My Best Movies.
Filamu zangu nilizo zikubali.
Flight movie Kali, Rubani mraibu wa vilevi /dawa za kulevya kama cocaine na pombe, rubani huyo hodari muda mchache kabla ya kurusha ndege anapiga mitungi, hitilafu inatokea kwenye ndege na chanzo Cha hitilafu si ulevi wake, Kwa ujasiri wa hali ya juu anafanya maamuzi magumu na kuokoa maisha ya abiria japo yupo nzwiii, baada ya ndege kutua kwenye makazi ya watu na anapoteza ufahamu anajikuta hospital wamempima damu na kugundulika alikua yupo tungi, noma inaanzia hapo akitaka kupoteza ushahidi. Movie Kali sana.
Hii movie ya 2006 lakini huwa naikubali sana, story ni mwaka 2027, baada ya uchafuzi wa mazingira, vita na machafuko ya kisiasa binadamu hawana uwezo tena wa kuzaa Kwa takribani miaka 20, anatokea binti mdogo ana ujauzito anaitwa Kee, kila mmoja anamtaka mtoto aliyezaliwa, vita inaanzia hapo panakuwa hapatoshi, siwezi elezea vizuri unaweza soma Plot IMDb, ni movie Kali sana hutojutia.
Kama unapenda Love Story tafuta hii movie inaitwa Acrimony, love story Kali sana, yupo Taraj P Henson. Nadhani ni one of the my best love story of all time.
Kwa India/Bollywood japo si mpenzi sana, lakini ANDHADHUN movie Kali, story Kali, love story na action za kutosha, jamaa alikua anaigiza kipofu katika harakati za kujitafuta, akiwa hodari wa kupiga piano akifanya kazi kwenye bar, anaitwa kwenye nyumba ya bilionare mmoja ili akapige piano, akiwa hapo anashuhudia mauaji ya bilionare huyo na muuaji anajua jamaa haoni ni kipofu, msala unaanzia pale wamemshtukia si kipofu na ili kupoteza ushahidi lazima auawe.
Movie za Zombies, Horror na fantasy si mpenzi sana japo kuna chache nilishazipenda kama Day Shift ya Jamie Foxx na nyingine baadhi, lakini kuna wadau wengi wanazikubali.
List ni ndefu, nimechoka kuandika, I wish tungekuwa tuna share, lakini watu wangu wa Jf nawaza iwepo platform ya kushare movie Kali na download links ukiachilia Telegram kwenye magroup ya malipo nowdays kuna restrictions sana, muwe mnashusha movies for free no malipo kabisa, Hapa kuna raia wanajua movies nyingi... Am thinking issue ya copyrights infringements, inabidi isivuke mipaka ili DMCA wasiipige chini, but nitafanikisha tu namna ya kufanya, Nina Google drive ina 100TB na Sina Cha kuifanyia.
Love you all, Good Morning..