Selfika na JF: Snap it. Show it

Aaah kama ibada ni kila siku, hapo lazima ujipange vizuri.

 
Ila wale faraghani ile mikato yao mimi hoii!marinda kabisaa
 

Hivi kumbe na kunyoa ni lazima eeh? Ndiyo nimemkumbuka rafiki yangu fulani hivi, kila nilipokuwa nakutana naye alikuwa amevaa marinda na sijawahi kumuona na nywele.

Yes, cha msingi popote ulipo, uwe na amani nafsini mwako, na Mungu umuone/umsikie: ndicho haswa tunachokitafuta.
 
Kunyoa ni lazima
Kuvaa marinda ni lazima
Ni marufuku kuongeza vikorombwezo mf hereni sijui mikufu..ukijitahidi sana harusini watakubandika lile bango la kimalkia kichwani,huku umechana kipilipili chko kichwani saafi.
Kuna jingine hili ambalo ndio gumu zaidi kwa kweli
la kuchaguliwa mchumba
,kule ukidate tu unakuwa umejiengua..lazima ufwate utaratibu wa kule..japo now kidogo naona wamelegeza,

Mimi huwa naenda kusali Mara mojamoja japo sijatubu bado,yaani ile kuingia rasmi mazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaaa imebidi niisave fasta.

Hizo skirt na sisi tunavaa siku hizi zz kisasa lakini. Hapo kwenye mashati ni lazima yawe hivyo, naona wengi naokutana nao wanakuwa ni kama wanashona suti sijui ( full), huwezi kuvalia blauzi nyingine? (Usinichoke na maswali yangu mweeh)
Ndio pigo zetu zile

Namna hii,unikute nimepitisha pasi kwenye rinda langu kaliii hadi linaweza kukata my
View attachment 1789508

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe uliza tu mimi nitakujibu


Miaka ya nyuma ilikuwa kama ni lazima kushona suti.
Miaka hii kidogo kumelegea,unaweza vaa blauzi yoyote..ila uangalie isiwe nje ya maadili.
Unaweza nunua suti ya dukani,ukachukua ile koti,ukashona na sketi ya marinda knayomatch na koti ukavaa..wengi wanafanya hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo kutubu ni kama kurudi kundini kwa sababu ulitoroka dhehebu eeh?

Hiyo ya kuchaguliwa mchumba ndiyo shughuli sasa, so kijana anamfuata kiongozi kwamba nimempenda fulani mnifikishie ujumbe; au viongozi wanakaa tu wanaona Saint Anne na John watafaana, mnaitwa mnaunganishwa au?

 
Hivi ni kweli upo Faraghani?

Nimezaliwa faraghani Mimi ila bado sijatubu,yaani ile kuingia mazima..
Na kwa umri niliofika inabidi niingie mazima,hakuna kuingia tena kwa mgongo wa mzazi.
Hata hili jina la Anne lilitoka faraghani,sema baada ya maombi makali wakachagua lile ninalotumia official.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Doh!
Tena wale watu wazima naona hao msimamo bado mkali.. No Bra.
Yaani wale wa zamani age za akina mama huwaambii chochote.

Vijana kidogo tunaanza kuimodify lakini hata nywele inatakiwa unyoe level moja..
Vijana siku hizi wanakwangua tu pembeni,katikati zinabaki nyingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie kumbe kweli, mimi sikuwahi kulifuatilia na kuvaa bra. Sasa wenye mizigo yetu na shimizi jamani mweeh.

Hivi na uzazi wa mpango hauruhusiwi? Jamani jamani kuna sehemu niliendaga nikamkuta huyo mama, ana watoto wengi, hawajapishana umri na anaendelea kufyatua kila inapowezekana. Ndiyo majirani wakawa wanateta eti hawaruhusiwi kutumia uzazi wa mpango

Nawaonaga nadhani hata Bra sijui ni hawaruhusiwi au vipi..
Hiyo ilikuwa miaka ya nyuma.
Ilikuwa unatakiwa kuvaa shimizi


Siku hizi wamelegeza,Kuna wanaovaa bra,,wengine wenye msimamo mkali bado wamekomaa na shimizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera mdogo wangu..
Umechagua fungu lililo jema..nakumbuka kuna familia moja niliwahi kwenda wanasali faraghani.

Siku moja Jumapili wakataka kunipeleka changamoto ikaja kwenye nguo. Kwanza skert au gauni linapaswa kufika miguuni. Blauzi inatakiwa kufunika mikono.

Mimi nikasema nyie nendeni tu. Ila ni watu mna UPENDO sana..
 
Yaani kutubu ni Kama kuingia rasmi..
Mfano umezaliwa uwata yaani wazazi wako wanasali humo...wewe unakuwa unaenda kusali hadi utakapokuwa mtu mzima Sasa ndio unatakiwa utubu,huingii tena kwa mgongo wa wazazi.
Yaani kama kupata kipaimara.

Mf mtu akitaka kuoa ,anapeleka kwa uongozi,anaweza ambatanisha majina ama akaenda tu hvyohivyo ,miaka hii kidogo wamelegeza, anaweza enda na majina pale..baada ya maombi wanamchagulia mmoja.
Hairuhisiwi kudate,ati sijui kaka amekupenda aje akuapproach,akikutaka na wewe ukakubali na ikabainika mna mahusiano basi tayari nyie mmejitenga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…