Self-Contained Houses: Kuna umuhimu gani wa kuwa na choo pamoja na bafu "separately"? Kwanini hivyo nyumba viwili visiwe na matumizi yanayofanana?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Katika ujenzi wa kisasa, kuna umuhimu gani wa kuwa na choo pamoja na bafu "separately" katika nyumba ambazo ni self-contained? Kwanini hivyo nyumba viwili visiwe na matumizi yanayofanana?

530945_img-20200919-185033-212_1500x1125.jpg

Yaaani yale yanayofanyika bafuni yafanyike pia kule chooni na yale ya chooni pia yafanyike bafuni.

Kwanini baadhi ya watu hupendelea kuwa na chumba kimoja ambacho kinakuwa na matumizi ya namna zote mbili ila wengine hutenga vumba viwili vikiwa na matumizi mawili tofauti?

WATAALAM WA MASUALA YA UJENZI PAMOJA NA DESIGNING MSIPITE BILA KUTOA UFAFANUZI JUU YA HII TREND.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE.
 
Kwa kifupi mkuu ujenzi mwingi hapa bongo watu wana copy na Ku paste..
Ukiuliza kwann nyumba nyingi chini wanapaka rangi nyeusi,,au wanapaka rangi tofauti na rangi ya ukuta wa juu ,,majibu hakuna,
Nyumba nyingi ni mfumo wa sketi na blauzi..
 
Kwanini hivyo vyumba viwili visiwe na matumizi yanayofanana?
Nadhani ni maamuzi yako tu mkuu hakuna sheria wala anayekupangia,
Choo kina gharama kuliko bafu katika ujenzi kwa hiyo ni wewe tuu
Usijenge nyumba kwa kuangalia mtu,jenga kwa hitaji lako ukiona uwe na public toiet mbili ni sawa tu
Wengine ndo maana uwa na choo cha nje na cha ndanj hayo yote ni mahitaji ya mtuyaani ndani anakuwa na public toilet na nje ya nyumba pia inakuwepo,kwa hiyo ni wewe tu na pesa yako na hapo hapo anakuwa na master room
 
Kwa nyumba za biashara tunajenga choo na bafu kuokoa nafasi. Tena sikuhizi mabafu ya cubicle ya mchina yametuokoa kweli 150 cm2 inatosha choo, sink la kunawa mikono na bafu.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Nimekuelewa sana Souldier, Kuna jamaa alikua anajenga hivyo nikamwambia huoni kama ni gharama, akaniambia kanuni za ujenzi lazima zifuatwe na kanuni yenyewe ni kuwa maji ya bafuni na maji ya chooni yanatakiwa yawe separate kwenye mfumo wa subtank.

Lakini sikumuelewa maana unaweza kutenganisha hayo maji kwenye zile chemba za nje. Kama angenielewa angeweza kufanya room nyingine ikawa self na bado public toilet ikabaki pia.
 
Kwa ujenzi wa kisasa una weka chumba kimoja kwa taka za ndani ya mwili kinyesi na mkojo na za nje kuoga kupiga mswaki n.k angalizo kama hauna hela za kutosha ni bora ukajenga kwa kutenganisha kwa sababu maji ya taka ya nje mwili na manisha yenye sabuni na kemikali kama shampool zina weza kuingia kwenye sinki la choo na kupelekea kuua backteria wanao mengenya kinyesi na kupelekea choo kujaa haraka ni hayo tu
 
Aisee maada nzuri sana hii, hata mimi kiukweli sion haja ya Kujenga choo na bafu kwa kutofautisha, hapo inatakiwa choo na bafu viwe chumba kimoja ila kama utataka kuwe na vyumba viwili basi kila chumba kiwa na choo na bafu humohumo kwani matumizi ni yaleyale, haiwezekani unaingia hiki kwa matumizi mengine halafu ukimaliza unatoka na kuingia chumba kingine kuoga huo ni usumbufu usio na maana....

Hapa nimepata hilo wazo punde hiki chumba cha bafu humu ndani nitamuita Fundi tujadiriane ili ikiwezekana kilekebishwe kiwe kinatoa huduma zaidi ya moja
 
maji ya taka ya nje mwili na manisha yenye sabuni na kemikali kama shampool zina weza kuingia kwenye sinki la choo na kupelekea kuua backteria wanao mengenya kinyesi na kupelekea choo kujaa haraka ni hayo tu
Mkuu, hii ndio kwanza nimeisikia leo kwako mzee baba. Hakika JF ni kisima cha maarifa...
 
Mkuu, hii ndio kwanza nimeisikia leo kwako mzee baba. Hakika JF ni kisima cha maarifa...
Choo kina kina mfumo maalum hivi vyoo vya kuchuchumaa ni mtihani sana vina itaji mfumo wa kutenganisha na maji taka ya nje ya mwili kwa umakini sana cha kukaa hakina shida ni easy sana so yote kwa yote ni kuzingatia maji ya nje ya mwili aya ingii kwenye chemba za kinyesi
 
Aisee maada nzuri sana hii, hata mimi kiukweli sion haja ya Kujenga choo na bafu kwa kutofautisha, hapo inatakiwa choo na bafu viwe chumba kimoja ila kama utataka kuwe na vyumba viwili basi kila chumba kiwa na choo na bafu humohumo kwani matumizi ni yaleyale, haiwezekani unaingia hiki kwa matumizi mengine halafu ukimaliza unatoka na kuingia chumba kingine kuoga huo ni usumbufu usio na maana....

Hapa nimepata hilo wazo punde hiki chumba cha bafu humu ndani nitamuita Fundi tujadiriane ili ikiwezekana kilekebishwe kiwe kinatoa huduma zaidi ya moja
Hilo lina wezekana me kama plumber cha muhimu ni kuzingatia maji taka hayaingii kwenye chemba za kinyesi hii ita pelekea kuua backteria wanao mengenya kinyesi na kupelekea choo kujaa haraka na ni choo Cha kuchuchumaa unaitaji uangalifu sana
 
Kwa ujenzi wa kisasa una weka chumba kimoja kwa taka za ndani ya mwili kinyesi na mkojo na za nje kuoga kupiga mswaki n.k angalizo kama hauna hela za kutosha ni bora ukajenga kwa kutenganisha kwa sababu maji ya taka ya nje mwili na manisha yenye sabuni na kemikali kama shampool zina weza kuingia kwenye sinki la choo na kupelekea kuua backteria wanao mengenya kinyesi na kupelekea choo kujaa haraka ni hayo tu
Shimo labda liwe dogo. Lakini pia ukitaka usipate usumbufu wa choo kujaa, tenga shimo lako yawe mawili (two in one), moja liwe la kupotezea maji.
 
Hilo lina wezekana me kama plumber cha muhimu ni kuzingatia maji taka hayaingii kwenye chemba za kinyesi
Mkuu, leo unanipa shule moja nzuri sana. Nilikuwa sijui kama kuna chamber special kwa ajili ya taka ngumu (kinyesi) pamoja na chamber za maji ya mwilini...
 
Back
Top Bottom