SEO writing, kazi inayolipa sana mtandaoni

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,045
Ushawahi kujiuliza kwanini ukigoogle kitu inakuwaje kuna tovuti zinatokea juu na nyingine chini. Yani mfano unaweza kugoogle coronavirus, ikakwambia kuna majibu billion tatu sasa inakuaje kuna tovuti zinatokea page ya kwanza na nyingine page za huko mbele?

Ni wazi kuwa watu wengi husoma majibu yanayotokea ukurasa wa kwanza; ni mara chache ukaenda kusoma kilichopo page ya pili ya google results. (ranking)

Sasa inakuwaje page inatokea kwenye ukurasa wa kwanza wa majibu ya Google mtu akifanya searching ya topic flani? Hapo ndipo SEO technics zinahusika.

Siko hapa kuelezea uandishi wa SEO wala kumfundisha mtu, ila kwa kifupi ile page itokee ukurasa wa kwanza inahusisha vitu vingi ikiwemo:

- Keywords
- Written to be read by humans
- Internal linking
- External linking
- Content iwe inajibu maswali ya mtafutaji
- Optimizing your keywords

Na mengine mengi.

Hii imekuwa kitu kikubwa na kila mzalishaji wa content anatamani sana zisomwe maana ndiyo biashara yenyewe, na angependa tovuti yake iwe inatokea page ya kwanza. Hivyo imepelekea kuwa ni ajira inayolipa sana katika ulimwengu wa freelancing ambapo mtu anaweza lipwa kuanzia dollar 70 - 800 kwa kuandika content inayorange kuanzia maneno 500 mpaka 3000.

Halafu ni kwamba demand yake ni kubwa sana yani katika ulimwengu wa content writting SEO experts wanahitajika sana kwasababu iwe ni kwa muuzaji wa Ebay, Amazon, iwe ni blog, au website kote inahusika.

Kama kuna freelancers ambao wamejikita kwenye content writing jaribuni sana kujifunza hiki kitu, pia wale bloggers nao wakitaka tengeneza mkwanja zaidi hii inawahusu sana.
 
Kaka hii kitu naisikia sana hvy napenda san kijua namna ya kuwa freelancing, na naanzaje kupost content writting
 
SEO imekuwa ni changamoto sna kwa wengi ata ukimwambia mtu pitia atakwambia anaona giza tu.
Mbaya zaid kwa watu ambao hawajasoma either computer science, computer eng, IT, software eng and like wanapata sana shida kuisoma hii coz vitabu ving vipo technical sana kuna mahali ibinabd uanze kucheza na CODE kidogo.
Lakin weng ni uvivu wa kusoma ndio inachangia SEO ni field ambayo haiwez kuisha uhitaj wake kwa sasa as long as search engines znaexist na kila inapoitwa leo ndo inazd kuwa hot cake siku za nyuma ilikuwa ukiwa tu na backlinks haijalish umezitoa wap ulikuwa unapandshwa juu now hali imechange.
Na mwaka huu Google wameongeza kilio tena baada ya ku-update system yake, website nying zmejikuta zmepoteza views weng sana.
Naona Bongo ndio inaanza anza kidog kidogo coz website zinazd kuwa nying but kwabwenzetu SEO expert analipwa vizur mno na kwa makampun makubwa unakuta kuna jopo la SEO experts .
 
Nahitaji wataalamu wanifanyie kazi hii! Sina pesa nzuri sana ya kuwalipa ila nitajitahidi kuwalipa kwa uwezo wangu.
 
Ni kweli CEO iko juu kwa sasa kwani hata matangazo ya uhitajio wa hao wataalam ni mengi sanaa

Sema sisi wa bongo ni wa vivu wa ku be up dated.

Any way mwenye mwanga utupe pakuanzia bila kujali gharamaa
 
Watanzania hata vitu vidogo kama hivi hatuwezi kabisa,yaani mtu kamaliza degree ya education anashindwa kujifunza fani ndogo tu kama hii
 
Ikichangiwa na English ndo maana tunapita kama hatuzioni
Hivi inaweza kukuchukua zaidi ya miezi 6 kujifunza kingereza kizuri.
Hivi unakuwa na nia na hizo ajira kweli.
Yani watanzania waweze ku master programming, electronics, physics nk mshindwe ku master kingereza. Kinaugumu gani ?
Wekeni jitihada acheni kupenda mteremko.
There is no free meal on earth.
Soma sana vitabu vya kingereza na summarize kila chapter. Sikiliza sana video za kingereza,movies, soma articles.
Ongea na kila mtu unaemjua kuwa anaweza kuelewa kingereza.
Fikiria kila jambo kwa kingereza.
Ongea kila siku peke yako, jirekodi, jisikilize jirekebishe.
Andika kila kitu chako kwa kingereza kwa siku nzima.
Jitolee kufundisha kingereza watito na wenye uhitaji.
Ukifanya hayo miezi sita na usiweze basi acha nenda kalime.
 
Watanzania hata vitu vidogo kama hivi hatuwezi kabisa,yaani mtu kamaliza degree ya education anashindwa kujifunza fani ndogo tu kama hii
Imagine hata Mwalimu wa English naye analalamika mshahara hautoshi!

Computer programmer hana hata 100 mbovu 🤣🤣🤣
 
Hivi inaweza kukuchukua zaidi ya miezi 6 kujifunza kingereza kizuri.
Hivi unakuwa na nia na hizo ajira kweli.
Yani watanzania waweze ku master programming, electronics, physics nk mshindwe ku master kingereza. Kinaugumu gani ?
Wekeni jitihada acheni kupenda mteremko.
There is no free meal on earth.
Soma sana vitabu vya kingereza na summarize kila chapter. Sikiliza sana video za kingereza,movies, soma articles.
Ongea na kila mtu unaemjua kuwa anaweza kuelewa kingereza.
Fikiria kila jambo kwa kingereza.
Ongea kila siku peke yako, jirekodi, jisikilize jirekebishe.
Andika kila kitu chako kwa kingereza kwa siku nzima.
Jitolee kufundisha kingereza watito na wenye uhitaji.
Ukifanya hayo miezi sita na usiweze basi acha nenda kalime.
I like this..
 
Back
Top Bottom