Serengeti yashinda Tuzo Hifadhi Bora Afrika kwa mara ya tano mfululizo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Hifadhi Bora ya Taifa Barani Afrika 2023, imeshinda tuzo hii kwa mara ya tano mfululizo, mwaka wa 2019, 2020, 2021, 2022, na sasa 2023.

=================

c5456b69-0eb8-433d-9337-1f662b1ab9a9.jpeg
Hifadhi ya Taifa Serengeti imeibuka kidedea kwa kuwa mshindi wa kinyang’anyiro cha Tuzo ya Hifadhi bora barani Afrika kwa mwaka 2023(Africa’s Leading National Park 2023) ikiwa ni mara ya tano mfululizo kushinda Tuzo hii baada ya kuwagaragaza washindani wa tuzo hii kama Central Kalahari Game Reserve- Botwswana, Etosha National Park -Namibia, Kidepo Valley National Park -Uganda, Kruger National Park -South Africa, mapoja na Masai Mara National Reserve - Kenya

Tuzo hiyo imetolewa na ‘World Travel Awards’ usiku wa tarehe 15 Oktoba, 2023 katika hotel ya _Atlantis The Royal Dubai _ katika nchi za Falme za Kiarabu na kupokelewa na Mkuu wa Kanda ya Magharibi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Izumbe Msindai, kwa niaba ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
3144634b-12f6-4a9c-8a94-2d32e0fc6654.jpeg
 
Welldone, sasa tuje kwenye numbers, watalii wangapi wanatembelea serengeti national park?,je ni fedha kiasi gani kinakusanywa kwenye national park hii?,je mapato ya serengeti national park ni makubwa kuliko ya kruger national park?,je watalii wangapi wa ndani wanatembelea serengeti national park ukilinganisha na kruger national park?,end of the day kinachohesabika ni pesa iliyokusanywa na sio awards
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom