Sera ya kodi ya mapato ya Tanzania inaemaje?

Exav

Member
May 6, 2010
64
95
Habari ya leo wanaJF? Naomba mwenye kufahamu mfumo au sera ya kodi ya nchi yetu (Tanzania) inasemaje kuhusu ukataji kodi katika mazingira yafuatayo:

Kwa mfano; mtu aliyeajiriwa (serikalini au kwenye NGO n.k.) na anapata mshahara (gross) labda sh. 300,000 (laki tatu) kwa mwezi. Vilevile mwajiri wake anampatia housing allowance labda sh. 100,000 (laki moja) kila mwezi na hii hela haitoki pamoja na mshahara.

Pia, hiyo gross salary inakatwa 10% kwa ajili ya PPF,NSSF n.k. kisha sh. 270,000 inayobaki inakatwa kodi ile ya pay as you earn (PAYE) kisha kiasi kinachobaki ndio analipwa mtu huyo, labda sh 251,100. Sasa hii allowance ya laki moja ikitoka, inatakiwa ikatwe kodi kwa kutumia utaratibu upi? Na je, kuna kiasi chochote kinatakiwa kiongezwe kwa ajili ya kuchangia PPF, NSSF n.k. kutokana na hii allowance?

Nawasilisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom