Maishamapya
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 1,279
- 375
hoja ya utanganyika, uzanzibari na utanzania tunaweza iweka kapuni for some time, kwani inapoteza dira na malengo ya mtanzania wa chini kabisa ambaye mahitaji yake muhimu ni chakula, mavazi, elimu, mahala pa kulala n.k. matatizo ni mengi sana tz yetu hii, hatuwezi fanya kila kitu ni priority, nadhani tungekomaa na mambo machache then mengine yatakuja baadaye, hapa ufisadi, hapa katiba mpya, hapa kilimo kwanza hakitekelezeki, hapa elimu duni, hapa uongozi mbaya, hapa kila kila kitu. yani ambacho si kizuri ndio kipo hapa. muda umefika wananchi tuamue priority ni nini kwetu na tuanze mapigano hadi kieleweke..
Hoja yako hapo kwenye nyekundu kwa kifupi ni RASILIMALI. Huwezi ukazungumzia rasilimali kama katiba haijakaa vizuri na katiba ina historia yake. Na mojawapo ya historia ya Katiba ya Tanzania ni suala la muungano ambalo halijakaa vizuri. Juzi juzi jamaa wamenusa mafuta huko Zenj wakasema hilo litolewe kwenye mambo ya muungano maana rasilimali hiyo ya mafuta itawafaidia wazenj tu. Mimi naamini matazizo ya watanzania siyo hayo uliyoyaorodhesha hapo juu pekee. Ni pamoja na misingi ya utawala ambayo ni ya kikatiba ambayo inawafanya watawala wetu wawe miungu watu wakijigawia mali zetu wapendavyo nasi tukiendelea kukosa hayo mambo muhimu uliyoyaorodhesha.