Sensa ya watu 2012 maandalizi yako wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sensa ya watu 2012 maandalizi yako wapi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Umsolopogaas, Feb 15, 2011.

 1. U

  Umsolopogaas Member

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Jul 18, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mbona watu wangu wanasahau sensa ya watanzania 2012? Nyie mlioko Takwimu, Mipango, Ikulu, na wadau wengine, mbona hatusikii lolote kuhusu sensa? Sensa ya mwisho ilifanyika 2002. Actually ilitakiwa kufanyika 1998 lakini wakazembea. kwa hiyo ili kwenda sawa sensa iliyofuata ilitakiwa ifanyike 2008 lakini mh! Mlizembea tena! Sasa angalao 2012 yaani miaka 10 tangu 2002.

  Hivi kweli huko serikalini koote hakuna mtu hata mmoja mwenye ujasiri wa kumkumbusha bosi wake kuwa kuna kitu muhimu kinasahaulika?

  Au mnatarajia kuchakachua tu kama mnavyochakachua mambo mengi, kwani ni nani atalalamika kuwa hakuhesabiwa?
   
 2. C

  Cayla Member

  #2
  Aug 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hi ndg zangun wanajamii forum, tujiandae kuhesabiwa na tuwape ushirikiano makaran wa sensa. Usikubal kutohesabiwa. Sensa kwa maendeleo ya Taifa. Sensa oyeeee....asanten sana.
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Karibu sana JF.
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Aug 25, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Wewe umejiandaa kuhesabiwa?
   
 5. a

  axel fowly Senior Member

  #5
  Aug 25, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umekuja na mbwembwe..wenzako wanasemaga hodi!
   
 6. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Poa na karibu,wewe umejiandaa?
   
 7. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mbona mkali? Bado mgeri yeye
   
 8. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,860
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  mgen????? mbna sijaona kamba mguuni?????
   
 9. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Karibu jamvini.
   
 10. kisugujira

  kisugujira JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 769
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  WanaJF tafadhalini niambieni biashara niliyoiona jana inayoendana na hali halisi iliyopo wakati huu wa sensa ni ya nani? Juzi usiku kwenye saa nne tulikuwa uwanja wa ndege wa kimatafa wa JK kule kwenye ofisi za DHL wengine hupaita DAHACO tukisubiri kupokea jeneza lenye mwili wa ndugu yetu aliyefia ughaibuni.

  Tulipokuwa pale tuliona mifuko mingi na mikubwa ya sandarusi mingine ikiwa imefumuka na kuonyesha kilichokuwemo ndani yake ambavyo ni vizibao(vikoti)kama wanavyovyaa waendesha bodaboda ikipakiwa ndani ya gari.Kilichonishitua zaidi ni kuwaona makarani wa sensa wakiwa wamevaa vizibao(vikoti) hivyo kwa wingi tu kama vile tulivyoviona kule Airport!
   
 11. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  SALAMU
  Binafsi nashukuru kwamba sensa sasa inafanyika/imefanyika na kwamba
  TAKWIMU za kuotea kwenye mipango ya serikali tunaweza kupata jibu pamoja na mambo mengine mengi.
  Lakini kila nilitokuwa nikisoma HABARI kuhusu sensa niliona makarani kama picha inavyoonyesha nikajiuliza maswali mengi
  Kulikuwa na UMUHIMU wote kwa hao makarani kuvaa REFLECTORS {karani ayelikwenda IKULU kavaa, kwa makamu wa raisi pia, source picha kwenye magatezi}
  Kwa jinsi ninavyoelewa REFLECTORS utumika ili watu wakuone kirahisi hasa kwenye maeneo yenye magari na machine zinazotembea, zinaweza kutumika kwenye matukio mbalimbali kama mpira au mikusanyiko mikubwa kwa ajili ya kuonyesha watoa HUDUMA.

  Lakini kwenye zoezi kama la SENSA karani anakwenda kwa wahusika kwenye makazi yao au kwenye biashara zao, zena akiwa wameongozana na wenyeji wa eneo husika (mjumbe na mwenyekiti wa kijiji), sasa hivi reflector wanavaa za nini?
  ni nani huyo aliyefanya LOBBYING office za TAKWIMU ili aweza kutumbua pesa yetu kwa kupitia huu mradi wake wa reflector?
  Tunafanya sensa ya mabilion kwa matumizi yasiyo na umuhimu kama haya.

  Mwisho
  I STAND TO BE CORRECTED
  [​IMG]

  [​IMG]

  Nimejaribu kuweka PICHA za mazingira TOFAUTI ili kuonyesha picha halisi
   
 12. Ben Nyangarya

  Ben Nyangarya Senior Member

  #12
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 152
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Umetuamsha wengi! hizi reflector hadi ikulu, kweli ni za nini? watu wengi hatukujiuliza hili!
  Makarani hawa wanavyo vitambulisho, wanafuatana na viongozi wa eneo husika (hawa hata posho hawakufikiriwa) sasa hizi reflector za nini?
  Nakumbuka tulikuwa tukizivaa migodini tuendapo site, au maeneo ya wazi, hususani yenye vyombo vya moto, ili tuweze kuoneka kirahisi kuepusha uwezekano wa ajali. Tulikuwa tukizivua pindi tuingiapo maofisini na kuzitundika kwenye viti, ofisini hazina kazi!
  Sasa hizi, ndani ya nyumba za watu, ndani ya ikulu, zinasaidia nini? Maana viongozi wa eneo hilo wanajulikana, karani ndiye mgeni, kitambulisho hakimtoshi?
  Mmh! wajanja wameshauza, pesa tayari kibindoni!
   
 13. C

  CHOMA Senior Member

  #13
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hali ya sensa ya watu na makazi inavyoendelea upo uwezekano wa hawa watu wanaogoma kuhesabiwa wakafika mahali wakasalimu amri kwa usaliti.Wanaweza wakajidai kushiriki sensa kwa kutoa majibu ambayo sio sahihi ili wavuruge zoezi hilo kwa mlango wa nyuma.
   
 14. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Wanakera na maswali yao hivyo wanaweza kuwa wanapewa majibu kulingana na wanavyouliza ...unaona mtu ni mwanaume still unamuuliza we ni Jinsia Gani?
   
 15. Kimbojo

  Kimbojo JF-Expert Member

  #15
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2009
  Messages: 387
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Watanzania wenzangu tujiulize kwa namna sensa inavyofanyika, vifaa havikutosha mfano t-shits, zile karatasi za sensa na tulikuwa tunasikia vyombo vya habari kuwa kuna maeneo makarani hawakulipwa kwa wakati. Hivi kweli kulikuwa na maandalizi?

  Imefikia hatua wasimamizi wa sensa wanatoa photocopy zile karatasi za sensa eti kwa sababu original zimekwisha, hivi haya ni maandalizi. Nilikuwa Mpwapwa Dodoma Makarani wanafanya kazi hiyo bila kuwa na sare maalum zilizokuwa zikisemwa kwenye vyombo vya habari, nimepita stationary moja watu wako bize kutoa photocopy zile karatasi za takwimu , je kwenye komputa zitasomwa kweli kwa sababu ni black and white sio coloured. Wakuu wamekuwa wakihangaika na kundi dogo ambalo limekataa sensa wakaacha kusimamia usambazaji wa vifaa kwa wakti. Je takwimu hizi zitakazo patikana zitatoa picha halisi ya watania kwaujumla.

  Jambo lingine ni uelewa wa makarani unatia shaka. mfano anakuuliza umri wa mtoto, ukamtajia miaka 4. afu swali lnalofuata ankuuliza je amezaa?. hii si ni ukosefu wa uelewa na upotezaji wa muda jamani!! Mtoto wa miaka anuwezo wa kuzaa?. Haya yote ni maandalizi dhaifu labda tungerusha kama ilivyitokea 1998.
   
 16. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hii ni nchi ya bongo. Huelewi nini?
   
 17. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Wandugu,
  Nimesoma huko kwenye blog la 'ZANZIBAR NI KWETU' kuwa Kata 256 huko Kilwa hazikutaka kuhesabiwa. Hii ni kweli? Mwenye habari za kuaminika atujulishe. Kama ni kweli basi hii ni hatari kubwa. Nchi yetu inaelekea kubaya jamani. Hili tatizo la udini ni lazima lishughulikiwe kabla halijakuwa kubwa sana na likatugawa zaidi na kutuangamiza.
  /Ngida1
   
 18. d

  dotto JF-Expert Member

  #18
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Bhandugu mimi natatizwa na huu utaratibu wa sensa kuwa siku saba. Hii isijekuwa na U-EPA mwingine. Kwa nini badala ya karani mmoja wa sensa anayelipwa siku saba mfululizo wasiajiriwe makarani sita Extra na zoezi likawa la siku moja au mbili tu?? Kuna nini zaidi nyuma ya hii kitu sensa na malipo??
   
 19. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #19
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Fatama Mwasa (Kamishna wa Sensa) akihojiwa na mwandishi wa habari wa TBC kuhusiana na kuchelewa kwa vifaa vya Sensa asema- ........''vifaa vyote vya sensa vimetoka nje ya nchi, utashangaa ndugu mwandishi kuwa hadi, CHAKI, KALAMU, ..........N.K vyote vimetoka nje ya nchi, China na Kwengineko''.
  Hoja yangu- iwapo Serikali inaagiza hadi CHAKI kutoka china kimebaki nini tena kuagizwa nje, labda ugoro!
  Sijapat kuona nchi ina vituko kama hii!
   
 20. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #20
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Duuuuh......wakati kuna wajasiriamali wa ndani wanatengeneza chaki .......daaah hii inji hii!
   
Loading...