Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

20220506_115927.jpg


Sent from my SM-M305F using JamiiForums mobile app
 
Morning Family...
[5]Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.
(Waebrania 13:5)

Mafafanuzi: Fedha ni baraka sana katika maisha yetu. Mungu ameweka fedha ili tuzitawale na si zitutawale. Wapo watu wameharibikiwa kwa sababu ya tamaa ya kupenda fedha. Fedha zisitutenge na Mungu bali zitufanye kuwa karibu zaidi na Mungu. Pia turidhike na vile Mungu alivyotupa hata kama unaona ni kidogo.

Si kila kitu lazima ulipwe fedha. Malipo ya Mungu wakati mwingine ni tofauti sana. Malipo hayo yanaweza yakawa ni amani, afya nzuri, familia nzuri, heshima, uhai, hekima, kibali na vingine vingi ambavyo kwangu mimi ni utajiri mkubwa sana kuliko hata fedha.

Wapo watu wana fedha nyingi lakini ni masikini wa kitu fulani; Mungu anasema kuwa hatakupungukia wala kukuacha kabisa.

Ridhika na ulicho nacho, fanya kazi kwa bidii na Mshukuru Mungu hata kwa hicho kidogo ulichonacho.

Mungu akubariki na nikutakie Ijumaa njema yenye baraka tele. Amen!!

Rev. Frank Kimambo
KKKT😀MP
 
Back
Top Bottom