani aongezewe nani asiongezewe ni wote," alisema.

Alisema vigezo vilivyotumika katika marekebisho hayo, ni pamoja na aina ya kazi, uzoefu na muda aliotumia mtumishi kukaa kazini.

"Unauliza kwanini watumishi wengine wamepewa nyongeza kubwa na wengine kidogo, ndugu yangu sifa zinatofautiana, mtumishi anayeanza kazi leo, hawezi kulipwa mshahara na mtumishi aliyepo kazini kwa miaka 20," alisema.

Alipoulizwa ni sababu zipi zilizoifanya Serikali kurekebisha ngazi ya mshahara kutoka TGS na sasa kutumia ngazi mpya ya LSS, Waziri Kombani alisema. "Hayo ni masuala ya kitaalamu zaidi."

Kombani alikiri kima cha chini cha mshahara ni kidogo na kueleza kuwa, Serikali ipo katika majadiliano.

"Kima cha chini kilipanda kutoka Sh 130, 000 hadi Sh 170, 000. Tunajua kima hiki hakitoshi lakini tupo katika majadiliano," alisema.

Source:Mtanzania Jumatatu
 
mkuu hebu uwe siriazi bana, hizi ni tetesi ama???.....mbona utanifanya niende kukopa tena lol!
Mi nimesikia kwenye Magazeti ya leo lakini ni vigogo...huku chini kajamba nani wala hawajagusa huenda kuna ukweli na kama ni kweli wasubiri maandamano

mzima weye!! namakumiss
 
Toka nioneshwe jedwali la ongezeko la mishahara sijapokea huo mshahara mpya. Sijui wameongeza wa nini sasa.
 
jaman mwenye habar kamili anijuze,ni kwel serikal imeongeza mishahara ya watumishi ghafla?

Serikali yafanya kufuru
JUMATATU, NOVEMBA 19, 2012 05:56 NA KHAMIS MKOTYA, DAR ES SALAAM
*Yapandisha mishahara ya vigogo ghafla
*Waziri Kombani adai imefuata taratibu
*Wengine waongezewa Sh milioni moja
SERIKALI imefanya marekebisho ya mishahara kwa watumishi wake kwa mwaka wa fedha 2012/2013, MTANZANIA imebaini. Sambamba na hilo, mishahara ya viongozi wa Serikali kwa mwaka huo wa fedha, nayo imefanyiwa marekebisho.

Marekebisho hayo ni kwa mujibu wa waraka wenye kumbukumbu namba S/AC 205/ 399/ 01/ 44, kutoka Ofisi ya Rais Ikulu (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), uliotolewa Julai 25, mwaka huu.

Waraka huo, umesambazwa kwa wakuu wote wa idara za Serikali, wakurugenzi wa majiji, manispaa, miji na wakurugenzi wa halmashauri zote za wilaya nchini.

Waraka huo, uliosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu (Utumishi), Hab Mkwizu, umehusisha pia marekebisho ya ngazi za mishahara kwa viongozi hao wa Serikali.

Kwa mujibu wa waraka huo, ngazi za mishahara zilizokuwa zinaanzia TGS I hadi TGS Q, zimebadilishwa na sasa zitasomeka LSS (E) 1 hadi LSS (E) 9.

Watumishi na viongozi wa Serikali walionufaika na marekebisho hayo, ni pamoja na makatibu wakuu wa wizara, manaibu wao pamoja na wakurugenzi wa idara zote za Serikali. Marekebisho hayo yameanza kutekelezwa Julai, 2012.

Hata hivyo, marekebisho hayo yamelalamikiwa na baadhi ya watumishi wa Serikali, wakidai kuwa hayana uwiyano unaoeleweka kati ya mishahara ya wamtumishi wa Serikali.

Marekebisho hayo yanaoneshwa katika kiambatanisho namba 1 cha waraka huo, ambapo watumishi na viongozi hao wameongezewa mshahara usiopungua 400,000.

Mfano mshahara wa mtumishi wa ngazi TGS P, umepanda kutoka Sh 3, 216, 000 hadi Sh 4, 500, 000 katika ngazi mpya ya LSS (E) 9, ongezeko ambalo ni zaidi ya Sh milioni moja.

Mmoja wa wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alikosoa marekebisho hayo na kusema kuwa, hayana uwiyano mzuri kati ya mshahara wa mtumishi na mtumishi mwingine.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani, amekiri kuwapo kwa marekebisho hayo ya mishahara kwa watumishi na viongozi wa Serikali.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu, Kombani alisema, marekebisho hayo ni ya kawaida na kwamba yanawagusa watumishi wote wa Serikali bila kubagua.

“Serikali ikifanya marekebisho ya mishahara, inafanya hivyo kwa watumishi wake wote. Hatuchagui nani aongezewe nani asiongezewe ni wote,” alisema.

Alisema vigezo vilivyotumika katika marekebisho hayo, ni pamoja na aina ya kazi, uzoefu na muda aliotumia mtumishi kukaa kazini.

“Unauliza kwanini watumishi wengine wamepewa nyongeza kubwa na wengine kidogo, ndugu yangu sifa zinatofautiana, mtumishi anayeanza kazi leo, hawezi kulipwa mshahara na mtumishi aliyepo kazini kwa miaka 20,” alisema.

Alipoulizwa ni sababu zipi zilizoifanya Serikali kurekebisha ngazi ya mshahara kutoka TGS na sasa kutumia ngazi mpya ya LSS, Waziri Kombani alisema. “Hayo ni masuala ya kitaalamu zaidi.”

Kombani alikiri kima cha chini cha mshahara ni kidogo na kueleza kuwa, Serikali ipo katika majadiliano.

“Kima cha chini kilipanda kutoka Sh 130, 000 hadi Sh 170, 000. Tunajua kima hiki hakitoshi lakini tupo katika majadiliano,” alisema.
 
mleta mada hayuko serious anataka tu kuvuta watu wachangie maana anajua hili suala linagusa wengi

..Habari hizi ni za ukweli wana JF. Mie nimesikia leo redioni, but kwa sie WALALAHOI nyongeza ni ndogo sana sio kama WALALAHAI. Wao walalahai wamejiongezea mpk milioni moja
 
Hakunaga kitu kama hiki ikiwa mpaka leo sisi polisi hatujapokea mshahara wa mwezi Oktoba sasa watawezaje kuongeza mshahara ,Tunaomba serikali msitugombanishe na wenye nyumba wetu.

siyo askari polisi pekee ambao hawajapata mshahara wa mwezi oktoba.hata askari magereza wengine hawajapata mshahara mpaka sasa.hiki ni kitu ambacho hakijawahi kutokea tz yetu askari kutolipwa mshahara ni ajabu.serekali ya jk isipoangalia itajikuta inafanya kile kitu alicho kifanya Seseko alie kuwa raisi wa zaire kuwakabidhi askari silaha na kuwaruhusu askari wajilipe mshahara kwa kutumia hizo silaha.baada ya kushindwa kuwalipa askari mshahara.huu ni udhaifu mwingine kwa amiri jeshi mkuu.
 
Wapuuzi kweli, yaani laki moja na thelathini hadi na sabini huku kuna watu wameongezeana zaidi ya milioni??
 
mmmh aisee lakini mbona mishahara imepanda kwa wale ambao tayari wanamishahara mikubwa na marupurupu kibao??Nilidhani labda watapandisha kwa waalimu na polisi aisee...
 
Ningeliona shavu lako ningekuzaba

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mi nimesikia kwenye Magazeti ya leo lakini ni vigogo...huku chini kajamba nani wala hawajagusa huenda kuna ukweli na kama ni kweli wasubiri maandamano

mzima weye!! namakumiss

miss yu sana tu jiwe...................dompo jamani nazimisije lol!
 
Hakunaga kitu kama hiki ikiwa mpaka leo sisi polisi hatujapokea mshahara wa mwezi Oktoba sasa watawezaje kuongeza mshahara ,Tunaomba serikali msitugombanishe na wenye nyumba wetu.

si mnawapiga mabomu wenye nyumba acha wawafukuze tu
 
mmmh aisee lakini mbona mishahara imepanda kwa wale ambao tayari wanamishahara mikubwa na marupurupu kibao??Nilidhani labda watapandisha kwa waalimu na polisi aisee...

walimu walishaondolewa kwenye payrol orijino ya serikali
 
..Habari hizi ni za ukweli wana JF. Mie nimesikia leo redioni, but kwa sie WALALAHOI nyongeza ni ndogo sana sio kama WALALAHAI. Wao walalahai wamejiongezea mpk milioni moja

kwenye gazet la mtanzania la rostam limeandika
 
Anasema majadiliano yanaendelea kwa wale wakima cha chin??????ambao wanapata mia sabin
 
jaman mwenye habar kamili anijuze,ni kwel serikal imeongeza mishahara ya watumishi ghafla?

Gazeti linaeleza kuwa nyongeza ni kwa waraka wa mwezi Julai. sina hakika lakini nahisi si ntongeza mpya ila ni kitu kilishafanyika ila gazeti limeandikwa habari iliyopitwa na wakati. Ni mtazamo wangu.
 
Back
Top Bottom