SEKEI ARUSHA:Mchango wa lazima 20,000 tshs

yorkshire

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2016
Posts
2,532
Reaction score
3,177
Nimetoka kibaruani hapa sasa hivi naambiwa kuna mchango wa lazima tshs 20,000 kuchangia sijui shule tena nikajulishwa kuwa sasa hivi imebadirika imekuwa elfu 70, kitu kilichonisikitisha zaidi nimeambiwa kwamba wale wote waliokutwa majumbani mwao leo hawana hiyo hela wamebebewa vitu vyao kama tv,deki n.k kufidia mchango wa lazima wa elfu 20,000 .Naomba kama kuna kiongozi yeyote wa serikali alitolee ufafanuzi hili maana mbaya zaidi wapangaji ndio walioipata adha hii
 
hili jambo la kweli kabisa limetokea leo na wapangaji wamechukuliwa vitu vyao
 
Kwani maeneo hayo ulipo hakuna viongozi wa SERIKALI au wa kwenu wapo humu JF?
 
Pamoja na kwamba kuna vitu umedanganya ili kuongeza chumvi na hivyo kutimiza dhamira yako, nakujulisha hakuna mchango wa namna hiyo bila wananchi wenyewe kupitisha kwenye vikao vyao.

Nakushauri uliza mikutano uliyokuwa unaitwa na kuingia mitini iliamua nini?
 
ilishatokea huku moshono kitu kama icho, niliwazingua kwanza sina mtoto so siwezi na sitachanga, pia niliwaambia waniletee barua officially ya serekali ya mtaa au jiji(whatever you may call it) yenye muhuri wa serekali na signature ya mwenyekiti wa mtaa, diwani na mkuu wa mkoa na pia kama ni lazma wanioneshe sheria inayonilazimisha nitoe mchango huo.
Haiwezekani nifanye kwani kodi yangu inaenda wapi tunalipa mapato kila mahala bado kodi ya kichwa tu.

Nimetoka kibaruani hapa sasa hivi naambiwa kuna mchango wa lazima tshs 20,000 kuchangia sijui shule tena nikajulishwa kuwa sasa hivi imebadirika imekuwa elfu 70, kitu kilichonisikitisha zaidi nimeambiwa kwamba wale wote waliokutwa majumbani mwao leo hawana hiyo hela wamebebewa vitu vyao kama tv,deki n.k kufidia mchango wa lazima wa elfu 20,000 .Naomba kama kuna kiongozi yeyote wa serikali alitolee ufafanuzi hili maana mbaya zaidi wapangaji ndio walioipata adha hii
 
Diwani wa Sekei ni Chama gani?
Diwani wa Sekei mi wa CHADEMA anaitwa Mheshimiwa Deus Kessy. Ila eneo linalolalamikiwa halipo kata ya Sekei bali kata ya Kiutu.

Mchango huu ni wa halali kabisa kuchangia maendeleo na vikao vya tangu mwaka Jana 2017 vilishaamua mchango uwepo. Mwenyekiti wa kijijini Sekei mheshimiwa Daniel Sambu Sagiraki amefanya kazi kubwa kuhamasisha maendeleo haya.

Tuwaunge mkono viongozi na kama hukutoa 20,000 ndani ya muda uliowekwa basi lipa tu hio elfu 70 na faini.

Na ujifunze kuhudhuria vikao/mikutano ya kijiji
 
Pamoja na kwamba kuna vitu umedanganya ili kuongeza chumvi na hivyo kutimiza dhamira yako, nakujulisha hakuna mchango wa namna hiyo bila wananchi wenyewe kupitisha kwenye vikao vyao.

Nakushauri uliza mikutano uliyokuwa unaitwa na kuingia mitini iliamua nini?
wewe usizungumze vitu usivyovijua mimi sina utaahira wa ubongo hadi nije kuropoka jambo lisilona ukweli kama umetumwa uje ukanushe ni bora ukaja sekei kuanzia maeneo ya idara ya maji na sehemu za muungano ufanye upate majibu maana ni familia nyingi zimekutwa na balaa hilo
 
Mtu asogeze pua yake kwenye Deki yangu nitamwonesha kwani Gunia na Dunia hutofautiana Herufi za Mwanzo.
 
Diwani wa Sekei mi wa CHADEMA anaitwa Mheshimiwa Deus Kessy. Ila eneo linalolalamikiwa halipo kata ya Sekei bali kata ya Kiutu.

Mchango huu ni wa halali kabisa kuchangia maendeleo na vikao vya tangu mwaka Jana 2017 vilishaamua mchango uwepo. Mwenyekiti wa kijijini Sekei mheshimiwa Daniel Sambu Sagiraki amefanya kazi kubwa kuhamasisha maendeleo haya.

Tuwaunge mkono viongozi na kama hukutoa 20,000 ndani ya muda uliowekwa basi lipa tu hio elfu 70 na faini.

Na ujifunze kuhudhuria vikao/mikutano ya kijiji
Diwani wa kata ya kiutu anaitwa nani na ni chama gani?
 
Back
Top Bottom