Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 301
"Waziri amesema moja kati ya mambo yaliyosababisha mabadiliko ya Katiba, ni mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar. Mabadiliko yale yameifanya Zanzibar kuwa nchi kamili. Na sisi tudai Serikali ya Tanganyika. Mwambieni Rais (Jakaya) Kikwete hivyo," alisema Sendeka
Mwanzo wa G55 nyingine?
MBUNGE wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, wamezozana hadharani wakipishana maneno kuhusu Muswada wa Mabadiliko ya Katiba. Mzozo huo ulizuka juzi kwenye mkutano wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (Alat) uliofanyika Kunduchi, Dar es Salaam juu ya mada ya Mabadiliko ya Katiba.
Baada ya Masaju kumaliza kuelezea madhumuni ya muswada huo, Sendeka alisimama na kuhoji kuhusu kauli iliyotolewa awali kwenye mkutano huo na Waziri Kombani kuwa, moja ya sababu za kuandikwa kwa Katiba mpya ni mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar iliyounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Sendeka alisema mabadiliko hayo yameifanya Zanzibar kuwa nchi kamili, hivyo ni muhimu sasa kwa Watanganyika nao wadai serikali yao. "Waziri amesema moja kati ya mambo yaliyosababisha mabadiliko ya Katiba, ni mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar. Mabadiliko yale yameifanya Zanzibar kuwa nchi kamili. Na sisi tudai Serikali ya Tanganyika. Mwambieni Rais (Jakaya) Kikwete hivyo," alisema Sendeka.
Hata hivyo, wakati wa kujibu maswali, Masaju alisema Zanzibar siyo nchi kwa maana ya dola, bali ni kwa maana ya mipaka.
"Siyo kweli kwamba Zanzibar ni nchi kwa maana ya dola, bali ni nchi kutokana na mipaka yake," alisema Masaju kwa hasira huku akinukuu baadhi ya vifungu vya Katiba ya Zanzibar na kuongeza:"Someni Katiba ya Zanzibar na hati za muungano."
Baada ya Masaju kukaa, Sendeka alisimama tena na kusema: "Sawa, yaani unatujibu kwa hasira hivyo? Katiba ya Zanzibar imetoa madaraka makubwa. Zamani kwa kesi za Mahakama ya Rufaa walikuwa wakija huku (Tanzania Bara), lakini siku hizi mahakama yao ina mamlaka ya mwisho. Wewe si umesoma sheria na sisi hatujui sheria, basi tunakwenda kutunga sheria na wewe utaitumia tu. Kidumu Chama Cha Mapinduzi."
Kauli hiyo ya Sendeka iliibua shangwe kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo.
My take:
Kauli ya Sendeka kuwa yeye(Masaju) ni mwanasheria lakini wao(kina Sendeka) ni watunga sheria watatunga na Masaju lazima ataitumia tu inaacha maswali mengi badala ya majibu kuwa wakati wa kujadili muswada huu kutakuwa na mvutato mkubwa sana baina ya wabunge wa pande zote.