Hayati Magufuli: Hivi kuna umuhimu gani wa Kuwa na Chipukizi wa miaka 8-10? CCM, Chadema, CUF wote wakiwa na Chipukizi hawa Watoto watasoma Saa ngapi?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,998
142,025

Pamoja na kutuma Salamu za mwaka Mpya na kuwapongeza Chipukizi Watoto wa viongozi nimeona niwaletee hii nukuu ya Shujaa Magufuli kama nilivyoikuta mtandaoni Mfanyakazi Online

" Hivi kuna umuhimu gani wa Kuwa na Chipukizi wa miaka 8-10? Sisi tukiwa na Chipukizi, Chadema wakiwa na Chipukizi, CUF wakiwa na Chipukizi hawa Watoto watasoma Saa ngapi?!" John Magufuli 23 July 2016

Mlale Unono 😀😀
 
Chipukizi sio jambo jipya, huko shule za msingi tume kuwa chipukizi miaka nenda rejea

Skauti nk

Hivyo tafuta maarifa kufahamu chipukizi ina nini ndani yake, scout pia nk

Sizani kama wazazi nao ni wajinga kuruhusu watoto kuwa ktk platform mbalimbali zinazo wajenga
 
Mwamba umemnukuu vizuri sana.

Upinzani wakireflect huu mfumo naamini miaka ijayo kuna mtu atapigwa 6-0.

Huu ni mfumo wa kupandikiza mambo kwa mtoto kuwa chama fulani ni hatari kwa afya yake.

Mtoto hutomwambia kitu huko mbele ya safari. Nijuavyo mimi haya ushabiki wa Simba na Yanga unaanzia utotoni.
Hivyo ni ngumu kumuaminisha mtu kuwa upande fulani asioupenda ni mzuri.
 
Pamoja na kutuma Salamu za mwaka Mpya na kuwapongeza Chipukizi Watoto wa viongozi nimeona niwaletee hii nukuu ya Shujaa Magufuli kama nilivyoikuta mtandaoni Mfanyakazi Online

" Hivi kuna umuhimu gani wa Kuwa na Chipukizi wa miaka 8-10? Sisi tukiwa na Chipukizi, Chadema wakiwa na Chipukizi, CUF wakiwa na Chipukizi hawa Watoto watasoma Saa ngapi?!" John Magufuli 23 July 2016

Mlale Unono 😀😀
Ngoja niwasaidie Matomaso.
 
Kuwa na chipkizi ni msingi bora sana kwa taasisi imara zenye maono na malengo ya mbali....
Huuandaa waongoza taasisi weledi na waadilifu...

kwa wenye ufinyu katika uelewa na ufahamu juu ya umuhimu wa chipkizi Lazima ataona hili ni anasa...

taasisi isiyo na maono ya mbali matokeo yake ni kujenga jumuiya ya waporomosha matusi, kuzira na kususa, fujo, maandamano, mihemko, ghadhabu, uporaji , ubishi bila hoja kama ambavyo hujitambulisha wanapogongwa na hoja humu Jukwani.....
 
Chipukizi sio jambo jipya, huko shule za msingi tume kuwa chipukizi miaka nenda rejea

Skauti nk

Hivyo tafuta maarifa kufahamu chipukizi ina nini ndani yake, scout pia nk

Sizani kama wazazi nao ni wajinga kuruhusu watoto kuwa ktk platform mbalimbali zinazo wajenga
Sizani = Sidhani

Huko shule mnasoma Saa ngapi?🐼
 
Magu alikuwa vizuri sana yule mwamba. Akili yake ilikuwa kubwa kuliko ccm wote nchini wakiwa combined.

Alizingua sehemu moja tu kwenye ukatili na kupenda kutumia maguvu kupitiliza ndo akaichafua CV yake. Otherwise angekuwa bonge moja la kiongozi na nusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa ccm hii na upumbavu wa wtz huu usipokuwa katili na kutumia maguvu si watakutia madole kwenye macho kama wanavyomfanya Samia?
 
Kuwa na chipkizi ni msingi bora sana kwa taasisi imara zenye maono na malengo ya mbali....
Huuandaa waongoza taasisi weledi na waadilifu...

kwa wenye ufinyu katika uelewa na ufahamu juu ya umuhimu wa chipkizi Lazima ataona hili ni anasa...

taasisi isiyo na maono ya mbali matokeo yake ni kujenga jumuiya ya waporomosha matusi, kuzira na kususa, fujo, maandamano, mihemko, ghadhabu, uporaji , ubishi bila hoja kama ambavyo hujitambulisha wanapogongwa na hoja humu Jukwani.....
Waongoza taasisi weledi bongo hii?

Utakuwa unaishi Ulaya si nchi hii.

Akina Kikwete, Lowassa nk waliandaliwa na ccm ya Nyerere ila cha moto tumekiona, unazungumzia weledi kwa chipukizi wa kuandaliwa na Mwigulu, Nape, January nk? Mbaya zaidi hadi DNA zao ziwe katika hao chipukizi, baadhi zikishikilia uongozi kabisa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom