Chuo kikuu Cha Dar es Salaam kimpe Rais Samia Udaktari wa Heshima katika uongozi na mahusiano ya kimataifa

Lucas mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
14,162
8,551
Ndugu zangu hayo ni mapendekezo yangu binafsi baada ya kuwa nimekaa kwa muda mrefu nikifuatilia utendaji kazi wa mh Rais Samia na kufikiria namna mh Rais wetu mpendwa alivyoipokea na kukabidhiwa nchi yetu Katikati ya wingu zito la majonzi na simanzi kubwa ya kuondokewa na Rais wetu Hayati Daktari John Pombe Magufuli

Ndugu zangu ilikuwa Ni mshituko mkubwa Sana kwetu watanzania kuondokewa na Rais aliyepo madarakani, kwani hakuna aliyekuwa akiwaza Wala kufikiria Wala kuota Kama Jambo lile linaweza kutokea, maana kwetu watanzania lilikuwa Ni Jambo geni sana ambalo halijawahi kutokea,

Hapa shukurani zangu za kipekeee kabisa lazima liviendee vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vilivyohakikisha kuwa mipaka yetu na nchi yetu inaendelea kuwa salama kabisa, lakini pia Namshukuru mwenyezi Mungu ambaye siku zote amekuwa nasi watanzania kwa kutuvusha salama salmini katika kipindi kigumu, lakini pia nawashukuru viongozi wetu wastaafu na hata waliopoo madarakani waliohakikisha nchi inakuwa na utulivu na wanatuongoza watanzania kuvuka salama katika bonde lile la uvuli, Asante pia kwa watanzania kwa namna ambavyo tulibaki watulivu na kuungana Kama Taifa mpaka mwisho wa kuhitimisha safari yake Hayati Magufuli katika nyumba yake ya Milele kule CHATO

Ndugu zangu macho yetu watanzania ndani na nje ya mipaka yetu yakaelekezwa kwa Mama huyu shupavu, mwenye moyo wa huruma upendo na unyenyekevu ulio jaa hekima busara Subira na Aliyejaa hofu ya Mungu, mwenye upendo wa kweli kwa watu na mzalendo wa dhati kwa nchi yetu, msikivu na mwenye kumaanisha kile akitamkacho, mwenye kuchuja maneno na kuchunga ulimi wake

Mh Rais wetu mpendwa Taratibu akaanza kufufua na kuinua matumaini ya watanzania ambayo wakati huo Tulikuwa Tumetoka kwenye majonzi na mshituko, akaanza kuwa mfariji wetu, Akaanza kutufuta machozi, Akaanza kutushika mikono kutunyanyua tulipo kaa ili tuanze safari ya Kuendelea kazi ya kuijenga nchi yetu kwa kauli yake ya kazi iendelee, Akaanza kutuunganisha watanzania kukabili maadui wetu wa ujinga umasikini maradhi Rushwa na ufisadi

Kuna watu walikuwa wamekata Tamaa, Kuna watu walikuwa wanatamani hata kuona kila baya linaipata Tanzania, lakini mama huyu Hodari akazizima roho hizo chafu na kupanda mbegu za upendo na uzalendo katika mioyo watanzania, Ndio maana unaona Leo hii Taifa Ni moja likisonga kwa pamoja,

Hivyo ndugu zangu kwa kuyawaza hayo Nikaona kuwa Ili kuonyesha kutambua mchango wa Rais huyu Hodari haina budi kwa Chuo Kama UDSM kumpa Udaktari wa Heshima mh Rais wetu mpendwa katika uongozi na mahusiano ya kimataifa, sote Ni mashahidi namna mh Rais wetu alivyoliongoza vyema Taifa letu kutoka katika kipindi hicho na namna maendeleo mbalimbali yalivyopatikana, kwani Tumeona namna miradi mingi ilivyojengwa na hata kuendeleze Ile iliyokuwa imeanza kujengwa

Tumeona namna alivyojenga umoja wa kitaifa na mshikamano wa watanzania, Tumeona namna nchi yetu ilivyopata mafuriko ya watalii pamoja na wawekezaji baada ya kuimarisha diplomasia yetu, Tumeona namna alivyoimarisha demokrasia na mahusiano mema na vyama vya upinzani kwa kuwachukulia wapinzani Kama wadau wa maendeleo na kuamini kuwa tunaweza tukatofautiana lakini bado tukaijenga nchi yetu kwa pamoja na tukajivunia mafanikio yetu kwa pamoja

Ni vyema atunukiwe na kupewa heshima hiyo ili Kuendelea kumpa faraja ya kusonga mbele zaidi na kuliinua Taifa hili kiuchumi, Nimependekeza UDSM maana najuwa ndio chuo kikongwe hapa nchini ambacho huwezi ukakiweka kando katika maendeleo tuliyoyafikia Leo hii kupitia wasomi wake waliopita na kupikwa pale,

Niseme tu ukweli Mimi LUCAS Mwashambwa Kama kijana nimetokea kuvutiwa na kuridhishwa Sana na uongozi wa mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani, Ni Imani yangu kuwa ombi hili litapokelewa na kutafakariwa vyema, Apewe tu maana Anastahili kupewa, Ametutoa pagumu Sana watanzania mpaka kufika hapa tulipo, maana amepokea nchi kipindi Cha mdororo wa uchumi Duniani

Kazi iendeleee, Mh Rais Samia Ndiye Joshua wetu atakayetufikisha Kanaan, Mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka na wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti
 
Aisee...
Utakuwa ulifata huu ushauri na kujichukulia..

3.Bachela ya Chawa with Uking'asti
8.Bachelor of Postology

Ndugu zangu macho yetu watanzania ndani na nje ya mipaka yetu yakaelekezwa kwa Mama huyu shupavu, mwenye moyo wa huruma upendo na unyenyekevu ulio jaa hekima busara Subira na Aliyejaa hofu ya Mungu, mwenye upendo wa kweli kwa watu na mzalendo wa dhati kwa nchi yetu, msikivu na mwenye kumaanisha kile akitamkacho, mwenye kuchuja maneno na kuchunga ulimi wake

Mh Rais wetu mpendwa Taratibu akaanza kufufua na kuinua matumaini ya watanzania ambayo wakati huo Tulikuwa Tumetoka kwenye majonzi na mshituko, akaanza kuwa mfariji wetu, Akaanza kutufuta machozi, Akaanza kutushika mikono kutunyanyua tulipo kaa ili tuanze safari ya Kuendelea kazi ya kuijenga nchi yetu kwa kauli yake ya kazi iendelee, Akaanza kutuunganisha watanzania kukabili maadui wetu wa ujinga umasikini maradhi Rushwa na ufisadi

Kuna watu walikuwa wamekata Tamaa, Kuna watu walikuwa wanatamani hata kuona kila baya linaipata Tanzania, lakini mama huyu Hodari akazizima roho hizo chafu na kupanda mbegu za upendo na uzalendo katika mioyo watanzania, Ndio maana unaona Leo hii Taifa Ni moja likisonga kwa pamoja,
Naunga mkono.
Kazi iendeleee, Mh Rais Samia Ndiye Joshua wetu atakayetufikisha Kanaan, Mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka na wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti
Katika kusifu, tusipitilize tukavuka mipaka, badala ya kusifu ukajikuta unatukuza na kumponza kwa machukizo, kuna vitu sisi binadamu tuna mamlaka navyo, na kuna vitu hatuna mamlaka navyo, ni vitu vya mamlaka KUU YAKE YEYE!. Anayejua kama Mama Samia ndiye Joshua wetu sio wewe!, sio sisi, wala sio yeye Mama Samia bali its only HIM!, YEYE!. Tuendelee kusifu lakini tusivuke mipaka!, tukamponza na huyu!.
Hili nimelizungumza hapa Kumkubali, Kumsifu na Kumpongeza ni Kumheshimu, Sio Kumuabudu, Kumtukuza na Kumsujudu!. Wakuabudiwa, Kutukuzwa na Kusujudiwa ni Mungu Pekee!.

P
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom