/
Mimi ni yule mmoja, kati ya wale kumi.
Uliowaponya ukoma, kwako nimerudi.
Wale tisa sijui,
Ila mimi nimekuja kusema Asante!
Najiuliza, Nikulipe nini?
Kwa yote ulonitendea mimi,
Baba ni mengi,
Siwezi lipa hata kwa senti.
Natafuta namna nzuri ya kukushukuru ninakosa,
Natafuta maneno mazuri ya kukushukuru ninakosa,
Ee Baba,
Nikulipe nini, nikulipe nini?
Uliyonitendea ni mengi,
Siwezi kuhesabu!
Ila nina neno moja,
ASANTE.
Uliyonitendea ni mengi,
Siwezi kuhesabu!
Ila nina neno moja,
ASANTE.
(Uliyonitendea...)
Uliyonitendea ni mengi,
Siwezi kuhesabu!
Ila nina neno moja,
ASANTE.