Tujikumbushe vikwazo hadi Tuzo ya Mwandishi Bora Afrika

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Naomba leo niwarudishe nyuma kidogo tulikotoka hadi leo nimepata Tuzo ya Mwandishi Bora wa Vitabu Afrika.

Nawakumbusha tu kwamba December 2017, kitabu cha Ujasusi kikiwa na mwaka mmoja hivi tangu kichapishwe, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dkt. Athumani S. Ponera (Akiwa ni Mhadhiri wa Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dodoma) alinunua kitabu na kukisoma, baada ya Kusoma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi alitoa mapendekezo/maoni yake kwamba Mwandishi wa Kitabu cha Ujasusi Bwana Yericko Nyerere anastahili kutunukiwa shahada mbili za "heshima" za udaktari.

Daktari Ponera katika maoni ama mapendekezo yake huru yanayosikika katika video hii, alisema,

"Yericko Nyerere kupitia kitabu hiki unastahili kupata PhD mbili, anafafanua zaidi kwakusema, PhD ni uzamivu wa mtu ktk Eneo/uga fulani. Mtu akisoma andiko lako anapata maeneo mawili au matatu yaliyofanyiwa kazi kwa kina. Kwa maoni yangu, Nyuga hizo ni pamoja na:

"1. Usalama, 2. Histo-tamaduni (maelezo ya kihistoria, matukio na utamaduni kuhusu jamii/maeneo mbalimbali), 3. (utamaduni wa)Siasa za maeneo mbalimbali. Any of the above fields zimeelezwa Kwa kina, na zinaweza kumegwa na kujaziwa kidogo kisha mtu anapata PhD....hongera sana Yericko Nyerere".

Mwisho wa kunukuu.

Baada ya maoni hayo, kwasababu ya siasa chafu za nchi yetu, alishughulikiwa kisawasawa, alinyanyaswa sana akitakiwa kujieleza kwanini ametoa maoni hayo kwa mtu ambae ni mpinzani nchini, baadae aliondolewa pale chuoni akapelekwa chuo cha Mwalimu Nyerere, kisha akapelekwa Zanzibar ambako aliendelea na utumishi wake kwa uaminifu mkubwa.

Miaka 6 baadae yaani 2023, Yericko Nyerere ametukiwa tuzo ya Mwandishi Bora wa Vitabu Barani Afrika. Sijui tunajifunza nini? Pengine wale maprofesa pale UDOM na wale viongozi wa kiserikali waliomshughulikia Dr. Ponera wanaweza kuwa na maoni tofauti leo wakisikia kuwa yule mtu waliyemchukia ilipopendekezwa apewe tuzo ya heshima ya PhD za Dar, Sasa amepewa tuzo ya Afrika ya uandishi Bora wa Vitabu.

Nakufahamisha incase umesahau au ulikuwa hujui, Mshindi wa Tuzo ya Mwandishi Bora wa Vitabu Barani Afrika ni YERICKO YOHANESY NYERERE kutoka TANZANIA.

Sifa na heshima ni za Watanzania!

Idumu Mizimu!

Na Yericko Nyerere

IMG_20231125_081540_695.jpg

 
Elezewa na wengine, usijielezee!
Acha wivu,huku nchini,mlileta ghiliba za kisiasa,lakini Africa nzima ikamtambua kua ni bora katika uandishi wa vitabu,unataka kusema alijielezea huko kote?
Acha roho mbaya,kuwa appreciative mwenzako anapofanya kitu kizuri.
Kaelezea vema kuhusu mambo ya siasa nchini,yanavyozuia baadhi ya michango ya watu wenye vipaji na akili za hali ya juu,kwa kufanyiwa mizengwe na kutopewa sifa stahki,hatakama michango yao ina manufaa kwa umma na taifa kwaujumla,huyo Dr.Ponera katolewa kama mfano wa watu hao,na Yericko Nyerere kama muhanga pia wa hizi siasa chafu.
Yericko angekua ni mtu wa mlengo wa chama cha CCM au ACT,angepata pongezi toka kwa mawaziri mbalimbali pamoja na hata Rais pia,na hata humu jukwaani ungeona watu kama akina@Paschal Mayalla,wakimpongeza,kwani ushindi wa hiyo tuzo ni ushindi wa Taifa nax ushindi wa huyu ndugu ni ushindi wa Tanzania,ndiyo maana unaona hata katika baadhi ya picha kabeba bendera ya Tanzania na siyo ya CHADEMA wala CCM kuwa kwao kimya ni kwasababu zilezile za kisiasa.
 
Karibu ndugu 0715865544
Siwezi kununua tena mkitabu wako,una mambo ya kipuuzi wewe na roho ya kishetani. Wale watumishi wa Geita wamekukosea nini mpaka umeenda kuwachoma kwa mamlaka? Dripu ya Tsh 950 bei ya jumla ndio ikutoe utu? Hao watumishi wanatumia muda mwingi makazini kuliko majumbani kwao,kuna ubaya gani kupata moment ya kufurahia kidogo? Utumishi ni utumwa kwako? Mnaacha kupigia kelele mambo ya maana mnahangaika na watu wanaofurahia siku za kuzaliwa kweli? Wamesimamishwa kazi,umepata nini sasa? Umefaidika na nini? Roho yako mbaya imefurahi?
 
  • Thanks
Reactions: EEX
Back
Top Bottom