Mimi nilikuwa namjibu hadi mwisho
Namuuliza nani,?
Kanitajia jina hata silijui..
Namuuliza ndio nani anasema hunikumbuki?
Mimi ni Fulani Fulani
Nikaona nimsikilize,
Anauliza Niko wapi nikamtajia.
Anasema yeye yuko mahala fulani,anafanya kazi huko na kampuni gani sijui
..anatafuta mashine..
Hizo machine Mbeya wanauza bei rahisi kwahiyo amenipa dili ili tupige Hela..
Ataniunganisha na mtu,huyo anaziuza mashine...nimpigie aniuzie halafu kwenye risiti aandike hela pungufu
inayobaki juu tunagawana.
Nikipiga nimwambie kaka Daudi amenipa namba
Anauliza nikutajie namba??
Nikamwambia nitumie kwenye msg..
Akatuma,akapiga Tena
Haki ya nani
nimecheka Mimi.