Seif Tumekusikia; Sasa jiuzulu na iondoe CUF kwenye SUK!

.

Afanye hivi ili chama chake kifanye harakati ya kuiondoa Zanzibar kutoka kwenye Muungano na Wazanzibar wakikubali kwenye kura ya maoni yao basi CUF ikishika madaraka Zanzibar ifikirie namba ya kuingia kwenye "muungano wa Mkataba' na nchi yoyote nyingine (si lazima iwe Tanganyika). Kwa kufanya hivi Seif ataonesha mfano kwa viongozi wengine wote wa Zanzibar wenye kuamini Muungano wa Mkataba kutoka kwenye nafasi zao na pia wale Wazanzibari walioko kwenye huduma ya Muungano wa sasa watoke. Lakini zaidi sana Seif akiamua kujiuzulu nafasi hizo wabunge wake wa CUF walioko kwenye Bunge la Muungano nao waamue kufuata mkumbo ili harakati za Uhuru wa Zanzibar (secession) zianze rasmi zikiongozwa na Seif.
.

Da Mwanakijiji siamini kama hii ni kweli!!!Nategemea watu wanao husika na hotuba za viongozi mara baada ya kusikia hiv nini kilifuata.Kwa Mshangao mkubwa hivi bado yuko ofisini!?????????????????.

Nina hoja mbili:
1: Kwake Yeye Binafsi
Kwa hotuba yake hiyo anapaswa kuanzia pale alipomaliza hotuba yake hiyo,awakabidhi maafisa anaoandamana nao vingola vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kisha aende kwa usafiri wake binafsi kwenda kukabidhi mafile yake anayomiliki kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ASIYOKUWA MUUMINI WAKE.

2: Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Kwao wao mpaka dakika hii Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwepo ofisini ni dhihaki na kama sio matusi basi, sisi watoto wa kizazi cha sasa Mungu anayetusimamia si wao!!!.

Marehemu baba wa Taifa wakati wakina Mzee Marecela walipomshauri Mzee Mwinyi mwalimu anaita ushauri Mbaya juu ya Serikali tatu,Mwalimu alichambua hoja ile na maarifa yao yote ya G55 walishindwa kuhalalisha hoja yao,na hatimae mpaka sasa sijaona hoja mbadala kujisimamia kupika hoja ya Mwalimu na wahusika wa matayarisho ya utetesi wa kile wasicho kiamini walijichimbia chini kama Mbuni mpaka kesho. Leo hii [Sijui Mwanakijiji hotuba hii imetoka lini?itabidi utamwabie imetolewa lini?] eti bado Kiongozi asimame mbele ya haraiki kubwa kama ile ya wananchi na kusema SI MUUMINI WA SERIKALI ANAYOITUMIKIA HALAFU MABOSI WAKE [IMINI WAKUBWA WAKE] WANAMTIZAMA? , WANAMCHEKEA?, WANAMWANGALIA? ,WANASTAAJABU?, WAMEFURAHISHWA?, WAMEPENDEZEWA? hata sijui Rais Jakaya Kiwete na Mwenize Rais Sheni wanasubili nini kuitisha kikao cha zalula tusikie kwenye Bomba kuwa huyu jamaa karudi maskani wao kama CUF wajipange kutafuta namna ya kusimamia hoja wanayoiamni.

Hivyo ili nalo likipita basi tena!!!!Manake kitendo cha kiongozi aliyeko serikalini kusimama mbele ya hadhara na kusema NINASIMAMIA NISICHO KIAMINI, kwayo hilo ni dharau kwa waliomteua haijalishi ni MWAFAKA,kwakuwa HAKUNA MWAFAKA usiokuwa na MAKUBALINO [AGREEMENT].Pia kama kulikuwa na makubaliano IWEJE MWINGINE AJE BAADAE KUSEMA SIVYO TULIVYO KUBALIANA.WANACHI TUELEWEJE KUWA ALIYEMWALIKA MWENZIE NDIYE ALIYEJIPENDEKEZA KUKUBALI YA MWENZIE INAMAANA BASI SERIKALI YA MAPINDUZI YAA ZANZIBAR NDIYO INAYOTAKIWA KUFUATA UUMINI WA SEIF AU SEIF KUFUATA UUMINI WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

NA HAKIKA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO INA SABABU TOSHA YA KUMWAMBIA KWAHERI AKSANTE TUTAKUTNA KWENYE SANDUKU LA KURA YA MAONI, KWA KUWA KILA MTU ANAKUMBUKA SPEECH BY THEN NZURI NA FUPI KULIKO ZOTE TOKA KWA MTEURE BWANA SEIF AKIISIFIA NA KUISIFIA ZANZIBAR HII ANAYOITUMIKIA NA SASA BAADAE TENA LEO ANATWAMBIA WANANCHI WA JAMUHURI YA MUUNGANO KUWA SIYO ANAYOIAMINI.

TUFIKE SEHEMU WATU WATEMBEE KWENYE YALE WANAYOYAAMINI!!NINA IMANI KUWA KAMA ANGEKUWA SI MUUMINI KWANINI ALISAINI MWAFAKA???????!!!!.BINAFSI SIPENDI USALITI, SIPENDI ULAGHAI NA UNAFIKI!!!!

Naamini binafsi unaweza uka na msimamo wa jambo lako juu ya wengine na msimamo huo wa weza kuwa na maana sana kwa jamii.Lakini wewe binafsi pekee yako unaweza kuwa ndiye unaeiona hiyo njia na unapaswa kuwaongoza wenzio kuiona hiyo njia kama Kiongozi.Lakini ukiwa kama kiongozi wa kuonyesha njia kuna gharama zake ambao zitakugharimu wewe mambo mengi muhimu sana.Binafsi uwa nakubaliana na matokeo yafuatayo katika kuipima dhamira unayotaka itokee katika kupigania unachokiamni.

1: Ukubaline kupigania unachokiamini mpaka tone la Mwisho [USHINDI]
Hapa ni pale kiongzoi anapoamua kusimamia kile anachoamini mpaka kieleweke kwa style nyingi nyingi,ikiwemo kufungwa,kunyanyaswa,kupewa hongo ya madaraka, fedha, kuathiliwa kisaikolojia, kubezwa, kuonekana hufai kwenye jamii. Na haya ufanya na wale walio upande wa pili wanaoshindana na kuipinga imani yako kuwa haifai kuwepo katika jamii husika.Lakini naamini kuwa kama unaimani na maono yako [Intuition] dhidi ya hicho unachokiona kama kiongozi basi ukisimamie kama wongozo wa nature [GOD] unavyokusukuma na nguvu hizo zitakuwa upande wako [Ndio maana kwenye speech yake anasema kwa kumtamka Mungu!!!Ingawa kwa hapa simaanishi hicho alichokitamka yeye kwangu mimi naona kaande kinyume chake,kwa kuwa angeyasema hayo huku akiwa amekataa kiti cha umakamu kwa kuwa walishindwana kuelewana kwenye mwafaka akiamini hayo aliyokuwa anayasema huyo Mungu ninayemwamini mimi angekuwa upande wake na angeshinda kwa mujibu wa imani yake].Kwa kusimamia upande huu wa kusimamia unachokiamini mpaka dakika ya mwisho unajitoa kwa mengi,kiasi kuwa unaweza hata kutengwa na familia yako kwa sababu ya imani hiyo na hatimae baadae jamii itakuja kufunguiwa na kujua ulimaanisha nini na hapo ushindi mezani.

Mfano wa haya ni Junior Martin Luther King {USA-I have a Dream, ambayo mkewe Colleta King aliishuhudia na Mungu akampa ushuhuda uko aliko alimthibitishia kuwa aliona ndoto yake hiyo. Mandera, alifungwa miaka mingi sana 20 na ushee, Nyerere aliiacha kazi,maisha ya familia yake yakawa matatani ajui watoto wake na mkewe watakula nini?Na wengineo wengi walio simamia dhamira ya ndani ya mioyo yao wakiwa kama ni viongozi wa ngazi yoyote ile iwe ni ya kifamilia, uko, jamii, Taifa n.K

2:Ushindwe Kupigania dhamira unayoimani na hivyo ujiunge na washindani wako [IF YOU CAN DEFEAT THEM JOIN THEM]
Hii ni pale unapokuwa na msukumo wa dhamira na unapoingia kwenye mapambano ya kudai imani au uumini wako huo kuna sehemu unakumbana na vikwazo na kwa jinsi ulivyo unashindwa kustahimili vikwazo, kama mateso, kukosa chakula, kuteswa kisaikolojia, kuchekwa na mengineyo basi unaamua kuachana na unachokiamini na kujiunga na humo unakosukumwa na upinzani wako.Ukifika huko wapaswa ukubali kufanana na sura ya uliowakuta huko [Ancient wanasema ufika Rome uongea kama Romans wanavyoongea na kutenda].Kamwe ukifika huko uwa umefanya maagano na dhamira /Ndoto/Intuition yako kuwa sio mwenizo tena na kuwa huwezi kuitimiza.Ndio maana wenye akili zao uwa wanaita USALITI.Na utakapo taka kuludi tena upande w pili [2] yani ulikokuwa mwanzoni unakuwa na dhambi nyingine ambayo ina hatari kubwaa sana.

Ebu tuone Picha hii itaishiwa wapi!!!

.
 
Muungano wa nini?
  • Wana bendera yao
  • Wana Rais wao
  • Wana wimbo wa taifa lao
  • Tulivyo mazezeta tunadhani ni ule muungano wa mwanzo!
  • Mbunge anawakilisha kama watu 150 tu wakati bara mbunge anawakilisha maeru ya watu
  • Wazanzibar wanasomeshwa bure na pesa ya muungano wakati wa bara mnapewa kama mkopo
  • Hivi tumelogwa?
Nawashauri vunjeni muungano waache kula vya muungano bure
 
Seif ni sumu ya mamba. Anaona Zanzibar ikiwa nchi itampunguzia fursa za kueneza sumu yake katika Tanganyika. Hana maana yoyote yenye tafsiri nzuri kwa Tanzania.
 
Kwa nini? Wananchi wakiamua haliwezekani?

Mimi naamini ni suala la hoja tu, hakuna haja ya "kuwalazimisha" wananchi muundo ambao "watawala" wanaona unafaa na wananchi hawautaki.

wananchi hao hao ambao hawajapatapo kukiweka chama cha upinzani madarakani na kwa busara zao wakaridhia Gnu ili kuzima mizizi ya fitna . Don't - under estimate, under rate- them.
 
hivi we mzee mwanakijiji zile harakati zako za ccj,cck,ccx na cheche zimeishia wapi?!!!

Saivi amelipwa ajaribu kufitinisha wazanzibari, lakini amefail totally mana anaongea pumba tu! Hivi ajiuzulu kisha nguvu apoteze nguvu totally?

Mzeemwanakijiji unatakiwa uwe mwanamjini inaonekana kijijini mnalima zaidi kuliko kusoma, mjini shule, kuwepo kwake katika madaraka ndio kupata nguvu shinikizo la wazanzibar. Kajipange upya kijijini kisha ndo uje mjini
 
Muungano wa nini?
  • Wana bendera yao
  • Wana Rais wao
  • Wana wimbo wa taifa lao
  • Tulivyo mazezeta tunadhani ni ule muungano wa mwanzo!
  • Mbunge anawakilisha kama watu 150 tu wakati bara mbunge anawakilisha maeru ya watu
  • Wazanzibar wanasomeshwa bure na pesa ya muungano wakati wa bara mnapewa kama mkopo
  • Hivi tumelogwa?
Nawashauri vunjeni muungano waache kula vya muungano bure
Inasikitisha kwamba wakati wazenji kila siku wanataka kujitoa kwenye muungano, watanganyika wako kimya kana kwamba wao wameridhika na mfumo huu wa muungano. Kwa nini na sisi tusiitake Tanganyika yetu tuakaachana na hawa kina Seif?
 
Hawa jamaa na nchi yao mi nilishawaacha zamani. Nothing of/from them ever concerns me.
 
Mi nadhani ni vema tukauvunja tu huu tunouita muungano coz hawa wenzetu wa Visiwani, pamoja na kuwa na mamlaka yao (niko tayari kusahihishwa), bado hawaishi kulalamika! Kuendelea kuwang'ng'ania ni UJINGA......
 
kweli dhana ya muungano wa mkataba na huu mkataba waliopo zinapingana.Sijui maalim ana kichaa au ni ule uhaini unamtafuna?Au ndio kunogewa na mkataba walio nao na CCM?
 
Seif ni sumu ya mamba. Anaona Zanzibar ikiwa nchi itampunguzia fursa za kueneza sumu yake katika Tanganyika. Hana maana yoyote yenye tafsiri nzuri kwa Tanzania.

Wewe utakuwa mwana CCM - Serikali 2. CHADEMA nao watakuwa sumu ya nini maana wanataka serikali tatu?!
 
Chuki dhidi ya Wazanzibari at work practically!!! Kimenuka kwenu katu hamuwezi kutufitinisha tena. Wacheni majungu yatawamaliza tumieni muda kuitafuta Tanganyika yenu.

teh teh teh...kwa mfano leo muungano ukafia hapo chini paa, nani atakuwa mhanga mkubwa wa kifo hicho?
 
kweli dhana ya muungano wa mkataba na huu mkataba waliopo zinapingana.Sijui maalim ana kichaa au ni ule uhaini unamtafuna?Au ndio kunogewa na mkataba walio nao na CCM?
Kwani kuchangia hoja mpaka utukane ndio hoja ionekane ina nguvu? Hayo ni maoni yake na wewe kama unayo ya kwako weka mkutano kama alivyofanya yeye! Kwani wewe unataka serikali ngapi?
 
Huyu Seif ndio mwanzo wa Matatizo yaliyo mengi ya Wazanzibar maana haeleweki sasa kwa nini amefunga ndoa na CCM? Wazanzibar huyu mtu mwogopeni kama ukoma eti.
 
Nielewe mkuu,

Seifu kuwa sumu ya Mamba haitokani na uwingi wa serikali ama uchache. Yeye anataka eneo kubwa zaidi la kueneza sumu yake ambayo mwalimu Nyerere aliingudua, akaamua kumbana pini. Sasa anajua wenye macho hawapo na hiyvo anauwezo wa kuieneza bila pingamizi kubwa. Lakini kama zanzibar itakuwa nchi, basi uwezo wake wa kuisambaza utakuwa umedhoofishwa maama Ki-Zanzibar hicho si mkoa mmoja tu hapa Bongo? Seifu hana nia nzuri yoyote kwa Tanzania.

Elewa hivyo. Sijasema ni mfumo gani wa Muungano ningependelea. Nimeongelea nia ya Seifu katika hicho anachoonyesha kukipigia debe.
 
Mi nadhani ni vema tukauvunja tu huu tunouita muungano coz hawa wenzetu wa Visiwani, pamoja na kuwa na mamlaka yao (niko tayari kusahihishwa), bado hawaishi kulalamika! Kuendelea kuwang'ng'ania ni UJINGA......

Hii ni rahisi sana. Watu wa Tanzania bara wapeleke mapendekezo kwenye tume ya katiba kama wanavyofanya wenzao wa visiwani. Kura ya maoni ikija wengi watapitisha mapendekezo na kupata kile ambacho kila upande unakitaka.
 
Nielewe mkuu,
Elewa hivyo. Sijasema ni mfumo gani wa Muungano ningependelea. Nimeongelea nia ya Seifu katika hicho anachoonyesha kukipigia debe.

Kwa mawazo yako ni ipi nia ya Seif - maana mwenzetu huenda ukawa una elimu za mitume!
 
mbona ndo yake na mkewe sio ya mkataba? kwamba waonjane, moja akimuona mwingine kesha choka basi anaanza.
hii ni kwamba wakipata nafuu za kiuchumi, basi muungano hauna faida, wakizidiwa basi wanataka muungano.
 
Seif kaapa hataonoka umakamo wa raisi, ilaa alawashauri jussa na mansour wajivue madaraka ili waijenge uamsho
 
Kwani kuchangia hoja mpaka utukane ndio hoja ionekane ina nguvu? Hayo ni maoni yake na wewe kama unayo ya kwako weka mkutano kama alivyofanya yeye! Kwani wewe unataka serikali ngapi?

kuhisiwa kuwa na kichaa si matusi kuitwa kichaa huku ukiwa is kichaa ndio tusi.

Nataka serikali 1 au 3.Mkutano wanini?Siwezi kuwa iressponsible na abusive kama seif.Ana abuse imani ya wazanzibar mara nyingine tena.Aliwaponza wakauwawa sasa wamepotea naively halafu akawatoa kwa kuingia mkataba na CCM nadhani akanogewa namikataba kama si uhai unamsumbua.
 
Back
Top Bottom