Serengeti: Ujenzi Holela Hifadhini

Mfikirishi

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
7,492
8,537
Ulishawahi kusikia ujenzi holela?

Basi tazama hiyo picha hapo utajifunza kitu. Huwezi amini kuwa hayo ni majengo ya mojawapo ya hoteli za kitalii zinazoendelea kuibuka kama uyoga ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti!
(Ninazo picha nyingi sana, nitaambatanisha nyingine very soon!).

Hivi NEMC mpo kweli? SENAPA mpo?? TAWIRI mpo? TAWA? WIZARA/WAZIRI mpo?
Mbona mnawapa ma-tour guides kazi kubwa ku-cover madudu yenu?
Hivi siku hizi GMPs zinaruhusu "urban sprawls" hifadhini?

Ukiacha hili tatizo la "out-of-place permanent structures causing eye-sore and visual pollutions", bado kuna lile tatizo endelevu la ugawaji holela wa kambi za kitalii maeneo ambako hata wanyama akina nyumbu, twiga, chui, simba n.k wanashangaa kinachoendelea kwenye makazi yao!

Nimejaribu kufanya survey kidogo kwa kuwauliza wageni (watalii) wenye uelewa; wengi wanadai "Huu sasa siyo utalii - This isn't tourism"!

Na to be honest wanajuta sana kuja kutembelea hifadhi hizi! Na tena wengine wanaenda mbali kutulaumu sisi wananchi kukosa uzalendo kusimamia mambo ya msingi! Jamani wenye mamlaka, ingilieni kati kuokoa hifadhi zetu kwa maslahi mapana ya sasa na ya vizazi vijavyo!!

Hivi ni kwa nini tukiuke misingi na tuanze "kugawa milima" kwa ajili ya ujenzi holela wa hoteli za kitalii?
Ni kwa nini tuwaachie wenye fedha zao dhamana ya kufanya maamuzi ya wapi wajenge hoteli au kambi zao? Hivi kama wanapesa kujenga mahekalu kama hayo ni kwa nini wasiyajenge nje ya hifadhi?

Bado nina imani kuwa chochote kinaweza kufanyika kuzuia sintofahamu hizi. Hifadhi ni makazi ya wanyamapori na si vinginevyo.

Msiziharibu kwa tamaa ya vipande vya fedha!

IMG-20200217-WA0001.jpg
 
Hili ni tatizo kubwa kabisa. Lakini anaweza kujitokeza mpumbavu mmoja akakuambia wewe siyo mzalendo.

Atakuambia hizo picha na malalamiko ulitakiwa uyapeleke sehemu zinazohusika kwani kusemea hapa unahujumu uchumi wa nchi.

Mtu unabaki kushangaa na kujiuliza: Mbona watalii wakienda huko wanakutana na haya mapungufu live?

Kwani hawajui kuwa wanaporudi kwao huwa wanaambiana hali ya sehemu wanazotalii?
 
Back
Top Bottom