Semina ya viongozi wa Rais Samia ilikuwa ni ufujaji wa fedha za wanyonge!

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
24,054
71,342
Labda kama walikua wanajipongeza kwa namna wanavyokula kulingana na Kamba zao.

Hayati Magufuli (JPM) hakuitisha cha Semina wala nini, lakini watu walichapa kazi, Pesa zilitokewa na kufika, Kwa JPM ulikua ukila Pesa yake utaitolea kwenye Tundu lolote la mwili wako. Kwa JPM watumishi wabovu walijitenga.

Et Semina, unaongea na watu wazima kama vile unaongea na Familia, tena unaongea na watoto.

Watu walokaa Serikali Kwa vipindi tofauti, na nafasi mbalimbali, bado unawaambia Acheni dharau, msisemane, msilumbane n.k.

Uwiii Taifa limepatikana kweli, eeehh , tutafika tumechoka sana.

Hapa ndipo wenye hekima, busara na akili, waliona mwenye IQ kubwa Hayati JPM apewe Nchi.

(Siku hizi kila linaloshauriwa ni ndiooooooo. Rais Samia anatafuta Cheap popularity, aina ya siasa yake ni halali wakina Nnauye wamshangilie ukizama Ndani zaidi utagundua kwa pamoja wako kwenye levo Moja ya uelewa. #Intelligence 👎).

Niwaombe sana, Wabunge wa JMT aina ya Luaga Mpina na wenye Kariba hiyo, Simameni, semeni, chapeni kazi, Bora muonekane mmekua Wapinzani lakini watanzania wanawaelewa.

Kueni Wapinzani kwelikweli, kwa kuwa sasa hatuna Upinzani.
 
Unateswa sana na roho ya unegativity, na ndyo sifa ya wabongo walio wengi.

Kwan nani kakwambia wamelipwa hela.
 
Ninafikiri ili tupate chama cha upinzani cha kweli inabidi upinzani uchwara uliopo ufe.

Magufuli alijitahidi sana kuua, Samia anauzika kabisa. Sooner or later, tunaenda kupata upinzani wa kweli.

Back to the topic; hii ni awamu ya kula kila mmoja kwa urefu wa kamba yake. Haishagazi.

Wanafidia walivyopoteza enzi za Magufuli. Kwahiyo wanatafuta mianya ili wapige pesa.

Ni wakati wao, kutesa kwa zamu. 😁

Ila wajiandae, baada ya Samia, kazi wanayo.
 
Sasahivi hela zinatafutiwa mifereji ya kutokea, vinaandaliwa vitu ambavyo havieleweki ilmradi pesa itoke tu.
 
Ye kila akiongea na mtu anaangalia namna ya kupata kura yako ya urais. Yaani yupo kwenye kampeni muda wote. Ndio maana alijikuta anasema kuleni kwa urefu wa kamba zenu.
 
Unautaka upinzani wa kweli wa nini wewe mataga? Wa kazi gani hasa??
Ninafikiri ili tupate chama cha upinzani cha kweli inabidi upinzani uchwara uliopo ufe.

Magufuli alijitahidi sana kuua, Samia anauzika kabisa. Sooner or later, tunaenda kupata upinzani wa kweli...
 
Labda kama Walikua wanajipongeza Kwa namna wanavyokula kulingana na Kamba zao.

Hayati JPM hakuitisha Cha Semina Wala nnn, lakini watu walichapa kazi, Pesa zilitokewa na kufika , Kwa JPM ulikua ukila Pesa yake utaitolea kwenye Tundu lolote la mwili wako , Kwa JPM watumishi wabovu walijetenga...
Acha hizo wewe huyo Magufuli si ndio alimweka Samia Kama mgombea mwenza wake au? Alijua ni mtu mwenye misimamo, mitazamo na uwezo Kama wake,😅msilambe matapishi au alimweka mgombea mwenza kama boshen? Unless sielewi maana ya makamu wa raisi 🤔
 
Back
Top Bottom