Imezoeleka kwa wachezaji wengi wanao sakata kabumbu katika klabu kubwa barani ulaya kwenda kupumzika sehemu mbalimbali za kifahari kama fukwe za Ibiza, Hoteli za kifahari, katika majiji ya kifahari au kwenda katika sehemu za kitalii kama alivyofanya mshambuliaji wa PSG Mauro Icard kuja kupumzika Tanzania kutembelea mbuga za wanyama za Serengeti.
Hali ni tofauti kwa mshambuliaji wa klabu Liverpool na timu ya Taifa ya Senegal, Sadio Mane, Nyota huyo badala ya kwenda kupumzika sehemu mbalimbali za kifahari, Yeye hutumia muda wake wa mapumziko kuwa na marafiki zake aliokua nao toka wakiwa watoto pamoja na ndugu na Jamaa na wanakijiji wa kijiji cha Bambali ambako ni nyumbani kwao alipozaliwa, kama anavyoonekana pichani akila maembe na rafiki zake wa kijijini kwao Bambali huku wakifurahi pamoja.
Mane ambaye amekuwa mstari wa mbele kuisaidia jamii yake kijijini kwao, amekuwa akitoa msaada mkubwa kwa jamii yake ya Senegal hususani katika Kijiji cha Bambali alipozaliwa, amekuwa akiwapa misaada mbalimbli ikiwemo pesa za kujikimu, kujenga shule na Hospitali,
Hivi karibuni Mane amefanya uzinduzi wa Hospitali kubwa na ya kisasa aliyoijenga kijijini kwao Bambali kwa gharama ya dola za kimerekani 5,30,000 ambazo ni zaidi bilioni 1.4 kwa pesa za kitanzania,
Mwaka 2019 Mane aliwalipia ada na kuwanunulia sare za shule wanafunzi wa kijijini kwao, kama kama hiyo haitoshi nyota huyo ana mpango wa kufungua kituo cha gesi kijijini kwao kama sehemu ya kuimarisha miundombinu ya nishati
Mane aliwahi kunukuliwa akisema hawezi kuishi maisha ya kifahari kama kumiliki magari ya kifahari, majumba ya kifahari, simu za kifahari wakati ndugu zake huko kijijini wanateseka hivyo chochote kile atakachokipata atagawana na watu wa jamii yake katika kijiji cha Bambali nchini Senegal