Umenikumbusha mbali sana sister juu ya definition ya pastor Roman wa zimbambwe tukiwa ester conference miaka hiyo..nikashangaa sana aliposema marriage is a union of two uncomplete people..nilitafakari sana ila siku nilipoingia ktk ndoa ilinisaidia kumvumilia mwenzangu ups and downs zipo popote pale pia ndoa ina raha zake nyingi tu sema ni hulka ya binadamu kuhesabu mabaya kuliko mazuri.....Ujue ndoa ni tamu sana kama ukichukulia kila ulipatalo kama challenge kwenye maisha yako na ukasonga mbele bila kuanza kuwashikirisha wa pembeni ambao always wanasubiri kusikia habari mbaya Wakati wa raha hutawasikia wala hakuna atakayeongea ila upatapo shida jua pia kuwa hiyo ni sehem ya ndoa na pambana na jaribu hilo mpaka mwisho bila kuangalia ndoa ya mwingine au bila kulinganisha ndoa yako na mwingine Ndoa ni ya kwako na always matatizo na mikwaruzano ni part ya hiyo ndoa Jifunze kuwa upatapo raha ndani ya ndoa ni hivyo hivyo pia wakati wa matatizo yanavyokuja na ujue kupambana nayo