Sensa ya mwaka 2012 kugharimu Sh113.7 bilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sensa ya mwaka 2012 kugharimu Sh113.7 bilioni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Jun 11, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Na Habel Chidawali

  JUMLA ya Sh 113.7 bilioni zinatarajiwa kutumika katika kazi ya sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwezi Agosti mwaka 2012, Bunge liliambiwa jana.

  Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Omar Mzee alilimbia bunge mjini hapa kuwa fedha hizo zitatumika kwa kazi yote ya sensa tangu maandalizi, ukusanyaji taarifa, na kutangaza matokeo kwa umma na watumiaji wengine.

  Kwa mujibu wa Waziri Mzee kiasi hicho cha fedha kitatumika kwa kipindi cha miaka saba kuanzia mwaka wa fedha 2008/2009 hadi 2014/2012.

  Waziri Mzee alisema kuwa shughuli katika mchakato huo ni ndefu na kila shughuli inahitaji mafunzo maalumu ili kuwezesha kazi hiyo kufanyika kwa ufanisi mkubwa.

  Mzee ambaye alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Ilala (CCM) Mussa Azan Zungu aliyetaka kujua ni shilingi ngapi zitatumika katika zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika mwaka 2012.

  Katika swali lake la msingi Zungu aliitaka serikali kuwatumia wenyeviti wa mitaa, vitongoji na vijiji kwa kuwa wao ndio wanaowajua wananchi kwa ukaribu zaidi na akaomba posho za watu hao zifahamike mapema ni shilingi ngapi watalipwa katika kazi hiyo.

  Mbunge huyo aliitaka serikali kuachana na mpango wa kuwatumia maafisa wa idara zake mbalimbali katika sensa hiyo ili kuepusha gharama za ununuzi wa magari yatakayotumika.

  Naibu Waziri alisema sensa ya watu na makazi ni zoezi shirikishi ambalo linashirikisha watendaji kutoka wizara na idara mbalimbali za serikali hivyo, akasema wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji nao wana majukumu yao na kwamba wao watashirikishwa kwenye mafunzo hayo ili waweze kutoa mchango wao kikamilifu.

  Kuhusu ni shilingi ngapi watalipwa katika zoezi hilo, Waziri Mzee alisema wakati ukifika hayo yatajulikana, lakini cha msingi wanatakiwa kujua kuwa na wao ni miongoni mwa watu muhimu katika kazi hiyo.

  Akizungumzia suala zima la kuazima magari ya taasisi mbalimbali ili yatumike ka ajili ya shughuli hiyo, Mzee alisema utakapofika wakati wa sensa serikali itafanya hivyo kwani utaratibu huo ulitumika hata katika sensa za mwaka 1967, 1978, 1988 na mwaka 2002.


  Source: Mwananchi
   
 2. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2009
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Tunaokaa nje ya Tanzania tutahesabiwa vipi???
   
 3. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,168
  Likes Received: 1,103
  Trophy Points: 280
  Waziri mkuu aliyasema haya wakati wa chakula cha mchana

  shillingi 141 bilion ni Kodi za wanannchi na wahisani;
   
 4. MZIMU

  MZIMU JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 4,080
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Hapa lazima watu wawajibike kwa kupoteza Mabilioni ya fedha na zoezi kudoda, kisa eti kuwakomoa waislamu wasijulikane wako wangapi. HAPA LAZIMA WATU WAWAJIBIKE. YOU WILL SEE.
   
Loading...