Selelii agoma kurudi Bungeni!?

Status
Not open for further replies.

Hata mimi nashangaa wale wote hapa wanaowatetea wabunge ambao hawajafanya lolote kwenye majimbo yao.

Mbunge mzuri anachanganya akili ya kwenye jimbo na ile taifa. Kumbuka yule mbayuwayu wa JK, tumia akili ya Mgaya na ya kwako.

Ni rahisi mno mtu kupiga kelele za mambo ya kitaifa kwasababu haziendani na utekelezaji. Kwa mbunge utekelezaji uko kwenye jimbo lake na wengi huko ndio wanachemsha na badala yake kuwa kwenye TV kila siku wakijifanya wanatetea maslahi ya taifa. Kama unaweza kutetea maslahi ya taifa kwanini ushindwe kutetea maslahi ya jimbo lako?

Mbunge anayeshinda kufanya mambo ya jimbo lake tu HAFAI!
Mbunge anayeshinda kufanya mambo ya taifa tu HAFAI!

Jimbo plus Taifa ni kidedea!
 

buckreef,

Maswali aliyouliza Mwanakijiji siyo rahisi kujibiwa na Mbunge mtarajiwa kama unavyodhani/ulivyojibu. Manake umejibu kama mpiga kura, in short, hujamjibia/kumsaidia mbunge mtarajiwa!

Jaribu kuvaa viatu vya mgombea and you are facing the nation.
 

Mheshimiwa mtarajiwa kigwangalla, natumaini MKJJ amekupatia nafasi muafaka ya kuonyesha nia yako kwa dhati!!
Uwanja wako sasa...
 


kama ungekuwa ni mtihani ndugu yangu ningekufelisha vibaya sana. Bado namsubiria mbunge mtarajia aje anipe mtazamo wake usiouliza maswali juu ya maswali bali majibu yanayoeleweka ya kila swali. Lengo langu ni kujua mtazamo na msimamo wake kuhusu mambo hayo na labda mengine nitaendelea nayo baadaye. Sina sababu ya kumtega.
 

Tatizo sio watu kuwa negative au kuzuia watu wasigombee. Tatizo ni kauli zao/zenu wagombea za kushindwa kuthamini michango ya wabunge wa sasa ndani na nje ya Bunge. Kauli kama 'seleli ametumia miaka mitano kuzungumzia ,masuala ya Richmond'. ndio zinazotia kichefuchefu wengi wetu. Siku hizi siyo kazi kupata hata hansard online kujua mbunge wako amepigania nini na serikali imemjibu nini katika miaka mitano. Jamani badilini strategy mpate response nzuri! Vinginevyo mtakuwa mkitoa kichwa tu mnashambuliwa faster.

Fikiria mtu (Zyansiku) anayehubiri habari ya Seleli kuchelewa Bungeni wakati huo huo anampamba Rostam kutawazwa ukamanda wa vijana. Kana kwamba ni suala la maana sana kitaifa, Mbunge ambaye ni mtoro Mkuu wa vikao vya bunge na ambaye hajawahi kuchangia chochote bungeni (kama katiba mnavyotaja wajibu wa mbunge/bunge). Halafu unategemea great thinkers warespond vp?

Narudia tena, WABUNGE WOTE WAPIGANAJI HAWAJAWAHI KUPITA BILA KUPINGWA. Hata huko nyuma walipitia kwenye michakato hiyo hiyo na wapinzani wao. Na kwa taarifa yenu wabunge hupenda wapinzani wengi ili kura zigawanyike wapite kilaini.
 
Mzee Mwanakijiji,

Huna shukrani kabisa mbona unakataa majibu yangu?

Ita mgombea yeyote wa kutoka CCM hawezi kukupa majibu ya maswali yako maana siasa ni umoja. Upinzani watatoa majibu lakini na wenyewe wakiingia madarakani basi wanafunga midomo.

Mimi nikiwa mgombea siwezi kuja hapa JF, kuna Wanoko wengi sana.
 
Sasa huyu ndiye nani? Mimi sipendi kweli haya magwanda ya kijani.
Nilidhani ndio dr hamis (Mfili embiei)? au zyansiku?
Nimependa pozi lake...kuhusu magwanda sisemi mengi maana hata Nyerere aliyeyabuni inasemekana hajawahi kuvaaa
mix with yours
 

Mkuu, allow me to apologize for sleeping early last night... nilimiss hii post yako!!! pili naomba uondoe ujinga wa kujisifia kwamba nilikuwepo tangu enzi fulani, huo ni upungufu wa uelewa na nashangaa sana eti umemaliza juzi elimu yako ya juu zaidi... you make wale watumishi wanaojisifia kuwa idara moja kwa miaka 40 wawe ma-genious!!! una upungufu mkubwa sana wa upeo na nahisi you dont listen to many people around you... in short unatia huruma!!!

Tatu, you can not tell me to shut up because you are not my mother

Nne, you know exactly what i mean and that is the reason your adrenaline went up last night buddy!!!

Now back to my points, Hamisi anaelewa nasema nini, na kwa kuwa mimi ni zao la MUCHS [even before MUHAS], tuna a very good network nyingine ambayo si jamii forums, jambo forums wa whats-up forum.... tunashare mengi na wewe si mwenzetu,.... he has his issues wakati akiwa daruso na hata alipokua intern wakati wa mgomo

he is a hypocrit... na kujisifia anawajua watu wote maarufu na kuwa mbishi wa kupokea ideas.... jiulize ule mgomo wa intern uliosababisha akina **** kupoteza kabisa wito ulikuaje???? he has lots of acronyms but ask him je ana-practice hiyo medicine?? je amesomea agriculture, ambayo ndiyo anaifanyia kazi kwa sasa?? nimemaliza na wewe unayedhani kuwa kwenye forum kuanzia 2005 kunakupa uhuru wa kuwa kiranja.... the motion was not about you but you really put a show ---- just like alicia keys

tuliza kitenesi na 2005 yako au unataka ku-trigger metamorphosis ya watu kuanzia 2007??
 
kwa anayeuelewa kweli mfumo wa sasa wa nchi hii... huwezi kuleta maendeleo sustainable kwenye jimbo lako kama sera, miongozo na ilani za nchi yetu bado ziko jinsi zilivyo... waliofanikiwa to go around wote ni wenye pesa za kutisha ambazo hazilingani na rekodi zilizopo TRA... tuache ujinga na kudanganyana kwamba kuna mbunge yeyote anayeweza kuendeleza jimbo lake kwa njia safi

its either yuko jikoni anaamua kupindisha plans na kuhamishia barabara, umeme au maji kwake
au ni rich fella to cash a few weak individuals kubadili mipango
au ni msomi aliyebahatika kupata research au fedha za mipango fulani na kuchagua kwao kama pilot
90% ya wabunge waliopo hawawezi kufanya hivyo na hamisi ni mmoja wao

maswali mengine yanahitaji kuangali unauliza ukiwa kwenye media gani!!!!
 

Hata mimi nashindwa kukuelewa, badala ya kudodosa dodosa si sema? Unaogopa nini? Toa madudu yote ya huyo jamaa ili wengine wote wajue.

Lakini kama huna pia kaa kimya kama alivyokuambia huyo jamaa mwingine. Naona kama unaandika mengi sana kwa kuficha ficha. Au na wewe ni fisadi unaogopa kujulikana ulifanya nini huko intern.

Inaelekea una mahasira sana, punguza usije ukapasuka.
 
Ngoja nende kulala kwetu huku ni saa 9 usiku sasa hivi. Nakuacha de novo ukiendelea kutapika ukweli wanaoutaka....hehehehehehehehehe wasiotumia literature background ni vigumu kukuelewa na hasa unapozungumza na mainjinia. hahahahahahahha
 

si lazima kuinua mkia wa mbwa kujua tundu liko wapi mazee.... i just showed you where the tail is
 
same, urambo, kyela, nzega, simanjiro, nk. tatizo si mabadiliko ndugu, tatizo ni dhamira iliyo nyuma yenu.... namjua hamisi vizuri sana na dhamira zake pia.... NEED WE GO DEEPER?

Come on DE Novo, We dare to talk openly!....and remember, You Will Never Walk Alone! :hail::hail::hail::hail:
 
sasa huyu ndiye nani? Mimi sipendi kweli haya magwanda ya kijani.

95% ya wavaaji wa magwanda ya kijani ni "yes sir," "huyu ni mwenzetu," "mzee kasema hivi." na mambo ya aina hiyo. Inawezekana yeye ni katika ile 5% inayobaki.
 
si lazima kuinua mkia wa mbwa kujua tundu liko wapi mazee.... i just showed you where the tail is


Inaelekea wewe unamjua sasa saidia maswali haya, na wengine mnaomjua mwaweza kutusaidia kumjua vyema Doctor wetu Mbunge mtarajiwa



Muhimbili alimaliza mwaka gani? Intern alifanyia wapi? MPH, & MBA yake aliipata wapi na chuo gani or was online? Tunaomba ingawa ka Research/Dissertation yake aweke hapa kwanza kabla ya hayo maswali ya Richmond, ATCL, TANESCO....etc :redfaces:
 


Huu ndio uchaguzi wa 2010....duh tutaona na kusikia mengi !
Mix with yours
 

Kaka, nimesoma michango yako mingi hapa JF, naona kweli hata huo udaktari haukufai kabisa. Unachemka shauri ya mambo madogo utafikiri ni mvuta bangi wa manzese? Daktari kama una hasira hivyo si unaua wagonjwa huko?

Hao unaowatuhumu lete ushahidi wote hapa na wengine tufaidi. Vinginevyo fungua Ze Utamu nyingine ambako ushahidi sio muhimu bali lengo ni kuchafuana tu.

Haya mambo ya kung'ang'ania huyu alifanya hili na yule alienda Monduli bila kuweka hata kaushahidi kadogo sio tabia ya mtu msomi, ni tabia za house wives wakiwa saloon.

Ningekufahamu kwa jina hiyo hospitali yako ningeigopa kama ukoma maana inaelekea umesoma lakini hujaelemika.

Mimi bado nakupa nafasi, lete data za huyo daktari mwenzako tumchambue kama mchele. Lete pia data za huyo aliyeenda Monduli na mwenyewe kama ni kweli tumuumbue. Kama huna kweli unastahili kukaa kimya ili kulinda heshima yako.
 
Sasa huyu ndiye nani? Mimi sipendi kweli haya magwanda ya kijani.

Baadhi yao ni marafiki zangu na huwa nawachekea vizuri tu lakini laiti wangefunua moyoni mwangu...ni kichefu chefu kama mama mwenye mimba changa
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…